Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
In short time, amefanya mengi mazuri ambayo kama ingekuwa imefanyika ivyo before him nadhani tungekuwa mbali sana kimaendeleo. suala la kufanya kila raia achangie kodi kuendeleza miradi ilikuwa safi.
all in all amefanya mengi sana mazuri.

rest in peace our hero - JPM
 
This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.


Itaendelea...
Kwa majambazi kajitahidi
 
Mi nilishangaa tu kwa mtu aliyedaiwa kuwa ni mcha Mungu hakuwakemea waliomfananisha au kumpa hadhi ya " umungu" sijui hakusikia au vipi ?
Maisha tunayoyaishi ni mafupi sana but binadamu huwa tunasahaulishwa na mambo makuu matatu either madaraka, pesa na afya so jiwe alilewa one among mentioned na akasahau siku za kuishi ni chache sana (rejea maandiko ya dini) so in my side naamini sana katika hofu ya mungu seriously ukiwa nayo huwez kukosa hekima especially kwa kiongoz kama rais!!!!!!!!!
 
Alisema ataongeza na kupandisha mishara akikaribia kutoka madarakani. Alisahau mwanadamu anapanga na Mungu anaamua.
Kuongeza mshahara wakati unakaribia kutoka ilikuwa ni uhuni na kumfanya Rais ajaye aonekane hafai.Angeongeza mishahara ingekuwa mikubwa zaidi kiasi kwamba ingekuwa ngumu kwa mwenzie kufanya miradi mikubwa ya Maendeleo.Alitakiwa aongeze mshahara akiwa madarani sio kusubiri unakaribia kutoka ili kuwapa mzigo wengine
 
Kutinga site kukagua maendeleo ya miradi na kuhoji matumizi ya fedha kama huna majibu na umefanya mambo ya ovyo anakutumbua mbele ya kadamnasi
 
Viongozi kuwacharaza wananchi viboko hadharani na yeye kukaa kimya (pengine aliwatuma au alikuwa anafurahia).
 
“A true leader has the confidence to stand alone, the courage to make tough decisions, and the compassion to listen to the needs of others. He does not set out to be a leader, but becomes one by the equality of his actions and the integrity of his intent.”
1.Msimamo
2.Kututia ujasiri
3.miundo mbinu
4.Kutuondolea ufisadi
 
“A true leader has the confidence to stand alone, the courage to make tough decisions, and the compassion to listen to the needs of others. He does not set out to be a leader, but becomes one by the equality of his actions and the integrity of his intent.”
1.Msimamo
2.Kututia ujasiri
3.miundo mbinu
4.Kutuondolea ufisadi
5. No double standards.
 
Hakuna lolote unalolijua.....afadhali ungekufa wewe abaki yeye tu. R.W.Y.D.(Rest Where You Deserve) JPM
Hahaha, ndugu tatizo waTanzania tunadhani kifo ni "Sanitizer" kwamba kinamsafisha mtu, marehemu asemwe kwa mabaya yake na mazuri yake, sio kutaja mazuri tu na kuacha mabaya,

Magu alikuwa na mabaya mengi kuliko mazuri, tena hayo mazuri hayakuwa special kwake tu, wanaosema alileta nidhamu serikalini watakuwa mabeki tatu wasiofika kwenye ofisi za serikali, nidhamu haikuwepo kabisa, wanaosema rushwa ilipungua ni mabeki tatu wasiofika kwenye ofisi za serikali, jamaa alikuwa na propaganda za hovyo, eti dunia inatuonea wivu, tangu lini maskini anaonewa wivu!, alikuwa na misimamo ya hovyo isiyo na faida!
 

Kwakweli sio uwongo maji ya bomba mtaani kwetu yalikuwa yanatoka usiku tu
Yaan unapeleka ndoo usiku unazifata asubuhi
Lakini sasa hivi kwanza kila nyumba ina bomba asiyevuta bomba ni ubahiri wake tu mwenyewe wa kijinga
Na maji yasipotoka mtaani siku 1 tu unapiga simu DAWASCO mbna maji hayatoki leo vipi ?
Na unajibiwa kuna matengenezo ya barabara yatatoka jioni au kesho nk yaan unapewa sababu yenye mashiko
Tangu magufuri aingie madalakani sijawahi sikia kuna Bomba limepasuka huko BOKO sijui Bunju kama miaka ya nyuma wiki nzima mpk tunashuka mkwajuni BONDENI kama sio frolida kufata maji au jangwani km hakieleweki tunaua winga boda la SUNA muhimbiri hiyo kufata bomba kubwa la maji ni noma miaka hiyo


Umeme sasa TANESCO zamani ile shoti nyumba hii inawaka halafu zingine haziwaki
ikitokeaga hivyo enzi hizo tunajisemea jamani hii mpk kesho leo tunalala giza tu
Lkn katika utawala wa magufuri yaani hata sasa hivi muda huu saa 9 usiku umeme transfoma lizogoe ukiwapigia TANESCO ndani ya lisaa au nusu saa washatia timu

Nazungumzia experience yangu kwa mkoa wa DAR kwa miaka zaidi ya 30 tangu Nipate Kuishi hapa MKOANI DAR ES SALAAM
sasa sijui huko NYANDA ZA JUU KUSINI hali ilikuaje BEFORE and NOW
Nimeishi Dar, Morogoro na Iringa, Dar kulikuwa na shida ya maji, ila Moro na Iringa ahida ya maji iliisha tangu Kikwete era, so nothing special hapo ni muendelezo, asionekane kama mkombozi wakati alikuwa na roho mabaya sana, katili mno!
 
Kati ya watu ambao walimlaani huyu mzee, na mimi ni mmoja wao! Maana hakututendea kabisa haki watumishi wa umma katika utawala wake.

Ila sijawahi kumuombea kifo. Katika hili, namtakia pumziko la milele.
Kifo ukisikie tu kwa jirani. Ila huleta maumivu makali sana unapo ondokewa na mpendwa wako.
Wangapi tulisikia walikufa kwenye utawala wake? Tuanzie hapo
 
Nitamkumbuka kwa mema yenye tija na maendeleo kwa nchi yetu. Hakika ni raisi wa kipekee kwangu aliutendea haki utendaji kazi wake bila kumuogopa binadam yeyote. Mungu ampumzishe kwa amani kiongozi wetu aliyekuwa na uthubutu wa kufanya mambo.

[emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992] [emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992][emoji992]l[emoji992][emoji992][emoji992][emoji992]
We utakuwa muangaliaji wa propaganda za TBC
 
Back
Top Bottom