Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Habari!
Mwaka 2014 nikiwa mfanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu chini ya Barrick na baadaye kuwa chini ya acacia niliwahi kutamka jambo mbele za watu kuwa nchi hii ya Tanzania ilipaswa iwe mikononi mwa Magufuli kama RAIS ndipo ifike pazuri. Mmoja wapo akanipinga akasema Mimi natokea Chato tena nimesoma shule ya sekondari Tunduru inayomilikiwa na Magufuli. Huyo mtu namjua hafai kuwa Rais.
Mwaka 2015- 2022 nimekutana na ndugu wa damu wa Magufuli, watu aliofanya nao kazi akiwa Waziri wa wizara mbalimbali, watu aliosoma nao primary, sekondari na chuo.
Magufuli alikuwa na roho mbaya sana sana.
Nimeongea na madereva 2 waliomwendesha kabla hajawa Rais, nimekutana na kuongea naye msaidizi wake mmoja alipokuwa wizara ya Ujenzi . Nimeongea na mtu aliyelinda nyumba yake zaidi ya miaka 20.
Nimeongea na aliyekuwa mkuu wa idara fulani wizara ya Ujenzi.
Kwa ufupi yule mzee alikuwa katili na mwenye roho mbaya.
Unaweza kuniuliza hao watu nimewatoa wapi na kwanini niwahoji mambo ya Magufuli?
Ni kwamba tunakutana kwenye kazi na ndipo huanzisha stori za Magufuli hapo ndipo ninawachimba kwa viswali vidogovidogo.
wewe toa povu na mijisababu mingi sisi tunamjua kuwa hakuna kiongozi aliyeijenga nchi yetu kama yeye nanukuu maneno ya kingozi mmoja mstaafu sisi tumeangaika kufanya mambo lakini tumeishia njiani wewe kwa muda mfupi umeweza yote haya
 
Lisu na mbowe wanalipwa na mabeberu ili tuweke lockdown Tanzania ,lakini i say never---' JPM
 
Tuanze kujilaumu kila mtu alikuta amezaliwa mikoa tofauti.
jamani ombeni kutenganishwa
 
Nakumbuka mbaazi ilikuwa lulu, gunia laki tatu, watu wakatajirika sana, akaja kipenzi Cha masikini na wanyonge, akaona arawapoteza masikini na wanyonge wake endapo watatajirika kwa bei nzuri ya mbaazi, bei ikaporomoka mpaka gunia ikawa elfu kumi na tano.

Masikini na wanyonge wakawa wanamshangilia mabarabarani kwa kuhakikisha kwamba urafiki wao na JPM unadumu.

JPM .....Laisi wa masikini na wanyonge
 
Kuwa na aibu hata kidogo ndugu yangu hata kama unatafuta ugali wako wa kila siku si kwa mtindo huu.
 
Magufuli alikuwa muuaji aliyevaa mavazi ya padre,akijificha kwenye migongo ya wanyonge.Rais mwongo kuwahi kutokea Africa na duniani,asiyejua kuvumilia mawazo ya wengine.Tokomea kabisa mwendazako na usiwahi rudi tena,uliowaumiza inatosha..Hata hivyo Mungu ni fundi sana,la sivyo watu wangeteseka sana kuimaliza hiyo miaka 10..
 
Aliwafurumusha wanunuzi wakubwa wa tumbaku Tabora akatuacha wakulima wa tumbaku kuanzia Mpanda, Lupa tingatinga, Sikonge, Urambo, Kaliua na kwingineko tumebaki mikono mitupu, shida kweli kweli
Mwenda zake hafai,ndo shida ya kumpa madaraka mtu ambae amekulia kwenye shida,lazima tu awachukie watu wenye vipato,Magufuli hafai..Alilazimisha watu wote sijui washindie matembele wasitajirike.Dah
 
Nakumbuka mbaazi ilikuwa lulu, gunia laki tatu, watu wakatajirika sana, akaja kipenzi Cha masikini na wanyonge, akaona arawapoteza masikini na wanyonge wake endapo watatajirika kwa bei nzuri ya mbaazi, bei ikaporomoka mpaka gunia ikawa elfu kumi na tano.
Masikini na wanyonge wakawa wanamshangilia mabarabarani kwa kuhakikisha kwamba urafiki wao na JPM unadumu.

JPM .....Laisi wa masikini na wanyonge
Alivyoua uchumi wa Mtwara sina hamu. Alitimua wazungu wa gesi, akaja akazamisha biashara ya korosho
 
Back
Top Bottom