Hiii ni legacy nyingine ya Magufuli.
Kabla ya magufuli kushika madaraka vikongwe hasa wa kanda ya ziwa waliripotiwa kuuawa kwa imani za kishirkina.
Kwa kipindi cha miaka mitano sijasikia wimbi la mauaji ya vikongwe hata katika media za nje kama BBC.

Ulitaka usikie kwenye vyombo vya habari ambavyo alivitishia kutangaza hizi habari? Kutokusikia sio lazima iwe hakuna hayo mauaji.
 
Kweli asee... Kundi hili liliishi kwa furaha sana na amani enzi za utawala wa jamaa.
 
VIKONGWE WALIKUWA WANAUAWA NA WASUKUMA WENZIE HIVYO SIRI YAO ALIKUWA ANAIJUA! LAKINI BEN SAANANE,MAWAZO NA GWANDA ALIWAUA!!
Je aliyemiminwa shaba 16 +!!
Mungu alimnusuru ili makusudi aone mbaya wake akiondokea zake!!
 
Marehemu dikiteta magufuli alikuwa anaua vijana tu, kama akina Ben, azory na wakosoaji wengi tu.
 
Aliombewa na ataendelea kuombewa ametunukiwa kuwa Rais wa malaika. Alivyowazia kipindi. Aliye na ile clip atupatie!
 
Aliyeturoga kafa kwakweli!!! Utasikiaje ilhali sheria kandamizi kwa vyombo vya habari ilikuwa kazini?
Miungu ya Baali ilitaka taarifa za kusifia na kuabudisha tyu. Hata ajali za barabarani zilikuwa hazitangazwi kutokana na uoga!!!
LAITI MNGEJUA KAZI ALIYOKUWA AMEPANGIWA WAZIRI WA WIZARA MPYA YA MAWASILIANO. HII JAMII FORUM ILIKUWA IFE!!!
Tumshukuru Mungu kwa kukutana na miungu hii KARMELI na kuonyesha ukuu wake. Mungu sniper. Anajua kuotea vichwa wallah!!!
 
Kuna watu hawana kazi yani wewe wazazi wako hiyo ada bora wangenunuwa Punda ziwasaidie kuchota Maji kuliko kukupeleka Darasani kufuta ujinga ndio umezidi kuwa mjinga
 
Chuki yako haibadilishi ukweli wa Mambo kuwa Magufuli ni shujaa Hadi wajukuu wako watamkumbuka kwa mema aliyoyafanya.Mimi nasisitiza tufanye jambo makhususi kumuenzi huyu shujaa wetu.
Shujaa aliyeshindwa asante mungu kwa kazi yako
 
No kawaida Watanzania kusikitika juu ya ugumu wa maisha. Hata wale wasiofanya kazi wanaoishi kwa kupiga vizinga huu wimbo wa Maisha magumu wanaupenda na kuuimba pia.

Sasa katika vipindi vyote 6 vya utawala, utawala wa Magufuli ndio umevunja record ya watu kusikitika juu ya ugumu wa maisha.

Samia Suluhu kaingia madarakani hakuna Economic Reformation yoyote ile kaifanya, tunaishi kwa shilingi aliyoikusanya Magufuli au tuseme kuwatunaishi kwa bajeti ya Magufuli lakini kelele za maisha magumu zimekata au kupungua.

Hii maana yake ni kwamba Magufuli alikuwa na nuksi.
 
Huku kwetu Mbeya, Magufuli kaja na kuonfoka kama alivyopita Mwinyi, Mkapa, Kikwete.

Wote hao walitoa ahadi ambazo hadi leo hakuna zilizotekelezwa.
Kero ha barabara iingiayo Mbeya mjini na kutoka kwenda Mbalizi iko vile vile kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Na sasa inaenda kuwa mbaya zaidi maana zkilande cha Iwambi-Mbalizi sasa linapita gari moja moja.

Barabara za wilayani zilizo ahidiwa ndiyo usisema.
Kule kwetu kijijini barabara ya Tukuyu-Masoko-Lwangwa-Katumba, kila Rais aliyepita kaahidi lakini hakuna kitu.
Airport ya Songwe ilianza kujengwa 2001, hadi leo haijakamilika.
Abiria wakiwa wengi, hakuna mahali pa kukaa na hatimaye kulowa mvua.

Huko Ileje, nasikia kuna mradi lakini mwendo wake ni balaa!
Wakati huohuo, Chato Airport imejengwa miaka 3, Busisi Bridge inaenda kasi,Chato inakua kama uyoga!

Sijui kwa kwetu nimkumbuke Magufuli kwa lipi?
 
Ukiona mwananchi wa Mbeya anamsifia Magufuli basi ujuwe kisomo chake ni duni au hajitambui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…