Kwanza nianze kwa kukiri kwamba mimi ni sio mwanasiasa ila kwa kipindi fulani nilikuwa shabiki mkubwa wa chadema. Kiukweli miongoni mwa wale waliokuwa wakimponda sana na hata kutokuhuzunishwa na kwenda kwa mwendazake na mimi nilikuwemo. Ninakiri wazi kuwa nilifanya makosa makubwa sana na sikujua kuwa nilikuwa nakataa almasi kwa kukusanya kokoto.
Ni miezi miwili sasa mzigo wangu umekwama bandarini kwa madai kuwa taratibu za ushuru kutokukamilika hali ya kuwa risiti zote halali ninazo. Mbaya zaidi ni mzigo wa biashara hivyo kadri muda unavyoenda nazidi kupata hasara.Sikujua kuwa ukali wa kiongozi mkuu unaweza kusaidia watendaji wa chini wakatimiza majukumu yao kwa weledi na uharaka kwa kumjali mwananchi.
Pili hali ya umeme huku mtaani kwetu ni tete, Kila mara umeme unakatika,Na mita za luku system hazifanyi kazi mara kwa mara umeme haununuliki. Ninajiuliza mbona kipindi cha mwendazake haya mambo hayakuwepo? Ina maana utendaji wa hawa wafanyakazi unaangalia zaidi kiongozi mkuu aliyepo juu yao?
Kiukweli nimeshuhudia mambo mengi ya hovyo ndani ya muda huu mfupi, Tukiachilia mbali la kuahirishwa mechi ya Simba na Yanga bila kiongozi yoyote kuchukuliwa hatua, Madawa ya kulevya yameongezeka kwa kasi huku mitaani, wizi na ujambazi navyo vinashamiri ndani ya muda mfupi,Kwanini?
Kwakweli niseme tu kuwa ninajuta sana kumponda mwendazake popote alipo anisamehe na Mungu anisamehe.Na ninamuombea azidi kupumzika kwa amani.