Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
View attachment 1734652
Picha: Hayati Rais Magufuli enzi uhai wake

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti (Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss, kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo.

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje, kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu, S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
Kwa sasa tutamkumbuka kama x president maana ametuacha katika mikono salama ya Rais Samia Suluhu mama ameifungua nchi Mama ametufuta machozi na anasimamia haki za wananchi na nchi kwa ujumla ameirejesha democrasia iliyokua imepotea kwa haya yote aliyofanya Rais Samia Suluhu hatuna haja ya kumkumbuka
 
Wakati wake, tsh 100.000/ ilitosha kuanzishia biashara, Leo utafanyia nini
Pengine upo sawa kuwa 100,000/= inaweza tosha kuanzisha biashara japo sina uwakika unless you tell me they kind of bussiness that can be established with only 100,000/= but on top of that huyo jamaa ndyo alitengeneza majobless wengi ambayo ili wabidi wa forgone elimu zao then wakaanzishe hizo biashara ambazo mtaji wake ni tsh 100,000/=.
 
Ukikodoa kidogo tu kwenye andiko, uliyemuuliza kuwa ndiye, ni ndiye!

Ndiye aliyeondoa tozo zote kandamizi kwa wananchi, ndiye aliyeshusha kwa kiwango cha sawa na bule kuwaingizia umeme wananchi, ndiye aliyewalinda masikini waliokuwa wamefanywa dampo la matajiri kwa kunyang'anywa haki zao! Sio mahakamani wala kwenye Taasisi zozote za kiserikali!

Ndiye aliyewapa matumaini wananchi kuona kwamba, kumbe kuuaga umasikini na kutendewa haki pia kuhudumiwa na kusikilizwa vema na viongozi inawezekana!

Ndiye aliyewapa matumaini walala hii kwamba, kumbe inawezekana kushinda kesi zao bila rushwa ila haki ikatawala
Rais Samia Suluhu ndiye aliyeikomboa nchi kutoka kwa watu wasiojulikana
ametoa ajira za kutosha kwa vijana na bado anaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri ameimarisha diplomasia sasa tunapata wawekezaji wengi kutoka nje pia amerejesha democrasia iliyokua imepotea kwaiyo Mama amefanya mengi sana ndani ya miaka miwili wenye akili tu ndio wanaelewa
 
Kwa hali ilivyo, si mkulima wala mfanya kazi, machinga wala mama ntilie mwenye ndoto ya kuondokana na umasikini, isipokuwa ni ule ubishi tu usiosaidia chochote, hasa wafanya kazi wanaubishi usiowasaidia hata wao,

Lakini kwa hali ya sasa, baadhi ya wafanya kazi wengi, wamejaa madeni na hawajui watayalipa lini na kwa kutumia nini! Wamejaa madeni ili tu waweze kukidhi maisha yao ya sasa na siyo ya badaye! Je baadaye yao ni nini? Ni umasikini tu uliokosa njia ya kuondokana nao

Ufutwaji wa tozo na kodi zisizo na umhimu na zilizokuwa kandamizi kwa maendeleo hasa kwa walala hoi, ni moja ya mpango wa serikali ya JPM kuwaondoa wananchi wengi kwenye umasikini wao!

Udhibiti wa bei bidhaa muhimu, ni mwendelezo wa kumrahisishia mwananchi aondokane na umasikini.

Utoaji wa huduma bora kwenye Taasisi za Serikali, ushindani wa kibiashara na kuruhusu kila mwananchi afanye kazi aitajayo na mahali popote bila kubughudhiwa, ilikuwa ni njia bora kumleta mwananchi mlala hoi kwenye unafuu wa maisha!

Kuwaacha huru wamachinga, wa mama ntilie wafanye biashara popote, hii ilikuwa pia ni njia na mpango mzuri wa kuwafanya watanzania wengi wajikomboe na umasikini.

Kufuta kodi kwa wakulima wadogo wadogo na kodi ya mazao yao, wafugaji, bodaboda kufutiwa faini zilizokuwa ni kero na ni wizi kwao n.k, bado hii iliwafanya wengi wawe na ndoto za kuondokana na umasikini.

Kwa sasa hata haieleweki ni nani tena mwenye uwezo wa kujikomboa na umasikini hasa wananchi wa kawaida.

Wanakamliwa hata kile kidogo cha kwao. Kwa hali hii, Kifo cha Magufuli kimefanya jamii kubwa kukata tamaa na kuondokana na ndoto ya kuondokana na umasikini wao!

Bidhaa bei ghali, wamama ntilie wametupwa kule, wamachinga hawatakiwi kuonekana mijini! Bodaboda kadhalika!
1.Sukari 16001kg enzi za Jk hadi 30001Kg ni kumletea maisha Bora mlalahoi apate nafuu
2. Cement 12000/= enzi za Jk Hadi 20000/= ni kumletea maisha Bora mlalahoi apate nafuu
3. Mbolea 46000/= Hadi 94000/= ni kumletea maisha Bora mlalahoi apate nafuu.

Brothers and sisters if you want to post a serious matters In any platform you first consider who are going to read your article or anything else like that.

