Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.


Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
I cant say more! Ni Nabii wetu na ni Mfalme wetu. Atakayefuata kama yeye ni miaka 50 ijayo!
 
Huu uzi ni kwa ajili ya watu tulioguswa na kifo cha mpendwa wetu Rais John Pombe Magufuli.

Kama wewe ni miongoni mwa wafiwa, pita hapa sema chochote, tueleze kwa nini umeguswa na msiba huu? unamkumbuka vipi hayati JPM?

Binafsi namkumbuka jpm kwa mengi ila kubwa zaidi, jpm alikuwa mwanaume wa shoka asiemuogopa yeyote.lakini pia hii nchi alikuwa ameiweka kwenye stari. Matunda wangefaidi vizazi na vizazi.

Watanzania wanapenda dezo, lelele mama hawataki kufanya kazi, hawataki kulipa kodi ndo maana wana chuki sana.

Sisi tulioumizwa na kifo chake tunaumia kwa sababu aliweza kufanya kwa vitendo. vitu alivyovifanya vinaonekana. Hata umchafue vip watanzania wanaona.

Humu kuna watu wenye akili timamu ambao wanaweza kusema hapa kuwa kipindi cha jpm wamefanya vitu vya maendeleo, ukifata utaratibu mambo yanaenda, rushwa ilikuwa imepungua sana.
Watu walipata kazi/ vyeo bila upendeleo.
Kama binadamu, kuna mengine alikuwa hajafanya lakini alikuwa anaelekea huko.

NB.wewe kama unajua wewe ni miongoni mwa walioshangilia na kusheherekea kifo cha jpm pita kimia kimia, nyuzi zipo nyingi za kuchangia.

Libarikiwe tumbo lililozaa hiki chuma.ni mwezi sasa bila chuma. RIP JPM

Wafiwa tujuane.
 
Kimia kimia.....ni Kimya kimya ......( naweza nahatisha kabila lako)

Btw Kifo cha mpendwa wetu JPM kimegusa watanzania wanyonge.
 
Kwanamna moja au nyingine na mimi ni mfiwa ingawa nimeguswa kwa mabaya aliyowahi kufanya marehemu alikuwa na ubabe wa kijinga akidhani ndio uongozi bora . Kiburi ,jeuri na dharau zilikuwa miongoni mwa sifa za marehemu na alijiona ana akili kuliko watanzania wote anaowaongoza.

Kiburi ni sifa ya Mwenyezi Mungu siyo binadamu. Marehemu ametuachia funzo kubwa sana.
 
Soon watakuja waliotahiriwa na JPM kuponda utawaona tu....
ukiona kelele ujue mtahiriwa huyo
 
Kuna vyeo vingi sana watu walipewa kwa upendeleo. Yaani kama ulihombania ubunge CCM 2015 ukakosa CV yako ikamkuta mheshimiwa basi lazima ulipata cheo tu. Na hata kwenye nafasi nyeti serikalini aliwajaza sana hao wakosa ubunge. Ilikuwa ni aibu chama kilishika hatamu kwa mara ya pili.

Unapozungumza magufuli na upendeleo huu sasa ndio upendeleo kwakuwa hii nchi sio ya CCM.
 
Magufuli aliifanya kwa vitendo dhana ya kujitegemea, alipunguza sana rushwa na ubadhilifu, aliwashinda mabeberu na kutetea rasilimali zetu. Ametusaidia kufikia uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda tarajiwa. Hakika alikuwa zawadi ya Mungu kwa Watanzania. Apumzike kwa amani.
 
Mimi sio mfiwa,ila nimeguswa na jinsi ulivyoguswa na aliyekugusa pole mamiloo.
 
Hakika aliwaza kuwanyoosha vibaraka wa mabeberu, wapigaji na wavivu. Hawana hamu naye. His love for his country couldn't be greater. May his patriotic soul rest in eternal peace. 🙏🙏
 
Back
Top Bottom