Salaam,
Leo Februari 29, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi...
Zitto ni mnafiki na kila tukio kwake ni fursa. Pili ana udini sana. Yeye kana alisoma chini ya nwembe sio kila mtoto nchi nzima alisomea chini ya mwembe. Kana hakuvaa shati labda ni umaskini wa babake. Nakumbuka zitto mpaka akiwa chuo kikuu akikuwa anasaidiwa na Mbowe sasa umaskini wa kwao asimtupie Nyerere lawama. Nitaeleza kidogo.
Mimi nimeanza shule mwaka 1971 (kabla Zitto hajazaliwa) na nimesomea shule nzuri na nilivaa uniform safi tu ( chou enlai). Nyerere alipoanzisha vijiji vya ujamaa kipaumbele kikubwa ilikuwa kila kijiji kiwe na shule yake ya msingi; hivyo wanakijiji walikuwa wanafanya kazi za maendeleo mara 2 kwa wiki ikiwemo kujenga shule na serikali ikitoa vifaa. Mwinyi hakukuta nchi imesimama kabisa. Tanzania katika hatua za maendekeo ilikuwa inafanya vizuri hasa sekta za elimu na afya. Vita ya Kagera ilipotokea ilibidi nchi kipaumbele kiwe kuihami hata kama angekuwa nani bado angelazimika kupigana vita.
Baada ya vita nwaka 1979 pamoja na matatizo ya uchumi ya dunia yaliyosababishwa na kupanda sana kwa bei ya nafuta, kuporomoka kwa bei ya mazao yale nane tuliyokuwa tunayategemea sana kuuza nje nchi iliyumba llakini kulikuwa na jitihada zinachukuliwa ili kupambana na hali hiyo. Sokoine mwaka 1982, 83 na 84 ndiye aliiyeanzisha mqgeuzi ya kiuchumi, aliruhusu daladala zibebe abiria zikaanza aina ya daladala (chai maharage) kenta ziligeuzwa daladala. Pia aliruhusu wutu binafsi wenye pesa nje ya nchi walete bidhaa na hawataulizwa wamepata wapi hela. Bidhaa zikaanza kumiminika nchini.
Mwinyi alipoingia nadarakani aliendeleza mageuzi yaliyoanzishwa na Sokoine yeye akakubaliana na nasharti ya IFM ambalo kubwa lilikuwa kushusha thamani ya shilingi, kubinafsisha nashirika ya umma, kutoza ada kwenye huduma za afya na elimu nk.
Jina la Ruksa lilianza ple waislamu siasa kali waliipovunja mabucha ya nguruwe Dsm . Mwinyi wakati huo alikuwa Zanzibar ndipo baadae akahutubia akasema anayetaka kula chura ruksa akataja na nambo mengine ambayo mtu binqfsi ruksa kufanya ( alikuwa anapinga hilo la kutaka kulazinisha watu wasile nguruwe)
NB: Mwinyi hakumaliza mageuzi yote, alipokuja Mkapa akaendeleza Mageuzi mbalimbali.
Mwanzilishi kabisa wa mageuzi kama Zitto anatafuta wa kumpa credit basi ni waziri mkuu Sokoine.