Je, utamkumbuka Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa mambo gani?

Je, utamkumbuka Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa mambo gani?

Sisi tulijaaliwa kuishi awamu zote za uongozi tutamkumbuka kwa aliyoyafanya ile awamu ya kwanza ya uongozi wake
Sisi wa toka utawala wa Mwalimu tutamkumbuka Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi kwa meni

1: Ndiye aliyetufungua watanzania macho kwa kuweza kusafiri nje na kununua vitu pamoja na kuanza kujenga.
2: Ndiye chachu ya kuwepo private sector na hapa neno Ruksa ndiyo hasa lilipoanzia .

Huyu mzee hakuwa na hiana na mtu na alikuwa mpole na nakumbuka nilipokutana naye nikiwa mdogo alinishika mkono na kuniambia kwa nini nilijificha sikwenda msalimia kumbe nilikuwa mchafu mzee alinichimba biti nisisogee kumuona raisi basi akajibu mzee huyu hapana wewe ni rafiki yangu na tulikuwa wawili hakutuachilia mikono yetu alizunguka na sisi pale mikocheni kwenye nyumba yake wakati huo anajenga. Tokea hapo kila alipokuwa anakuja alikuwa anapenda nikamsalimie nami nilifanya hivo.

Mzee huyu nilibahatika soma na wanawe na kimaadili kiukweli amewalea katika misingi ya kinidhamu mno huwezi jua kama walikuwa ni watoto wa Raisi. Na hata tulipobahatika fika Ikulu alikuwa anapenda sana kutufundisha kiswahili.

Huyu mzee alikuwa anatukanwa sana lakini alikuwa ni kiongozi ambaye anasamehe na maisha yanakwenda mbele.

Hata waseme vipi huyu ndiye aliyetutoa tongotongo machoni
 
Salaam,

Leo Februari 29, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi. Soma: Thread 'Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia' Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Kunako Utawala wake Hayati Mwinyi alifanya mambo mengi na kuacha historia kupitia Utawala wake na sera zake.

Mimi nitamkumbuka zaidi namna alivyoifungua nchi kupitia sera yake ya ruksa Miaka ya 1990.

Je, wewe utamkumbuka Mzee wetu huyu kwa mambo gani hasa?

Loliondogate
 
Kuna zee la ovyo lili dinya hadi mama yake mzazi ....ila ndiyo hivyo wema hawafi
 
Salaam,

Leo Februari 29, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi. Soma: Thread 'Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia' Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Kunako Utawala wake Hayati Mwinyi alifanya mambo mengi na kuacha historia kupitia Utawala wake na sera zake.

Mimi nitamkumbuka zaidi namna alivyoifungua nchi kupitia sera yake ya ruksa Miaka ya 1990.

Je, wewe utamkumbuka Mzee wetu huyu kwa mambo gani hasa?

Hakuwa na roho ya kutu au fitna. Nakumbuka kisa chake na Waziri mmoja aliyechukua nafasi yake baada ya Mzee Mwinyi kujiuzuru u-Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Kisa kilihusu mzigo wa saruji na mabati. Mzee aliporwa bati zake na saruji, lakini alipokwaa u-Rais miaka michache baadaye, alimteua mtu huyohuyo kuwa Waziri..!
Allah ampunguzie adhabu ya kaburi..."Innallilah Wainnalillah Raj'uun"
 
Nazikumbuka sana ''Chai maharage'. Pia shift mbili kwa shule za day.
 
Nitamkumbuka kwa kutuleteaa waaarabu wa OBC

Kampuni ya kitapeli ya uwindaji
Ambayo SAS HV ndio inawaondoa wamasai kwenye ardh Yao asilia
 
1. Kupenda Dini na Kusali sana.

2. Kupenda Utani na Ucheshi.

3. Kukitukuza Kiswahili na Kujivunia Kukiongea Kiufasaha.

4. Kuridhika na Maisha aliyonayo huku akipenda sana Kula Vyakula vya Kiasili na vya kuutunza Mwili kwa muda mrefu.

5. Kupenda mno Mazoezi hasa ya Kutembea kwa Miguu kwa Umbali mrefu.

6. Huruma,, Kusamehe na kutokiwa na Kinyongo na Mtu hasa hasa Adui.

7. Kutopenda Kujitukuza kama Kiongozi na kupenda Ushirikiano na Watu na kuwa mwepesi Kushaurika na Kujifunza.

Pumzika Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi hakika Mwendo Umeumaliza na huna baya hata kama lipo Watanzania tulishakusamehe Kitambo na Uhai wako huu mrefu ulikuwa ni Zawadi na Faraja kwetu.

Ulale mahala pema. Peponi AHM.
Pia aliweza kusema ukweli hadharani kwa kuzikubali Kaz za magufuli kwamba Wai mwemshindwa kufanya mamb makubwa lkn magufuli wewe umeweza aliyaongeaa hadharani hayo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Salaam,

Leo Februari 29, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi. Soma: Thread 'Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia' Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Kunako Utawala wake Hayati Mwinyi alifanya mambo mengi na kuacha historia kupitia Utawala wake na sera zake.

Mimi nitamkumbuka zaidi namna alivyoifungua nchi kupitia sera yake ya ruksa Miaka ya 1990.

Je, wewe utamkumbuka Mzee wetu huyu kwa mambo gani hasa?

