Ukali wake ulisaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzembe kwenye taasisi za serikali, lakini sio huyu mama wa kuparwa anayesema tujiandae kwa maumivu ya bei ya mafuta kupanda, ndio maana PM anajaribu kufukia hayo mashimo ya udhaifu wake.
 
Democracy, democracy sasa mbona nchi za kifalme hakuna democracy lakini wameupiga mwingi tu kimaendeleo?

Nchi zinazoendelea ni kichwa cha mwendawazimu kuhusu kasi ya maendeleo kiuchumi.
 
Wezi walimsumbua sana Magufuli. Walipobanwa wakapiga kelele kubwa sana. Bahati mbaya watu wa kawaida wakaunga kupiga kelele bila kujua kwanini wenzao wanapiga kelele.
 
He is My sons's legacy

Ametusaidia Mambo mengi.

JPM kafanya mengi makubwa kuliko Rais yeyote aliwewahi pita nakosa la kuandika kabisa vidole vinatetemeka, Nimelia Mimi leo

Naogopa nchi yetu inarudi shimoni

MUNGU TUANGALIE TENA WAJA WAKO
Au ww ndo komredi Musiba?!!!
 
Ni kweli inawezekana bado mna uchungu na maumivu makali sana mioyoni lakini hasira zenu nyie watetezi wake kuwakasirikia waliokuwa wakosoaji wake hazina mashiko.

Watetezi wa legasi kejeli na hasira zenu hazina mashiko kwa sababu wakosoaji wake wakubwa na wa wazi hawahusiki na kuondoka kwake, aliondoka au alitwaliwa muda wake ulipofika.

Hata kama bado angekuwepo leo wakosoaji wake wa wazi wangeendelea tu kumkosa, hiki wanchofanya sasa ni muendelezo wa kile walikuwa wakifanya muda wote.

Hasira zenu zielekezeni kwa wale waliokuwa wakimsifia mdomoni huku wanamchukia mioyoni mwao. Hao ndio watu sahihi wa kuwaelekezea ghadhabu yenu.
 
Wenye hasira ni wale waoga woote ambao wamesubiri Magufuli afariki ndio waanze kumtukana.
 
Ama kweli muosha naye hatimaye huoshwa! Baada ya kutamba sana akiwa madarakani na kusababisha madhila kwa watu wengi hatimaye amekufa na sasa anaoza!

Nianze maelezo yangu kwa kipande cha shairi:
Nchini kulichafuka, barani na baharini, Kitini ameshatoka, yule bichwa mjivuni, katunusuru Rabuka, na myama wa porini!"

Alikua akitamba kutumbua watu naye katumbuliwa 'moja kwa moja'... I think operation ya 'kutumbuliwa' kwake ilifanywa bila ganzi!..._ Just kidding 😂.

Ni zaidi ya siku 400 sasa ( miezi 14) tangu bwana John Pombe Magufuli afe, azikwe na aanze kuoza! Kifo cha huyu jamaa ni funzo kubwa kwa Watanzania na kwa kweli tumshukuru Mola kwa kutunusuru na jinamizi la uongozi mbaya na hofu iliyokua imetanda nchini tangu Jakaya aondoke..... Hakika kuondoka haraka kwa Jiwe at a tender age of 61, ni fumbo kubwa..... Nchi ilikua inaelekea kubaya sana thus Heavens had to intervene!!

Ilikua ni kosa kubwa kwa CCM kumpitisha Magufuli kugombea urais mwaka 2015! Yapasa sasa vyama kuanza kuwapima akili wagombea urais.

Huyu jamaa alikua kiongozi ktili, mnafiki,mchonganishi, mpenda sifa, asiyeshaurika na hakika hakua na adabu! ( Kumbuka alivyo deal na akina Mzee Kinana na Makamba). Jiwe alikua hana chembe ya staha... Lugha yake ilikua ya hovyo sana akiwa hadharani_ kumbuka alitamka neno mavi!!! Jamaa alikosa kabisa busara na hekima ..Itoshe tu kusema kwamba Magufuli alikua mtu mshamba unworthy kabisa kuukwaa urais nchini Tanzania... Kwa kifupi hakua presidential material!! At all!

He was such a coward leader.. Kumbuka jinsi alivyoli handle suala korona... Ati alijaribu kuwapumbaza watu kwamba ugonjwa ule ungaliisha kwa 'maombi'... Alijaribu pia kuuhadaa ulimwengu kwamba kulikuwa hakuna korona hapa nchini.. !! Disgusting!!
Jiwe alikuwa mbabaishaji, mtu asiye na utu, asiyeshaurika, mdini na alijaa chembechembe za ukabila!!

Tumempata Samia.. Kiongozi mstaarab, msikivu, mwenye utu na subira na busara pomoni. Hivi sasa Ikulu kunapendeza.. Wafanyakazi sasa ni kicheko!! Wafanyabiashara na wakulima ni nderemo!! Kumbuka Jiwe hakuongeza mishahara hadi anakufa!!

Nchi sasa inaheshimika kote duniani.. Rais Samia ameponya majeraha mengi.. Masheik wa Uamsho wako huru, Mbowe huru, magazeti huru nk nk.. Kwa kweli kama humpendi Samia go to hell!!

....
 
hv kumbe watu wengi hivi mlimchukia Jiwe?

Yule alikua jiwe kweli kweli, sisi kama vijana tuliosoma ualimu hatutamsahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…