Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Ukatili, ubabe, uuaji, kupoteza watu, kusigina katiba, kupirisha sheria kandamizi, wizi, kubambikia watu kesi, lugha chafu, hotuva za hovyo, mirdi isiyo ya tija, kukandamiza upinzani, uongo mfarakanishi hayo ni nusu tu.
Comments reserved
 
Nimekaa nikatafakari nikaona ile comment niloandika mwanzo ni kama kejeli so nimeifuta. Ki ukweli ntakukumbuka sana Magufuli kwa uthubutu wako kwenye kutekeleza ilani ya chama chako cha ccm. Ilani zilikuwepo ila uthubutu wa kuzitekeleza haukuwepo kwa waliotangulia. Tutakukumbuka na zaidi wanachama wa chama cha ccm watakukumbuka sana. Na sie wananchi tusiokuwa na upande wwt tutakukumbuka umegusa at least kila nyanja kwa uwezo wako na nafasi ulokua nayo. Mengine ni madhaifu ya kibinadamu tusameheane hatujui mwisho wetu nasi ni lini na utakuwaje.
 
Alivyokuwa anasimamia na kuikomalia miradi miradi na kutotuweka kwenye lockdown

Ova
 
Kuiba 1.5 trillion halafu kuuza nyumba z serikali na moja kumpa hawara yake Sundi Mollemo. Shetani mkubwa Magufuli
 
Kuna clip moja ambayo vyombo vya habari wanairudia rudia mara kwa mara.

Clip yenyewe ni moja ya hotuba ambazo hayati Magufuli alizitoa wakati wa uhai wake.

Maneno yanayosemwa kwenye clip hiyo ndiyo ambayo ni mada yangu kuu, kwenye uzi wangu huu.

Anatamka kuwa "Mtanikumbuka kwa mema wala si kwa mabaya yangu, nawasihi tusibaguane kwa vyama vyetu vya siasa, wala ukabila na udini na kamwe tusiache kumwabudu Mungu wetu" mwisho wa kunukuu.

Kwa maelezo hayo na namna alivyokuwa akiiendesha nchi hii vina umbali kama kutoka mbinguni hadi duniani!

Hebu turudie baadhi ya matamshi yake wakati akiwa hai.

Mkinichagulia mpinzani mtakuwa mnajichelewesha wenyewe maendeleo yenu!

Nyinyi wenyewe ndiyo mlifanya makosa safari iliyopita kwa kuchagua mbunge wa upinzani, safari hii msirudie kosa hilo!

Kaskazini (hususani mkoa wa Kilimanjaro) mlipendelewa sana katika awamu zilizopita, hivi sasa na nyinyi subirini, wakati maendeleo ninapopeleka kwingineko(akimaanisha mikoa ya kanda ya ziwa)

Wakati akiyatamka maneno hayo, alijua fika kuwa nchi yetu toka tupate Uhuru, imejengwa katika misingi ya umoja wa kitaifa, ambayo hatubaguani kwa vyama vya siasa, ukabila wala dini zetu, kwa maana nyingine ni yeye aliyetaka kuligawa Taifa hili.

Vile vile akifahamu kuwa tokea mwaka 1992, nchi yetu iliandika ndani ya Katiba ya nchi kuwa nchi yetu itakuwa ya mfumo Wa vyama vingi, jambo ambalo hayati Magufuli, alionekana wazi wakati Wa uhai wake kuwa anauchukia mfumo huo na alikuwa akitamani nchi yetu irejee kwenye mfumo wa chama kimoja!

Lakini haishangazi kwa hayati Magufuli kutamka maneno hayo, kwa kuwa tunajua fika kuwa alkkuwa ni mtu wa "double standards"

Anatamka Leo kuwa maendeleo hayana chama, wakati kesho yake anawaambia wapiga kura kuwa msinichagulie betri na gunzi!
 
