Mama tunakuomba uache sasa kuwalipa hawa vijana wako kumchafua magufuli…Tayari wewe ni raisi na utachaguliwa tena 2025 Magufuli ameshafariki na wala hatofufuka kugombea tena.
Asante mkuu kwa huu ujumbe inawezekana pia hata hawajatumwa bali ni chawa tu kujipendekeza.
 
1. Kwa nini sisi Waafrika hupenda kujutia yalopita? 2. Kwa nini Waafrika hupenda kuzungumzia kumbukizi zaidi ya Hali iliyopo?
3. Na kwa nini hatuwapendi watu wanaojituma kazini isipokuwa wale wanao tuhongera.
4. Kwa nini sisi Waafrika tunapenda kuzungumzia WATU badala ya FIKRA?
 
Inawezekana mwenzangu umenizidi kwa ujinga, unadhani kwa miaka sita bei ya bidhaa zilikuwa zimesimama zinamsubiria yeye? Na kikubwa kinachoshusha bei ya bidhaa ni mafuta siyo umeme
Viwanda vingapi vidogo na vikibwa vinavyotumia mafuta,
 
Ripoti za makinikia.

Bwawa la Nyerere

Sgr

Uchumi wa kati chini

Hali ngumu ya kisiasa na kidemokrasia 2015-2020

Namna alivyoshughulikia Corona kwa kipekee na kujilipua.

Sakata la watumishi wa umma wenye vyeti feki.

Hali ya sekta binafsi na ajira kwa ujumla kabla na baada ya janga la Corona.

Na mengine mengi tu....
 
Vyeti feki ni wapinzani tu ndiyo vyeti feki?
 
Namwomba mtoa mada aijumlishe hii👆🏻 nazan aliisahau, mkuu hapa umesahau WASIOJULIKANA
 
Kuwaweka wafanyakazi wa Uma miaka 7 bila nyongeza ya mshahara wala kupanda daraja. Hili haliwezi kusahaulika.
Lakini vitu havikupanda Bei.
Wafanyakazi walimwamini sana mana waliona alichokua anakifanya na kuchukua hatua Kwa wezi waliokua wanahujumu Taifa .
Mtu akuongezee Elfu 50 Kisha apandishe umeme Bei kutoka 27000 mpaka laki nane . Mahindi kwa sasa gunia ni laki na Elfu 60. Mchele gunia laki 2.5 mpaka tatu.
Tozo kila mahali. Umeme wa Elfu 30 haufiki unit 70. Laiti JPM angewanyonya wananchi na kupata misaada kama tunayoipata Leo nadhani nchi hii baada ya miaka Kumi ingekua kama Dubai.


Bidha nyingi zinazoingia hazina viwango.
Watu wanaweka mchanga kwenye ghala za umma badala ya Mbolea.

Kuna chumvi zinauzwa zimechanganywa na mchanga.
Watu wanaongezena posho za safari ambazo hazina Kodi wanaonufaika ni wakubwa mana wanajipangia safari za kufilisi nchi Kwa manufaa yao .
Wageni wamevamia ardhi Kwa ajili ya kulima wakati 80% ya watanzania ni WAKULIMA. Watalima Nini watoto wetu wanaosomea kilimo na wanaokosa ajira wakati Mashamba wanauziwa Wahindi ,wachina na Waarabu !!

Mh. Rais Fanya juhudi ubadili Katiba hii inayowanufaisha wezi na mafisadi waliokuzunguka .

Katiba ya mwaka 1977 ni katiba ya Kidikteta . Wewe Mama yetu sio dikteta huwezi kwenda na mziki wa katiba 1977 . Wewe ni mpenda Demokrasia na utawala Bora unaohitaji watu waadilifu wasiopenda kusukumwa Bali kusukumwa na SHERIA.
Sasa ukikumbatia katiba ya Kidikteta wakati umezungukwa na wezi waliozoea kukoromewa na kutumbuliwa na kufokewa adharani Kwa kuitwa wajinga na wapumbavu ndipo wafanye kazi wengine Kwa paniki na presha mpaka wanaingiwa na hofu kama vile wako mbele ya kiti Cha hukumu Cha Mungu ,hakika nchi hii itaibiwa sana huku wengi waliishi maisha magumu Kwa BIDHAA kupanda Bei na gharama zote za maisha kuwa juu huku wateule wako wakitafuta namna ya kupata 10% Kwa kuagiza magari ya kifahari kila mwaka na kucheza na miradi ya umeme na kujenga madaraja ya matope mvua zikinyesha yanasombwa.

Watu waliostahili kuswekwa ndani Kwa uhalifu wao na kutokua na huruma Kwa watanzania Leo wao ndio wanatanua mitaani kisa Hakuna dikteta wa kuswasulubu.

Basi tupe katiba itakayotupa Sisi wananchi nguvu ya kuwashughulikia wezi wa Mali za umma na wazembe na Wala rushwa. Tutawashughulikia wenyewe kupitia katiba ya warioba.

Mtu anapewa ofisi ya umma mwaka mmoja anakua bilionea na kuanza kukimbizana na Manji. Umma utamhajo na kumkataa kwenye ofisi za umma Kisha kumweka mtu mwadilifu wa kushumghulikiwa mwizi.

Itoshe TU kusema kila zama na kitabu chake . JPM atakumbukwa Kwa mema yake vizazi Kwa vizazi. Wachache walioguswa katika safisha safisha ya uchafu wa kitaifa basi hao pia watakumbukwa Kwa mabaya na mema waliyofanyia familia zao huku Taifa likikwama Kwa sababu ya hujuma zao.

Wanasiasa nao watamkumbuka JPM Kwa kuweza kutuonyesha nani wapinzani wa kweli na nani ni ndumilakuwili na wasaliti.
 
Na walikwapua 1.5trillion usisahau
 
Ukimwona mtu mzima Analía lía kuna Jambo linamsibu. Hizi kelele za kumlilia Magufuli mnaozipuuza endeleeni kupuuza ila Mda ni Mwalimu mzuri.

Narudia Mambo ni Mengi mda ni mchache tunaomkumbuka Hayati na kulialia Mambo ya hovyo tunayoyashuhudia Kwa sasa TZ ni mengi mno.
 

Ebu mpumzisheni aisee kila mara mnaleta thread zake,mnapoleta issue zake na ndiyo anazidi kupopolewa.

Kama unamkumbuka sana nenda chato ukakae pembeni ya grave.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…