Kipindi akiwa RAIS WA ZANZIBARI aliruhusu gari aina ya "PICK-UP" maarufu kama CHAI MAHARAGE kubeba abiria 🙏🏾
 
"Mzee wetu Mwinyi kaishi miaka 98.
Japo wengi hatujui undani wa maisha yake, ila kwa jicho la Public hakua mtu wa kujikweza, hakua na toxic lifestyle (kama alivyokuwa jpm Mzee wamahasira na visasi kila mahara na kwa kila hasimu wake mpaka kumuua), hakutengeneza maadui, aliishi a simple lifestyle, ila pia hakua na mke mmoja"
 
Ile kashfa ya kuuza Wanyama kwa kupitia Mama Siti, wengi mlikua hamjazaliwa
Kuna familia moja ya waarabu wa Mombasa ( akina Akasha) wauza madawa ya kulevya mmoja wao alikamatwa hapa nchini, mzee Ruksa akamuachia!!
Zakaria Hans Pope ; mfadhiri wa Simba aliachiwa toka jela baada ya mama yake kwenda kumuomba mzee Mwinyi!
Hii ni mifano midogo
ya jinsi alivyokuwa na utu!
Hata hivyo kama alivyokili mwenyewe kwenye kitabu chake, alijutia uamuzi wake wa kuwauzia waarabu Loliondo!! Samia sidhani kama amejaliwa kusoma kitabu cha mzee Mwinyi, ama sivyo asingediriki kuuza bandari zetu!!
Mama Abdul soma vitabu kuepuka kurudia makosa!
 
Katika kitu kikubwa sana ambacho huyu mzee amekiacha na alikifanya ni hali ya unyenyekevu mkubwa sana . Kwa wale wasiojua kama utulivu wa Mwinyi kati ya 1985 na 1990 nchi hii ingeingia kwenye mambo magumu. Baba wa taifa akiwa Mwenyekiti wa Chama so raisi anafanya maamuzi yanaweza kupigwa kwenye chama. Na isotocheze Baba wa taifa akaishia kuandika kitabu ambacho kilionyesha ufa wa uongozi lakini mzee alikaa vyema akiamini kuwa kazi yake ilikuwa ni njema na kama neno linavyosema wema huzidi mabaya. Alikuwa na maadhaifu yake kama binadamu ila ilikuwa ni Tunu iliyoweza kuhimili matatizo mengi sana. Kubadilika kwa hali ya hewa kule Zanzibar ilibidi awekwe kuziba hilo pengo ingawa wazanzibar walimuona ni mbara lakini kutokana na utulivu alihakikisha kuwa wamoja. Kujaribu sana kubadilisha maisha ya kawaida. Ingawa sentensi ya Ruksa inabeba falsfa nzima ya mzee Mwinyi ilitolewa kutokana na baadhi ya watu wakiiamini sana kula nguruwe sio sawa wakaanza kubomoa mabucha hapo kwa Thomas palipo na kituo cha mwendo kasi cha Bucha cha mwendo kasi kwa sasa. Ndipo alitoa maelekezo ya kwa watu waache kula wanachotaka na hili kwa kuwa watu walijua kujua dini na kuwa muisilamu safi wakamwelewa sana na hapo kula Kiti Moto dar ikaanza kuwa sio kitu cha ajabu kwa jiji la Dar Es salaam.
 
Salaam,

Leo Februari 29, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi. Soma: Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Kunako Utawala wake Hayati Mwinyi alifanya mambo mengi na kuacha historia kupitia Utawala wake na sera zake.

Mimi nitamkumbuka zaidi namna alivyoifungua nchi kupitia sera yake ya ruksa Miaka ya 1990.

Je, wewe utamkumbuka Mzee wetu huyu kwa mambo gani hasa?

Loliondo na uwanja wa mpira wa kikapu wa gymkhana
 
Mzee ndio alitufanya tuijue dunia baada ya Nyerere kutukalisha kwenye zama za mawe.
Nyerere aliimairisha utulivo na umoja wa makabila yote akaangukia pua kwenye uchumi.
Mwinyi alifungua madirisha yote basi yakaingia mazuri mengi na mabaya vile vile
 
Wanyama tulivyokuwa nao wengi halafu rais achukue wachache kuuza inakuwa ishu ,
Watu wanaroho ya kwanini sana
Yule mama aliefungwa iringa kwa Nyama ya swala ila jiwe alieibiwa tausi wa mjengoni hakuguswa
 
Pale Mzee aliteleza,Ila mpiga Kofi naye akili Hana,ule ushauri ni sawa na polisi kushauri wezi njia nzuri na salama ya kuiba,Nina Imani mzee alifanya toba
Yule dogo aliempiga kofi mzee Mwinyi alikuwa na matatizo ya ki afya alisona tabora boys lakin mwishoni kama alichanganyikiwa vile dini ilimkaa vibaya sana
Region is the opium of the masses dogo alikufa kitambo sana nafikiri alikuwa na matatizo mengi
 
KC mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema Darasa la 1-3 alisomea chini ya Mwembe na wakati huo Walitumia Sanda kushona mashati ya Shule kule Ujiji Kigoma

Ila alipoingia Rais Mwinyi mambo yakabadilika badala ya Sanda wakaanza kuvaa tatroni

Credit: Clouds TV
 
Back
Top Bottom