JPM ulifahamu yaliyokuwa yanaendelea nchini katika utumishi wako wa miaka ishirini na tano kwenye medani ya siasa. Wakati wa uongozi wako ulijali Sana wananchi wa daraja la chini ambapo tulinunua mchele tsh. 1200/= kwa kilo; kwa utawala wa Sasa unaojipambanua kwa kuingiza magari 60 ya Mwigulu Lameck Nchemba kwa siku moja; kilo moja ya mchele kwa Sasa tunainunua kwa tsh. 3500/=. Hakika tutakumbuka baba ila uliokuwa umeziba mirija yao ya matumizi mabaya ya fedha ya umma daima wataendelea kukulaani bila kufahamu kuwa ulishalala milele na hakuna siku amabayo utaweza kuwajibu.
Wamebaki wanasiasa uchwara akina Hussein Bashe wasiofahamu hata jembe linashikwaje lakini eti leo Bashe ndye waziri wa kilimo. Wananchi tunaumia Sana Tena Sana lakini BEPARI Bashe anajinasibu kuwa mazao sio Mali ya serikali kwa hiyo wakulima waachwe wauze wanavyotaka. Mkulima wa kawaida hanufaiki na kauli ya kijinga, KEJELI, DHIHAKA na KIZANDIKI ya bepari Hussein Bashe bali anawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwani wanufaika wakuu wa mfumuko Mkubwa na wa kutisha wa Bei ya chakula Ni bepari Bashe na washirika wake.
Wakati wa uongozi wako hakukuwa na nyongeza ya mshahara lakini maisha yaliendelea bila shida kutokana umakini wako wa kudhibiti mfumuko wa Bei ya chakula. Leo mtu anaona vema kuhudumia watoto wa jirani wake wakati nyumbani kwake watoto wa wanalala njaa!. Daima tutakumbuka JPM.