Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Kwa kupandisha bei ya sukari... kuvuruga biashara ya korosho... kupiga wapinzani risasi... kuua demokrasia... miradi mikubwa...
 
Hakuna kiongozi ameweza kufanya makubwa kama magufuli, mbona kipindi kile, mishahara ilipandishwa lakibi huduma katika jamii ni za hovyo kuanzia miundombinu, huduma hospitalini, kilw mmoja kafanya yake ila huyu mzee kaenda extra miles.
kwa upande wangu hata huduma ziwe mbovu sana kwenye jamii ila mfukoni pesa ikiwepo naona fresh,utafurahia vip huduma bora kwenye jamii ukiwa huna hela,tunadanganyana mzee.yaan utolewe out na washkaj uone meza imejaa af mfukon huna mia ya kujitetea unafikir utafurahia kama wengne.,[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Wiki moja iliyo pita, nikiwa Njombe nilishuhudia vibanda vya machinga na kina mamalishe vikibomolewa kwa nguvu bila hata kuwatafutia mbadala.. na kufukuzwa kama vibaka wakati enzi za Magufuli hakuna mtu aliye wagusa machinga na kina mama ntilie ambao wanapata riziki zao kupitia hizi kazi zao ndogo ndogo.

Jana kule Tanga mtaa 12, vipanda vya kina mama lishe vimebomolewa kwa amri ya tajiri mmoja hapo mkoani.

Kina mama wameonekana kulia na kukosa mayimaini huku wakimtaja mama samia kwamba yupo wapi? Mbona enzi za Magufuli wamesomesha hata watoto kwa pesa za kudunguliza kupitia kazi zao, iweje leo wanafukuzwa kama mbwa.

Naona matajiri wamerudi na wanacho fanya wanatest kwa mambo madogo madogo hadi utawala wa awanu ya 6 uzoee na kuona ni sehemu ya maisha.

Mzimu wa huyu mzee ni balaa.

Huu wimbo wa alikiba, kila nikiusikiliza naona unaishi unabii wa Mzee Magufuli.

 
Watu mna roho ngumu kweli kweli? Hivi unaanzaje kumkumbuka shetani mtu?
 
Hakuna binadamu yeyeto duniani aliyewahi kuwasilence watu na akafanikiwa.
 
Kuwaweka wafanyakazi wa Uma miaka 7 bila nyongeza ya mshahara wala kupanda daraja. Hili haliwezi kusahaulika

Hii ilisaidia sana kwa wafanyakazi kujiongeza na kujifunza Ujasiliamali. Maana watu wengi walibweteka na mishahara yako.. Inchi ipo kwenye construction MODE. Pesa nyingi inatumika kugharamia miradi mikubwa ya kimkakati na kupitia hiyo miradi, ajira nyingi mpya zimepatikana. Hivyo basi, haikuwa rahisi kupandisha wafanyakazi madaraja ihali hakuna Pesa ya kuwalipa kutokana na kupanda madaraja katika sehemu zao za kazi.

Kitu ambacho tunatakiwa tukifahamu ni kwamba, JPM alikuwa na UTHUBUTU wa kufanya MAAMUZI MAGUMU kwa manufaa ya FUTURE ya Tanzania. Ingawa kwa Maamuzi hayo magumu, UKIMFU (upungufu wa Kinga Mfukoni) uliongezeka sana, but all for the better
 
Hii ilisaidia sana kwa wafanyakazi kujiongeza na kujifunza Ujasiliamali. Maana watu wengi walibweteka na mishahara yako.. Inchi ipo kwenye construction MODE. Pesa nyingi inatumika kugharamia miradi mikubwa ya kimkakati na kupitia hiyo miradi, ajira nyingi mpya zimepatikana. Hivyo basi, haikuwa rahisi kupandisha wafanyakazi madaraja ihali hakuna Pesa ya kuwalipa kutokana na kupanda madaraja katika sehemu zao za kazi.