Nimetumia lugha ya kizungu kutia msistizo ila Mimi ni shuhuda wa mambo mengi kwenye kwenye jamii yangu tangu Jk
 
Kmmko! Chadema ndo wanakusanya ushuru na Kodi? Chadema ndo wanachukua mikopo?
Na wwe ni mpiga kura wa chadema,hiki chama kimejaa wahuni watupu kuanzia kwa Lemma hadi nyie walamba viatu,Lugha za matusi sio mtaji ata sisi tunajua kutukana ila sio mahala pake humu.
 
Hivyo vitu vidogo sana, kama ingepigwa high way mpaka airport hapo tungesema yes, lakini siyo kadaraja uchwara kale. Sisi kama Taifa tutajenga vingine bora zaidi.

By the way kadaraja kale ka Tazara ni mradi wa Awamu ya nne ila ujenzi ulikamilika ktk awamu yake
Sawa kadaraja la kwako liko wapi?
 
View attachment 1734652
Picha: Hayati Rais Magufuli enzi uhai wake

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti (Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss, kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo.

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje, kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu, S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
Ninamkumbuka kwa kubana demokrasia,kupoteza watu,kuokota watu kwenye viloba,kunyang'anya wafayabiashara,kununua wanasiasa waupinzani wenye njaa na waoga,kuikandamiza Zanzibar ndani ya muungano,matumizi ya ovyo ya pesa za serikali bila ya kufuata utaratibu hayo ni kwa uchache.
 
yaani unatetea mtu kutompandishia mshahara miaka sita,kutalingana na kupanda maisha kwa sasa?Vipi kuhusu kutoajiliwa watu?
Ww nikicho
yaani unatetea mtu kutompandishia mshahara miaka sita,kutalingana na kupanda maisha kwa sasa?Vipi kuhusu kutoajiliwa watu?
WW mijinga, solution sio kuongeza mshahara ni kuwapunguzia watu matumizi njia bora alioiona ni kujenga bwawa LA umeme uzalishaji ishuke bei maana ghalama za umeme angeshusha kwaiyo viwanda vingepata nishati Kwa bei ndogo vingezalisha Kwa ghalama ndogo ,mshahara ungebaki pale pale ila vitu vingeshuka be.Bwea we uwe na akili
 
Kiongozi unafikia kuingia uwanjani kucheza kibao kata ili kumfurahisha mteule?

Mawaziri walifikia kuamini kuwa ili uendelee kuwa na nafasi yako basi lazima ufanye matendo ya hovyo ili mradi Jiwe afurahi.

Kama taifa tulikwama na hatukujua nini kesho yetu .

Mtazame kiongozi wa ngazi ya uwaziri anacheza mbele ya Jiwe ili alinde teuzi yake.

Sioni kama hilo ni tatizo la kiongozi, tatizo ni hao mawaziri walio tayari kufanya lolote kutetea matumbo yao, kwani nani ana hakika kama hao mawaziri wameacha hizo tabia zao?

Kinachotufanya tuone wameacha ni kwasababu huyu aliyepo hataki hayo mambo, lakini kama ikitokea siku akayataka, basi hao wakata viuno wapo tayari.
 
Sioni kama hilo ni tatizo la kiongozi, tatizo ni hao mawaziri walio tayari kufanya lolote kutetea matumbo yao, kwani nani ana hakika kama hao mawaziri wameacha hizo tabia zao?
Kama huyo kiongozi asingekuwa anapendezwa na hayo yanayo fanyika angewakataza kabisa wasaidizi wake kuyafanya.

Mtoto umleavyo ndiyo akuavyo hivyo huwezi kumtenganisha mteuzi wao na matendo ya hao
 
Kama huyo kiongozi asingekuwa anapendezwa na hayo yanayo fanyika angewakataza kabisa wasaidizi wake kuyafanya.

Mtoto umleavyo ndiyo akuavyo hivyo huwezi kumtenganisha mteuzi wao na matendo ya hao
Kwanini umkataze mtu kufurahi? Magufuli hakuwalea hao mawaziri na tabia zao, aliwakuta nazo, hakuwapeleka darasa lolote kuwafundisha hayo.
 
Mama tunakuomba uache sasa kuwalipa hawa vijana wako kumchafua magufuli…Tayari wewe ni raisi na utachaguliwa tena 2025 Magufuli ameshafariki na wala hatofufuka kugombea tena.
Brother huwezi kuufunika moshi kwa karai, uta toka tu kupitia pembeni .
Bora karai liondolewe moshi utoke wote then ndio moto usio na moshi uwake.

Hapo ndipo mema na mazuri ya Magufuli yatajulika bayana kwa kila mtu , na matumaini kila ulimi utakiri ya kua yule ndugu alikua ni kiongozi bora kwa nyakati na nyakati.
 
Kiongozi unafikia kuingia uwanjani kucheza kibao kata ili kumfurahisha mteule?

Mawaziri walifikia kuamini kuwa ili uendelee kuwa na nafasi yako basi lazima ufanye matendo ya hovyo ili mradi Jiwe afurahi.

Kama taifa tulikwama na hatukujua nini kesho yetu .

Mtazame kiongozi wa ngazi ya uwaziri anacheza mbele ya Jiwe ili alinde teuzi yake.View attachment 2549998
Ila aliibambia
 
We jamaa ni mjinga sana
Kucheza acheze kangi hlf unamlaumu jiwe
 
Back
Top Bottom