Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
kwamba kipindi chake umeme ulikuwa haukatiki?
umesahau mpaka nyuzi za malalamiko zilivyotamalaki humu Jf?

Tatizo watu wanajidai kusahau, kutokutangazwa kuwa umeme haukatiki sio kuwa ni kweli haukatiki. Umeme ulikuwa unakatika, sema Shujaa alipiga marufuku kutangazwa migao, ikawa inaendelea chini chini. Mfumo wa Luku pia umewahi kusumbua hii si mara ya kwanza. Na yote haya taarifa imetolewa.
 
..Usihofu vumilia Nyerere Dam inakaribia kukamilika tatizo la kukatika umeme litakuwa historia, na mwingine tutauza kwa majirani!
 
Sukuma Gang! Watu wa "Doho shida" wanapenda kusifia hata ambayo havistahili... Si ajabu hata ukiwaibia mke unaweza kusifiwa tu na Sukuma Gang, Watasema "Ole ngosha gete"..
 
Hivi kipindi cha Magufuli umeme si kuna kipindi ulikuwa unakatika nchi nzima hadi watu wakaanza kuhisi kuna mgao wa kimya kimya?
Nakumbuka ilikuwa mwezi Februari mwaks huu hadi watu wakaanza kuhoji hiyo reli ya SGR itatengenezwaje
Unaishi wapi mkuu? Mi sijawahi shuhudia umeme ukikatika siku mzima kipindi cha JPM. Na tulipewa taarifa.
 
..Usihofu vumilia Nyerere Dam inakaribia kukamilika tatizo la kukatika umeme litakuwa historia, na mwingine tutauza kwa majirani!
Kwa nchi kama Tanzania sababu waga haziishi, Unaweza kuambiwa hata maji yameanza kupungu, mara sijui Turbines zinafeli kuzunguka, au upepo ni mkali sana eneo la Rufiji una sababisha maji yanarudi kinyumenyume hivyo mashine hazizunguki..

Hii nchi ngumu sana..
 
Usimkumbuke kwa kukosa kuajiriwa miaka 2 sasa unapuyanga mtaani umkumbuke kwa tatizo la kiufundi la Tanesco? We wa wapi wewe
Kusoma sio lazima uajiliwe na serikali. Mi mingekuwa na mindset kama zako...sasa hivi ningekuwa nazunguka mtaani na bahasha zangu. Ila Kwa sababu nilijua suala ajira ni shida dunia nzima niliamua kutoka ili nijishughulishe na inshallah baada ya miaka2 nategemea kufungua shule ya watoto. Vipi mkuu, unatafuta kazi?
 
Swala la kukatika umeme ni tangu Magu yupo, ulikuwa unakatika asubuhi unarudi usiku daily na hakuwahi kuliongelea hata siku moja
 
Kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita ilikuwa ni kwa public interest?
Kununua viongozi wa upinzani ilikuwa ni kwa public interest?
Kumtwaga marisasi yote lissu ilikuwa ni kwa public interest?
Kufungia account za watu na kuwapora fedha zao ilikuwa ni kwa public interest?
Ukiambiwa ulete uthibitisho utapeleka? Nenda mahakamani mkuu.
 
Tanesco wenyewe wanajionea poa tu sababu wako peke yao kwenye soko la usambazaji wa umeme, kwa hiyo, hutawakimbia, utaendelea kuwavumilia tu.

Ambacho serikali yetu inatakiwa kufanya ni kuwaagiza Tanesco wajikite kwenye uzalishaji na usafirishaji tu wa umeme, huku kwenye usambazaji wa umeme kuwe na kampuni zaidi ya moja ikiwemo na hiyo Tanesco kama ikipenda.

Kama kampuni mojawapo ikikuzingua na huduma zao mbovu unaipiga chini, unaenda kwa kampuni nyingine, maisha yanaendelea, na hata bei ya umeme ingeshuka zaidi kwa sababu tungekuwa na ushindani wa kibiashara. Kama hawajui hilo linawezekanaje, waende UK wakajifunze.
 
Unaishi wapi mkuu? Mi sijawahi shuhudia umeme ukikatika siku mzima kipindi cha JPM. Na tulipewa taarifa.
Acha mambo yako! Hapa npo naishi mtaa wa Bugando, jijini Mwanza Toka mwezi wa 12 mwaka jana mtaa jirani wa Igogo kusini kila siku umeme ikifika saa 1 lazima ukate na urudi saa 5 au 6 usiku na siku zingine asubuhi ya siku inayofata, ila kuanzia mwezi wa 3 mwishoni tatizo halipo saiv naona umeme upo 24hrs labda zitokee inevitable emergencies za kawaida...
 
Back
Top Bottom