Kitu ambacho tunatakiwa tukifahamu ni kwamba, JPM alikuwa na UTHUBUTU wa kufanya MAAMUZI MAGUMU kwa manufaa ya FUTURE ya Tanzania. Ingawa kwa Maamuzi hayo magumu, UKIMFU (upungufu wa Kinga Mfukoni) uliongezeka sana, but all for the better
Maisha ni leo sio kesho,kesho haiishi,tangu uhuru nchi inajengwa, huwezi wanyima watumishi haki zao za kikatiba kisha unajenga miradi igusayo maeneo machache huku haki za wengine zimesimama.
 
Kuna watu wamezoea kuishi kama watumwa kulingana na walivyolelewa.

Lakini kwa tuliolelewa kwa uhuru hakika tulionja ladha ya ukoloni.

Namwombea mama afute ukoloni, nchi yetu ipate uhuru wake tena.
watu wasijulikana na shambulio baya la Tundu Lissu.
 
Mosi Kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na kumaliza kabisa mbio na matamanio ya zaidi ya Wanachama 42 wa CCM kuwa Rais.
ii) Kuhamishia Serikali Dodoma na kuipa hadhi ya Jiji
iii) Kuanza Ujenzi wa Ikulu mpya kwa kutumia JKT.
iv) Kuanzisha Ujenzi wa Stigler's gorge HEP .
v) kuanzisha Masoko ya Madini kila Mikoa zenye Madini.
vi) Kuanzisha Maduka ya Madawa muhimu ya Serikali yaani MSD
vii) Kufufua TTCL
viii) Kufufua Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
ix) kufufua ATCL
x) Kufufua Viwanda vilivyokufa kama Tanlec, kurudisha Mali za Nyanza Cooperatives , nk
xi) kumteua CGP kutoka JWTZ hakika imeleta sura na taswira mpya ndani ya Magereza.
xii) kujenga Daraja la Tanzanite
xiii) Kusimamia ujenzi wa Barabara karibia 80% zimejengwa akiwa Waziri wa Ujenzi na Rais wa Nchi.
xiv) Kujenga Interchange za Dar
xv) Ujenzi wa Nyumba za Magereza
xvi) Ujenzi wa Hostel za UDSM,
xvii) Kuanzisha Mkoa mpya wa Songwe,
xviii) Kuua Vyama vya Upinzani
Xix) Ujenzi wa Uzio wa Mererani kuzunguka mgodi wa Tanzanite,
xx) Kuwapatia na kuwajengea Wachezaji wa Taifa Stars Viwanja pamoja na Nyumba
xxi) Ujenzi wa Viwanja vya Ndege akiwa Waziri wa Ujenzi na Rais ,
xxii) Ununuzi wa Rada 4 za kuongozea Ndege,
xxiii) Ujenzi wa SGR,
xxiv) Ujenzi wa Hostel mpya za MUST
xxv) Kusomesha Wanafunzi wa Kidato ha kwanza hadi cha Kidato nne bila malipo
xxvi) Kutosafiri kwenda Ulaya akiwa Rais,
xxvii) Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Musoma (Kwangwa)
xxviii) Uanzishaji wa Hifadhi ya Nyerere
xxix) Uanzishaji wa Hifadhi ya Burigi-Chato
xxx) Uanzishwaji wa Kampuni ya Twiga Corp.
xxxi) Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Mtwara
xxxii) Ujenzi wa Hospital ya Uhuru Mkoani Dodoma
nk

Pumzika kwa amani Hapa Kazi Tu.
 
Jana usiku nilienda kumtembelea mzee mmoja ambaye ni mtu wangu wa karibu anae jihusisha na biashara ya madini,akinipa story fupi tu ya rafiki yake ambayo ilinihuzunisha sana.

