1. Uzalendo - kuipenda nchi yake na kuhakikisha resources za nchi ni kwa manufaa ya wananchi na sio viongozi na wawekezaji wezi.
2. No-Nonsense - kutopuuzia uzembe kazini wala ubadhirifu. Alitumbua immediately! Alikataa mikataba ya wizi na kurekebisha sheria ziwabane wawekezaji wezi. Nasikia sasa wataingia kirahisi tu![bila shaka wataiba kiraisi pia]
3. Rais wa watu - aliwapenda na kuwatetea kwa nguvu zote watu wa chini sana. hii itachukua miaka mingi sana kutokea. Umati wa watu katika msiba wake na vilio vyao viliwaziba midomo waliosema alikuwa ni Rais aliyechukiwa na wengi!
4. Uchapakazi wake - hakuwa Rais wa kupokea report tu bali kuzifanyia kazi na kutosinzia ili ajue mambo.
5. Uchumi - Hii nchi kaipeleka haraka sana - walimpinga sana lakini statistics zote za maendeleo ua uchumi zilikuwa upande wake. Iwe infrustructure, services kama umeme, elimu na afya, na rank yetu kimataifa. NASIKIA sasa tunaanza kushuka!
6. Ucha Mungu - Pamoja na madhaifu yake [nani ni mkamilifu?] sio tu alisali, bali aliwaheshimu viongozi wa dini wote na kuwaomba wamwombee. Tunasikia kwenye death bed yake aliombewa na viongozi wote hata waislamu wakati yeye alikuwa mkristu!
Kazi ya Mungu haina Makosa. RIP JPM!