Aisee mbona bashe ni mkulima wa mpunga huko kwao nzega tokea akiwa mwanafunzi? Hilo la bashe kutokujua kushika jembe umelipata wapi?
 
..
 

Attachments

  • JamiiForums839866055.jpeg
    46.5 KB · Views: 7
  • 1679652251550.jpg
    74 KB · Views: 6
  • IMG-20200403-WA0003.jpg
    12.9 KB · Views: 7
Kwa kuwa tunaamini kimwili haupo na sisi ila kiroho upo na sisi, naomba nikupe taarifa hii.

1. Nyumba yetu uliyoiacha ikiwa haivuji kwa zaidi ya 91%, sasa inavuja karibu kila kona kwa zaidi ya 78%.

2. Panya na mchwa uliowafunika na jiwe zito ili wasiendelee kuleta usumbufu katika nyumba yetu, mlinzi wa nyumba amewafungulia na amewapa kazi ya kulinda ghala la chakula chetu.

3. Cha ajabu kabisa na cha kushangaza ni kwamba, mlinzi aliyewakaribisha panya na mchwa chumbani, ndiyo huyo huyo anayetoka hadharani kulalamika eti panya na mchwa wametafuna nguo na kuharibu chakula kilichohifadhiwa.

Mlinzi huyu kazi yake kubwa ni kulalamika tu bila hata kuwachukulia hatua kali hawa panya na mchwa ikiwa ni pamoja na kuwafukuza hapa nyumbani.

Kwa ujumla Baba, hali ya nyumba yetu si shwari kabisa.

RIP Shujaa wetu, JPM.
 
Hii ni ishara ya kuwa unawaamini watu wengine kuliko unavyo jiamini wewe mwenyewe.

Huyu unae msema hawezi kukusia all Isha kufa, kuna sehemu Kuna shida upambane tulio Hai kurekebisha Marehemu Hana msaada kwa tulio Hai hata tumsifu vipi
 
Nini kilimtoa Prof. Assad offisini kama so kuhoji ufisadi wa lile chizi lenu
 
Baba wakati wako ulikuwa unakula peke yako na Wananzengo ulio wachagua mwenyewe ila Sasa kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.

Miradi uliyoiacha inaendelezwa kwa kiwango Cha kuridhisha na itakamilika ila waimba mapambio wako wanamkwamisha mama.

Anajitahidi ila kundi lako halifurahii mafanikio yake.

Demokrasia imetamalaki ila enzi zako hali ilikuwa mbaya.

Uendelee kuongoza Malaika wa kuzimu salama.
 
RIP JPM ama kweli tutakukumbuka 1. 1..TOTO Afya Kodi hamna tena huku baba.

2. Mchele tulionunua 1600 sasa ni 3500 baba.

3. Baba Petrol uliacha 1900 sasa ni 3000.

4. Bwawa la Nyerere halijanza mpaka leo.

5. Baba wajua kwamba tulichanjwa na chanjo ya COVID 19 na mikopo juu?.

6. Nakunong'oneza baba "Eti Mwigulu Nchemba Ndiyo waziri wa fedha, Makamba nishati na Nauye mawasoliano.".

7. Mwanza tulienda Kwa elfu 45 Sasa billa 65000 hufiki.

Ni hayo tu Kwa leo Mzee wetu
 
Ngoja vyeti feki waje uone utakavyooga matusi.

Kuna muda ni heri tu mngemwacha huyu mzee akapumzika kwa amani,kuliko kumtaja taja,mnaganya anazidi kutukanwa kila kukicha.
 
Unamuomba mfu kweli kabisaa?

Au ndiyo kutafuta kiki?
Amefikisha ujumbe kwa njia ya sanaa.

Humo ndani pia kataja,mchwa,panya,nyumba nk. Hivyo vyote si vitu halisi katika katika context ya alichokikusudia kufikishia hadhira. Ni sanaa na usanii ili ujumbe uwafikie wahusika.
 
Amefikisha ujumbe kwa njia ya sanaa.

Humo ndani pia kataja,mchwa,panya,nyumba nk. Hivyo vyote si vitu halisi katika katika context ya alichokikusudia kufikishia hadhira. Ni sanaa na usanii ili ujumbe uwafikie wahusika.
Yeye mwenyewe chawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…