Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Alikuwa mwanaume pekee aliyeweza kusimamia nchi nzima bila kiumbe yeyote kunyanyua shingo kwa kifupi San zote tulifyata mkiaa
kutumia madaraka yake vibaya kutisha, kuumiza na kupoteza watu wote ambao waliokwenda tofauti ya mtazamo wake.
 
Putin ameshadhibitiwa kiuchumi kwa 75% lakini mzunguko umekuwa mkubwa mno.

Palihitajika Kiongozi mfano wa shujaa Magufuli anayeweza kusema na kutenda hapo hapo lakini kwa bahati mbaya sijamuona pale Ulaya, wote wanaogopa baridi.

Kiukweli Magufuli alikuwa Kiongozi wa level ya sayari nyingine aisee!

Mungu wa mbinguni mpumzishe kwa amani John Magufuli!
 
The kind of leaders watu weupe hawapendi wawepo Afrika!! The ones that can be easily compromised and can compromise their national interests!!
 
Putin ameshadhibitiwa kiuchumi kwa 75% lakini mzunguko umekuwa mkubwa mno.

Palihitajika Kiongozi mfano wa shujaa Magufuli anayeweza kusema na kutenda hapo hapo lakini kwa bahti mnaya sijamuona pale Ulaya, wote wanaogopa baridi.

Kiukweli Magufuli alikuwa Kiongozi wa level ya sayari nyingine aisee!

Mungu wa mbinguni mpumzishe kwa amani John Magufuli!
Kwa kweli Magufuli alikuwa jasiri hadi kupora rambirambi za maafa ya tetemeko la Kagera!
 
MR BEN una mawazo ya kitoto sana wakati mwingi
Putin ameshadhibitiwa kiuchumi kwa 75% lakini mzunguko umekuwa mkubwa mno.

Palihitajika Kiongozi mfano wa shujaa Magufuli anayeweza kusema na kutenda hapo hapo lakini kwa bahti mnaya sijamuona pale Ulaya, wote wanaogopa baridi.

Kiukweli Magufuli alikuwa Kiongozi wa level ya sayari nyingine aisee!

Mungu wa mbinguni mpumzishe kwa amani John Magufuli!
 
hii vita inaenda kubadilisha kila kitu tulichokuwa tunajua...........stay tuned
 
Magufuli alikuwa kichaa. Sijui ni uchawi yaani akili kama Ile alikuwa rais!

Makosa ya 2015 yasirudiwe.
 

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.


Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
Nitamkumbuka kwa ushamba wake
 
Salaam ziwafikie wote.

Leo nimeamka nikiangalia mitandao ya kijamii fb,whatsapp n.k. nikaona jinsi Marehemu anavyosifiwa kuliko chochote kile. Nimewaza sana kwa kuona baadhi ya wasifiaji wakuu ni wafanyakazi wa serikali ambao kwa miaka 5 ya uongozi wa bwana yule hawakuwahi kuona nyongeza za mishahara, za kupanda madaraja wala za kuhamishwa kikazi nikarudi kwa waliokuwa vyuoni ambao wengine wamekatwa makato makubwa ya mishahara kulipia mikopo waliyosomea.

Kundi lingine la waimba nyimbo za sifa kwa marehemu ni wale ambao ndugu zao walicharazwa marungu na polisi na kubambikiziwa kesi za ajabu wakitishiwa kupigiwa mpaka shangazi zao, wengine ni wale wa vyombo vya habari ambao walitishiwa kufutiwa leseni na wengine walifutiwa kabisa.wengine walivamiwa kabisa kwenye vituo vyao na silaha za moto na engine waliokuwa na Youtube channels walitakiwa mpaka milioni 1 kupata leseni.

Kundi lingine ni waliofilisiwa na kujaziwa kesi za uhujumu uchumi, waliotengenezewa vitambulisho vya ujanjaujanja hela zikapigwa n.k.

Nimewaangalia waimba mapambio wote leo hii nikajiuliza hawa waliishi Tanzania wakati yule Bwana alikuwepo ama walihadithiwa? Japo maisha hayajabadilika sana lakini kuondoka kwa yule Bwana ilikuwa baraka najitoa kwenye huu unafiki niuonao. Nchi ilifika mahali ukitoka kwako una hofu ukimuona mtu usiyemfahamu anakuangalia.
 
Ningekuwa Mungu, wapagani wote wangeiona pepo, na wenye dini karibu wote(wakiwemo viongozi wao) ningewatupa Jehanamu.
 
" Jifanye mjinga siku ipite" Waswahili

Unafiki uliotukuka ni sehemu ya maisha ya wana CCM.
 
Ndio naamka saivi baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani kwa mfuriko wa status za jana zinazomkumbuka chuma. Kumbe status zina expire 24 hours 😀😀😀😀

Baada ya usingizi mzito nikatoka na wazo langu, huyu jamaa ananyota ya kupendwa.

Nilichogundua ukitaka kuwini siasa za bongo saivi nikutembea nyuma yake. Kutembea nyuma yake ni kufuata sera zake.

Nimekata shauri wakuu, natembea nyuma ya Chuma saivi.

Ngoja nikanywe chai sasa.🤗🤗🤗🤗🤗🤗🤗🤗🤗🤗🤗🤗
 
naona umeiadhimisha siku ya kulala duniani vyema kabisa.
 
Back
Top Bottom