Jamaa yake alikua na zaidi ya bilioni 7 kwenye account yake bank mwaka jana mwanzoni,alipigiwa simu na branch manager aende urgently na alipofika pale mida ya mchana akajulishwa kwamba account yake imepigwa spana na tra (task force). Ikabidi aende tra mkoa ili kufuatilia hiyo ishu.

Tra mkoani wakamwambia inabidi awasiliane na TRA makao makuu,ikapigwa sim akapewa appointment saa tatu asubuhi next day. Akapanda ndege jioni hiyo kuelekea huko, asubuhi kafika mapema kasechewa kweli kweli then akaingia ofisini kuzungumza na team roho mbaya.

Wewe ndio fulani? Ndio, inaonekana una pesa nyingi sana kwa account ila hulipi kodi. Jamaa akasema akasema kodi nalipa na ninapata tax clearance kila mwaka mbona sielewi? Wakamwambia ana option 2 TRA wachukue 5B wamuachie 2 au akalete vielelezo huku wakiendelea kuzuia hela zote. Vielelezo visipo jitosheleza watachukua hela zote pamoja na kesi ya uhujumu uchumi.

Pale ulikua huruhusiwi kwenda na mwanasheria wala accountant,jamaa akatoka nje kufikiria kwa muda akaona isiwe nongwa akawaachia 5B lakini pia akaambiwa arudi CCM kwa kujitangaza kwenye media kwa sababu alikua supporter mkubwa wa lowasa uchaguzi wa 2015.

Matajiri wengi wa mawe wameumizwa sana huko kanda ya kaskazini ila wamekaa kimya tu,bora huyu jamaa amekufa maana alikua anatupeleka shimoni/motoni kiuchumi na kijamii.
 
JPM alisema tutamkumbuka kwa mazuri. Je, wewe unakumbuka mazuri yapi?
Naanza mimi. Nakumbuka haya mawili yenye ufanano aliyoyakuta JPM na akayafyekelea mbali.

(1) Nakumbuka Enzi zile za utumwa ambapo Madawa ya kulevya yalitapakaa mithili ya MAHARAGE na UNGA.
Wakati ule, mtu akishikwa na yale Madawa ya kulevya, vyombo vyombo vyetu vilimlinda mhalifu ili asidhuriwe, mbaya zaidi ilikuwa yale Madawa yakipelekwa kwa mwenye mamlaka ya kubainisha ikiwa ni Madawa au la, yeye alisema kuwa, vipimo havioneshi kuwa yale ni Madawa. Ilikuwa balaa tupu.

(2)Kubwa zaidi ni lile la ndugu zetu walemavu wa ngozi(Albino) kukatwa mikono mchana kweupe.
Hali kadhalika Wakati ule ilikuwa ni lazima huo mkono uliokatwa ili kuthibitisha kama ni wa Albino au la kwenda kwa mwenye mamlaka ya kubainisha hivyo.
Kwa bahati mbaya, majibu yalipindishwa. Watu waliambiwa eti kilichoonekana si mkono wa Albino bali ni wa mnyama ambaye si binadamu. Ilikuw ovyo kabisa.

RIP, Commando wetu,JPM.
 
Mazuri ya Magu yapo kwenye vitu ila hivyo vitu utakuwa vimeumiza watu wengi kiasi kwamba unaweza kuyasahau mazuri
 
Kuwanyonga watumishi wa umma kwa kuto wapandisha madaraja na kuto kuwaongezea mishahara, kuwahenyesha wakulima wa korosho baada ya kuingilia mchakato wao wa kuuza korosho zao, bomoa bomoa ya kibabe kule Dar, kudhoofisha upinzani wa nje na ndani ya chama, ukaidi, ukabila, ubaguzi, u umungu mtu, na mazuri mengine meeeengi!!
 
Hivi alikuwa na mazuri yule mwendazake?
Watu tunapumua sasa alikuwa ana roho mbaya yule baba
 
Alianza vizuri akaponzwa na wale majirani wabaya waliokacha kuja kumzika
 
Back
Top Bottom