Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Wananchi wengi ambao ni wa kawaida wana mmisi sana Magufuli.
Bahati mbaya mafisadi na wanasiasa uchwara ambao bahati mbaya tena ndiyo wanacontrol habari wanalazimisha picha ya kuto mmisi au kujenga chuki kwa Magufuli.

Ujiulizi kwa nini mpaka leo hii zaidi yanmiezi 10 toka amefariki bado kuna kampeni kubwa ya kumchafua? Watu wanaacha kujadili mambo muhimu yanayojiri wanatumia pesa kuset agenda za kumchafua au kumdogosha magufuli.

Kama watu hawa mmisi kwa nini kila siku mnatunga ’visred’ vya kumchafua? Sababu mnajua moto wake haupoi, na amekaa kwenye roho za walio wengi, hivyo bajeti kubwa na nguvu kubwa hadi leo zinaelekezwa kwenye project chafua Magufuli.

Na hii ni sababu mnajua you cannot do better than him, kwa hiyo pona yenu mnafikiria ni kuchanganya uelewa wa wananchi juu ya Magufuli.

Matatizo yote ambayo Magu aliyamudu yanaibuka lakini yanapambwa kwenye media kama hayapo vile au yanastahili kuwapo! Badala ya kupigia kelele haya wafitini wanaendeleza kumchafua Magu!
  • Mgao wa umeme umerudi, gharama za kuunganisha umeme juu
  • Bei za bidhaa zimepanda kwa kasi ya ajabu, hakuna anayejikuna. Wananchi wa kawaida wanalalamika sana, lakini vyombo vya habari kwao siyo news sababu ”who pays the piper calls the tune”
  • Ubovu wa huduma za kijamii na kutojali wananchi kunarejea
  • na mengine mengi!
 



we lost a visionary president.lakini mtanzania mvivu hawezi kuelewa.

lazima philosophy ya kujitegemea iendelezwe.Binafsi sipendi misaada japo twaonekana maskini.sisi siyo maskini.tuna rasilimali nyingi za kujikwamua japo siyo kwa kuhamisha watu.


^Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndicho chombo chetu kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini. Ni ujinga vilevile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe.^ ~ JKN.
 
Kwa uwezo wake mdogo wa uongozi. Hakuwa na maono ya kiuchumi, kidiplomasia, na kiusalama. Aliligawa taifa kiukabila na kisiasa. Kimsingi alikua mtu hatari kwa mustakabali wa umoja wetu wa kitaifa. Huyo marehemu ni historia mbaya kwa taifa letu.
 



we lost a visionary president.lakini mtanzania mvivu hawezi kuelewa.

lazima philosophy ya kujitegemea iendelezwe.Binafsi sipendi misaada japo twaonekana maskini.sisi siyo maskini.tuna rasilimali nyingi za kujikwamua japo siyo kwa kuhamisha watu.

Duh! We huyu laana bado tu wampigia promo!!
Nyie ndo mnasababisha tusisahau machungu tulopitia
 
Ben Saanane
Mwangosi
Kupigwa Risasi Lissu
Korona
Makondakta
Miili kuokotwa kwenye sandarusi cocobeach
Bastola hadharani kwa Nape
Uvamizi Clouds
Uchaguzi/uchafuzi wa 2020!
japo sisapoti maujaji ya mtu ,lakini ukifanya mizaha mbele ya mfalme sharti uliwe kichwa.Kuna wafrica wengine ni kama funza .
 

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.


Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
watu kupotea.. !!
 
Back
Top Bottom