Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
We will miss you for ever

Msikilize kwenye dakika ya 4:51
 
Moja ya Jambo linalothibitisha uimara wa kiongozi nipamoja na muda unaotumia ofisini kutekeleza majukumu yako pamoja na wivu ulionao dhidi ya nafasi uliyopewa.

Hayati Magufuli anaingia kwenye kumbukumbu za Dunia za kuhudumu muda mrefu( miaka mitano) bila kukasimisha madaraka yake au kukaimisha madaraka kwa mtu.

Kwamba kutokaimisha madaraka au kukaimisha Kuna faida ni Jambo lakujadili ila anahutaji pongezi kwa kukaa na waliompa madaraka bila kukimbiakimbia Dunia. Tumwenzi kwa kukaa ofisini na kuachana na sera zakupishana angani zilizodhulumiwa kuigharimu nchi fedha nyingi.
 
Haiyumkiniki labda hakutaka mtu akae karibu na anapokaa yeye ili kuficha mafaili yaliyokuwa yanaonyesha hasara kwenye miradi aliyotudanganya inaingiza hela na kutoa gawio kwa serikali kuu kumbe sivyo?

Refer issue ya ATCL!
 
Kwa dunia ya sasa unaweza ukawa Chato watu wasikufikie / washindwe kuku-approach lakini unaweza ukawa Toronto ukawasiliana na wadau kwa video conference na kuelewana kama vile mpo chumba kimoja
 
Sijamuuwa Meko na wala sikuwahi kumwombea kifo lkn ilimpasa Mungu kumwondoa ili Tanzania ipone.
 
Mbona watanzania mnaendelea kumtukuza mtu MFU wakati Tz ina watu wasomi,wababe na wajuaji zaidi ya huyo jiwe mnakera Sana kumzungumzia zungumzia mtu ambaye keshaliwa na funza huko udongoni[emoji51][emoji51]
 
Uchaguz Wa 2020 na ushindi wa kishindo wa CCM [emoji16]
 
This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
Utawala usioheshimu sheria na
Pili nitamkumbuka kwa mauaji na utekaji wa kundi la watu wasiojulikana
 
Nitamkumbuka kwa majibu ya hovyo.Sitasahau Siku ile alipokuwa kule mbezi alipomwambia yule bwana "abaki na mavi yake nyumbani"
 
This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti ( Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss , kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo..

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J.. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje , kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu , S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
Mi nitamkumbuka kwa ujasiri wa mradi wa Stiglaz.

Lakini vile vile nitamkumbuka kwa kodi za kubambikwa.
 
Duh, nime-miss sana yale maneno yake ya shombo! Jiwe bwana nimeanza kukumiss sana! Hakika Jiwe sitamsahau kwa hayo maneno yake!
1. Kama huna 200 piga mbizi,
2. Mimi niliahidi nitaleta tetemeko
3. Usipofanya kazi na usile, na usipokula utakufa
4. Ukija mjini mavi yako yaache nyumbani
5. Wewe mama unataka kupanuliwa wapi?
6. Wewe mzee ungekuwa nyumbani kwetu ningekupa mama yangu umwoe kabisa
7. Kwe ye utawala wangu hakuna mjamzito hata mmoja anarudi shuleni!
8. Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Alikuwa anafahamu wafanyakazi wa chini kama walimu kuwa nao ni wanyonge. Akaahidi kuwaongezea mishahara Zaidi ya mara 100% lakini Mwenyezi Mungu bhana - sio kama yule Athumani rafiki yangu wa Tandale.

Kamtenda kabla ya kuwaongezea hiyo mishahara - na hatakumbukwa kamwe kama aliwahi boresha maisha ya wanyonge. Hata wale machinga na wanyonge wengine wa vijini hamna aliyebadilishiwa maisha kwa kupitia hayo maflyover na madaraja na midege mikubwa mikubwa.

Kazi kweli kweli! Eti jana kuna ndege imetua Chato. Ni kweli?
 
Back
Top Bottom