Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
UVIKO-19.
 
Mimi sijawaona na kama ilitokea basi lete ushahidi au kawashtaki walio tenda huo unyama.....
Kama una ushahidi funga bakuli lako..
Nikawashtaki waliofanya unyama wakati waliofanya unyama ni pamoja na hao wanaohusika na kuprocess mashtaka?Kwa nini kesi ya Tumbili nipeleke kwa Ngedere?
 
Si serikali ileile ya CCM au unakiri hapa kuwa hampo competent kuendesha nchi?
Kwamba mimi ni CCM!! Hata kama ningekuwa CCM, kauli na matendo yangu hayawakilishi CCM. Chama ni kikubwa kuliko mtu binafsi.

Yawezekana hoja yako kwenye hivyo vyama vya upinzani ikawa sahihi na mashiko kwa kuwa chama ni mtu na mtu ni chama
 
Yaani Mama Samia mpaka amekuwa Rais si alipitishwa na CCM ina maana mlimuweka pale kwa vigezo leo hii akivurunda mnajifanya mnalalamika kwani sio CCM ile ile??

Ndio maana nmekuuliza kukiri kwamba Mambo yameharibika means unakubali kuwa CCM imeshindwa kuongoza coz ndio imemuweka pale.

Huwa mnajitapa hapa kwamba system cjui inafanya vetting mara Ikulu takatifu ndio maana upinzani hawapewi nchi and all that crap.... Ssa hyo system na CCM mnayosifia kila siku ndio imewaletea Samia. Sasa mnalia lia nini?? Mnajifanya kma hamumtambui hivi utadhani ametokea CUF sijui

Tuache unafiki huwezi tenganisha CCM na failure za Rais
 
Uwiano uliotumia hauna mantiki linapokuja suala la utendaji. Hata kwenye kaya (household), ambayo ni taasisi ndogo kabisa duniani, mifumo hufanana ila ubora wake hutegemea matendo na mahusiano ya wanafamilia ambao ndio taasisi yenyewe
 
Kwahiyo mfumo wa CCM ni mzuri ila kiongozi waliomchagua ni Mbovu?? So unakubali kwamba CCM ni incompetent kwenye kuchagua mtu wa kusimamia mfumo??
 
Ubungo unapita haupiti? Tazara unapita hupiti? Mbezi unapita hupiti? Hospital unaenda huendi? Vyeti feki vipo havipo? Msoga gang walikuwepo au walidhibitiwa? Bwawa la umeme linajengwa au la?SGR ipo au haipo? Ni kazi ngumu sana kuongoza washenz washenz wasiojua nchi inapaswaaa kuwaje? Democrasia unaijua ww? Niambie nchi yenye democrasia hata moja duniani? Watu kama nyie ni kuwalima shaba tu pumbavuu mnatucheleweshea maendeleo..tazama sasa hv mswahil anachofanya..
Huna hoja unajamba jamba tu kama bata,
 
Mwinyi alikuwa akipiga ndogo ndogo mwanawe afikiriwe urais Zenj.
Haihitaji akili kubwa kuelewa hilo!
 
Sijawahi kuyazingatia hayo maneno ya mwinyi kwa sababu kwa uzee alionao naona kabisa kuna frequencies haziko sawa yaani ni kama kunguru katua kwenye antena tena ile ya vimwiba 🤗🤗
 
Ni kweli kabisa Magufuli amepiga kazi kubwa sana ndani ya muda mfupi ukilinganisha na wenzie ndani ya muda huohuo.
 
Back
Top Bottom