Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...
Hakuna lolote unalolijua.....afadhali ungekufa wewe abaki yeye tu. R.W.Y.D.(Rest Where You Deserve) JPM
 
Ni kweli hakuwa mtimilifu, pia aliibua chokochoko nyingi tu na kusababisha malumbano yasiyokuwa na tija ila binafsi kuna vitu nilipenda sana kwake na kujifunza pia. Mojawapo zaidi ya vyote ni namna alivyokua mjasiri na mwenye kujiamini kwenye kila uamuzi aliouchukua.

Kwenye kazi zangu nimebahatika mara kadhaa kuwa kiongozi/meneja kwenye baadhi ya miradi na udhaifu mkubwa niliokuwa nao ni hilo la kutokua mjasiri wa kufanya maamuzi magumu palipostahiki, mara nyingi nilijikuta nakosa hamu ya kula, nakosa usingizi kabisa, mwili wote ulikuwa unanitetema na kuloa jasho kila nikiwaza hatua za kuchukua na hii ilinigharimu sana hadi kuboronga kwenye ufanisi.

Sijui hawa viongozi (marais wa mataifa, akiwemo Trump) huweza vipi huo ukali na ujasiri wa kuyafanya yote ambayo wao huyafanya. Kuna watu walizaliwa wawe viongozi maana kuna baadhi yetu ni mwendo wa presha tu.

RIP mkulu JPM, kuna vitu sikukubaliana na wewe ila kuna mambo nilijifunza kutoka kwako, nilipenda sana baadhi ya video zako.
 
Kwakweli sio uwongo maji ya bomba mtaani kwetu yalikuwa yanatoka usiku tu
Yaan unapeleka ndoo usiku unazifata asubuhi
Lakini sasa hivi kwanza kila nyumba ina bomba asiyevuta bomba ni ubahiri wake tu mwenyewe wa kijinga
Na maji yasipotoka mtaani siku 1 tu unapiga simu DAWASCO mbna maji hayatoki leo vipi ?
Na unajibiwa kuna matengenezo ya barabara yatatoka jioni au kesho nk yaan unapewa sababu yenye mashiko
Tangu magufuri aingie madalakani sijawahi sikia kuna Bomba limepasuka huko BOKO sijui Bunju kama miaka ya nyuma wiki nzima mpk tunashuka mkwajuni BONDENI kama sio frolida kufata maji au jangwani km hakieleweki tunaua winga boda la SUNA muhimbiri hiyo kufata bomba kubwa la maji ni noma miaka hiyo

Umeme sasa TANESCO zamani ile shoti nyumba hii inawaka halafu zingine haziwaki
ikitokeaga hivyo enzi hizo tunajisemea jamani hii mpk kesho leo tunalala giza tu
Lkn katika utawala wa magufuri yaani hata sasa hivi muda huu saa 9 usiku umeme transfoma lizogoe ukiwapigia TANESCO ndani ya lisaa au nusu saa washatia timu

Nazungumzia experience yangu kwa mkoa wa DAR kwa miaka zaidi ya 30 tangu Nipate Kuishi hapa MKOANI DAR ES SALAAM
sasa sijui huko NYANDA ZA JUU KUSINI hali ilikuaje BEFORE and NOW
 
Usingizi umekataa kuja kabisa, roho yangu inauma Kama kidonda kilichochomwa na mwiba.

Najisikia huzuni isiyo na mfano kiongozi niliye mpenda kwa moyo wangu wote ametutoka daaah 😭😭😭😭😭😭😭

Nenda Baba nenda JPM, Tanzania tutailinda na kuitetea daima

Mungu wewe ni mkuu siku zote

Ujasiri, ushupavu, uchapakazi, uchamungu, uzalendo uliotukuka hakika wewe ni zawadi ya Mungu kwa Watanzania

Nakupenda JPM
 
The man was cooocoo for cocoa puffs.....

I'm sure he was a great husband and father and I hope the almighty grants his family heavenly peace.

However, I know for a fact he was a shitty president. All in all I pray and hope tanzania gets the president they need. Good luck my neighbors

Just my opinion
 
Ni kweli hakuwa mtimilifu, pia aliibua chokochoko nyingi tu na kusababisha malumbano yasiyokuwa na tija ila binafsi kuna vitu nilipenda sana kwake na kujifunza pia. Mojawapo zaidi ya vyote ni namna alivyokua mjasiri na mwenye kujiamini kwenye kila uamuzi aliouchukua.

Kwenye kazi zangu nimebahatika mara kadhaa kuwa kiongozi/meneja kwenye baadhi ya miradi na udhaifu mkubwa niliokuwa nao ni hilo la kutokua mjasiri wa kufanya maamuzi magumu palipostahiki, mara nyingi nilijikuta nakosa hamu ya kula, nakosa usingizi kabisa, mwili wote ulikuwa unanitetema na kuloa jasho kila nikiwaza hatua za kuchukua na hii ilinigharimu sana hadi kuboronga kwenye ufanisi.

Sijui hawa viongozi (marais wa mataifa, akiwemo Trump) huweza vipi huo ukali na ujasiri wa kuyafanya yote ambayo wao huyafanya. Kuna watu walizaliwa wawe viongozi maana kuna baadhi yetu ni mwendo wa presha tu.

RIP mkulu JPM, kuna vitu sikukubaliana na wewe ila kuna mambo nilijifunza kutoka kwako, nilipenda sana baadhi ya video zako.
 
The man was cooocoo for cocoa puffs.....

I'm sure he was a great husband and father and I hope the almighty grants his family heavenly peace. However, I know for a fact he was a shitty president. All in all I pray and hope tanzania gets the president they need. Good luck my neighbors

Just my opinion
He was neither a good husband, father nor a good president. Nobody has ever been happy around him than himself
 
Poleni sana ndugu zetu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
 
Usingizi umekataa kuja kabisa, roho yangu inauma Kama kidonda kilichochomwa na mwiba.

Najisikia huzuni isiyo na mfano kiongozi niliye mpenda kwa moyo wangu wote ametutoka daaah [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Nenda Baba nenda JPM, Tanzania tutailinda na kuitetea daima

Mungu wewe ni mkuu siku zote

Ujasiri, ushupavu, uchapakazi, uchamungu, uzalendo uliotukuka hakika wewe ni zawadi ya Mungu kwa Watanzania

Nakupenda JPM
Hya maumvu Wenzako tulpata
sku ccm walshindaa viti vyoooote vya Ubunge

[emoji30][emoji30][emoji30]
 
Back
Top Bottom