Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Nakumbuka mwaka fulani alikuwa waziri, Nauli ya kivuko cha Magogoni ikapanda hadi Tsh. 200, basi bana, wanakigamboni wakacharuka kupinga ongezeko hilo, JPM a.k.a Chuma kikawanyookea bila kupepesa macho kuwa... kivuko cha Busisi Mwanza wanalipa 400 na hawalalmiki, basi ambaye hana hiyo 200 akaogelee! Tangu hapo kimyaaa! [emoji28] Pumzika kwa amani mwamba!
 
Dr alituaminisha kuwa nchi ni tajiri Wala hatuna haja ya kuomba mikopo Tena akaenda mbali Sana kuwa sisi tuna paswa kutoa misaada kwa mataifa hayo ya nje, na ukweli watu wengi tukaamini kuwa nchi imepata mkombozi.

Kinyume chake Dr ameenda zake na huku katuachia madeni makubwa.

Kumbe Dr alikuwa anakopa Tena mikopo ya kibiashara ,mikopo yenye riba , mikopo ambayo mingi ilikuwa inaanza kulipwa baada ya miaka miwili hadi mitatu baada ya kukopwa.

Dr ameacha madeni, ambayo sasa yana muingiza mama kwenye lawama, Kila sehemu ukipita utasikia hali ngumu sijui mama anatupeleka wapi.

Ukweli usio pingika ni kwamba Mama anafanya kazi njema na iko wazi, wapo wanao jifanya kuwa hawaoni Ila ukweli ni kwamba waliishi kwenye uongo wa Dr.

Swali ni hili hivi kwanini Dr aliamua kututenda haya?
 
NAONA MAKABURI YANAFUKURIWA KWA KASI SANA

Mkuu ukisema haya kwenye kijiwe cha wamachinga watakugawana kama andazi
 
Ni wazee wa magomeni mapipa, mikumi, mwembechai, makuti, kagera, mburahati, Agentina hadi manzese wanasema ni kama vile hayati Magufuli aliwaonjesha asali kwani sasa maji hayatoki tena.

Wazee hao wamemuomba RC Makalla kulishughulikia tatizo la maji na kulimaliza kama alivyolimaliza tatizo la wamachinga na sasa jiji limekuwa safi kila mtaa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Njaa mbaya sana
 
AA35EB81-696B-497D-B973-553FBF4576C7.jpeg
 
Back
Top Bottom