Udikteta uchwara na watu wasiojulikana ,ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na utawala bora plus uvunjifu mkubwa sana wa demokrasia uliofanywa na huyu ibilisi Zanzimana .
 
Huyu mzee katuvuluga sana
Hakika ametuvuruga sana.............

Kwanza nawashangaa hawa TBC na vyombo vingine vya habari vya ndani, wakimwita hayati Magufuli, kuwa alikuwa shujaa wa Afrika!

Shujaa gani wa Afrika ambaye alikuwa haruhusu namna yoyote ya kukosolewa na kuamua kuwanyamazisha hata kwa wale waliokuwa wanatoa "critical critisism" katika utawala wake?
 
.
FB_IMG_1616709652129.jpg
 
Anatamka kuwa "Mtanikumbika kwa mema wala si kwa mabaya yangu, nawasihi tusibaguane kwa vyama vyetu vya siasa, wala ukabila na udini na kamwe tusiache kumwomba Mungu wetu" mwisho wa kunukuu.
Jamaa alikuwa 'conflicted' sana.

Ni kama mtu anayepambana na mashetani kichwani mwake, maanake mara nyingi alipokuwa akisema jambo jema, akiondoka hapo anakwenda kufanya kinyume kabisa na alichokuwa akikisemea.

Nadhani utashi wake ilikuwa atende mema, lakini kulikuwa na nguvu/msukumo mkali uliozidi utashi wake na kuanza kuangukia mabaya aliyotaka kuyaepuka.

Mfano wa maneno hayo ni ushuhuda kamili juu ya mapambano aliyokuwa akiyapitia kichwani mwake.

Kuna wakati mapambano yake, yale mazuri yaliweza kuyashinda yale mabaya.

Kwa mfano: Matukio ya watu kutekwa, yalikoma, mazuri yalipoyazidi mabaya, na ikaendelea kuwa hivyo. Kuna mengine mengi ya aina hiyo.
Mfano mzuri ni huo uliouweka hapo: Anasema "Maendeleo hayana vyama", na hapo hapo anakandamiza wapinzani na kuwaambia watu wakichagua wapinzani hatawaletea maendeleo.

Ni kama alikuwa na ukichaa wa aina fulani kichwani.
 
Jamaa alikuwa 'conflicted' sana.

Ni kama mtu anayepambana na mashetani kichwani mwake, maanake mara nyingi alipokuwa akisema jambo jema, akiondoka hapo anakwenda kufanya kinyume kabisa na alichokuwa akikisemea.

Nadhani utashi wake ilikuwa atende mema, lakini kulikuwa na nguvu/msukumo mkali uliozidi utashi wake na kuanza kuangukia mabaya aliyotaka kuyaepuka.

Mfano wa maneno hayo ni ushuhuda kamili juu ya mapambano aliyokuwa akiyapitia kichwani mwake.

Kuna wakati mapambano yake, yale mazuri yaliweza kuyashinda yale mabaya.

Kwa mfano: Matukio ya watu kutekwa, yalikoma, mazuri yalipoyazidi mabaya, na ikaendelea kuwa hivyo. Kuna mengine mengi ya aina hiyo.
Mfano mzuri ni huo uliouweka hapo: Anasema "Maendeleo hayana vyama", na hapo hapo anakandamiza wapinzani na kuwaambia watu wakichagua wapinzani hatawaletea maendeleo.

Ni kama alikuwa na ukichaa wa aina fulani kichwani.
Kalamu1
Washwahili wangeweza ita hali hiyo kuwa Mzee alikuwa na " mawenge" kichwani
 
Alidhani Chato itakuwa Paris, kumbe Chato unaenda kuwa mji wa magofu mapya
Hiyo Chato itageuka Gbadolite ya TZ

Ambapo "runway" ya ndege itaota nyasi na zile nyumba zilizojengwa chap chap, zitakuwa magofu na makazi ya popo!
 
Back
Top Bottom