Kuwaweka wafanyakazi wa Uma miaka 7 bila nyongeza ya mshahara wala kupanda daraja. Hili haliwezi kusahaulika.
Lakini vitu havikupanda Bei.
Wafanyakazi walimwamini sana mana waliona alichokua anakifanya na kuchukua hatua Kwa wezi waliokua wanahujumu Taifa .
Mtu akuongezee Elfu 50 Kisha apandishe umeme Bei kutoka 27000 mpaka laki nane . Mahindi kwa sasa gunia ni laki na Elfu 60. Mchele gunia laki 2.5 mpaka tatu.
Tozo kila mahali. Umeme wa Elfu 30 haufiki unit 70. Laiti JPM angewanyonya wananchi na kupata misaada kama tunayoipata Leo nadhani nchi hii baada ya miaka Kumi ingekua kama Dubai.
Bidha nyingi zinazoingia hazina viwango.
Watu wanaweka mchanga kwenye ghala za umma badala ya Mbolea.
Kuna chumvi zinauzwa zimechanganywa na mchanga.
Watu wanaongezena posho za safari ambazo hazina Kodi wanaonufaika ni wakubwa mana wanajipangia safari za kufilisi nchi Kwa manufaa yao .
Wageni wamevamia ardhi Kwa ajili ya kulima wakati 80% ya watanzania ni WAKULIMA. Watalima Nini watoto wetu wanaosomea kilimo na wanaokosa ajira wakati Mashamba wanauziwa Wahindi ,wachina na Waarabu !!
Mh. Rais Fanya juhudi ubadili Katiba hii inayowanufaisha wezi na mafisadi waliokuzunguka .
Katiba ya mwaka 1977 ni katiba ya Kidikteta . Wewe Mama yetu sio dikteta huwezi kwenda na mziki wa katiba 1977 . Wewe ni mpenda Demokrasia na utawala Bora unaohitaji watu waadilifu wasiopenda kusukumwa Bali kusukumwa na SHERIA.
Sasa ukikumbatia katiba ya Kidikteta wakati umezungukwa na wezi waliozoea kukoromewa na kutumbuliwa na kufokewa adharani Kwa kuitwa wajinga na wapumbavu ndipo wafanye kazi wengine Kwa paniki na presha mpaka wanaingiwa na hofu kama vile wako mbele ya kiti Cha hukumu Cha Mungu ,hakika nchi hii itaibiwa sana huku wengi waliishi maisha magumu Kwa BIDHAA kupanda Bei na gharama zote za maisha kuwa juu huku wateule wako wakitafuta namna ya kupata 10% Kwa kuagiza magari ya kifahari kila mwaka na kucheza na miradi ya umeme na kujenga madaraja ya matope mvua zikinyesha yanasombwa.
Watu waliostahili kuswekwa ndani Kwa uhalifu wao na kutokua na huruma Kwa watanzania Leo wao ndio wanatanua mitaani kisa Hakuna dikteta wa kuswasulubu.
Basi tupe katiba itakayotupa Sisi wananchi nguvu ya kuwashughulikia wezi wa Mali za umma na wazembe na Wala rushwa. Tutawashughulikia wenyewe kupitia katiba ya warioba.
Mtu anapewa ofisi ya umma mwaka mmoja anakua bilionea na kuanza kukimbizana na Manji. Umma utamhajo na kumkataa kwenye ofisi za umma Kisha kumweka mtu mwadilifu wa kushumghulikiwa mwizi.
Itoshe TU kusema kila zama na kitabu chake . JPM atakumbukwa Kwa mema yake vizazi Kwa vizazi. Wachache walioguswa katika safisha safisha ya uchafu wa kitaifa basi hao pia watakumbukwa Kwa mabaya na mema waliyofanyia familia zao huku Taifa likikwama Kwa sababu ya hujuma zao.
Wanasiasa nao watamkumbuka JPM Kwa kuweza kutuonyesha nani wapinzani wa kweli na nani ni ndumilakuwili na wasaliti.