Habari!
Mwaka 2014 nikiwa mfanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu chini ya Barrick na baadaye kuwa chini ya acacia niliwahi kutamka jambo mbele za watu kuwa nchi hii ya Tanzania ilipaswa iwe mikononi mwa Magufuli kama RAIS ndipo ifike pazuri. Mmoja wapo akanipinga akasema Mimi natokea Chato tena nimesoma shule ya sekondari Tunduru inayomilikiwa na Magufuli. Huyo mtu namjua hafai kuwa Rais.
Mwaka 2015- 2022 nimekutana na ndugu wa damu wa Magufuli, watu aliofanya nao kazi akiwa Waziri wa wizara mbalimbali, watu aliosoma nao primary, sekondari na chuo.
Magufuli alikuwa na roho mbaya sana sana.
Nimeongea na madereva 2 waliomwendesha kabla hajawa Rais, nimekutana na kuongea naye msaidizi wake mmoja alipokuwa wizara ya Ujenzi . Nimeongea na mtu aliyelinda nyumba yake zaidi ya miaka 20.
Nimeongea na aliyekuwa mkuu wa idara fulani wizara ya Ujenzi.
Kwa ufupi yule mzee alikuwa katili na mwenye roho mbaya.
Unaweza kuniuliza hao watu nimewatoa wapi na kwanini niwahoji mambo ya Magufuli?
Ni kwamba tunakutana kwenye kazi na ndipo huanzisha stori za Magufuli hapo ndipo ninawachimba kwa viswali vidogovidogo.