Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Kwahiyo unajustify kuwa watu wote waliokuwa ni wabaya au?

Hapa jamii forum kuna visa sana kwahiyo hawa walio hai ndio wazuri sio??

Kweli, when Trust gone Sorry is Nothing
 
Kila binadamu anamapungufu yake,hata waliopo nao wanamapungufu yao pia tena mengi tu.........
 
Kwa kawaida mtu anayefuata utaratibu watu wazembe, wasiopenda kufanya kazi, wanaopenda magumashi humuona mtu wa aina hiyo akiwa hivyo mleta mada anavyomzungumzia Magufuli.

Aliwabana sana matapeli,wezi na wauza unga waliokuwa wanajifanya watu wema kwenye jamii kumbe behind the scenes wanafanya mambo haramu sasa ile iliwakasirisha mno watu wa aina hiyo.
 
Kwa hiyo kuongea na hao watu kunamfanya umjue?wewe kama wewe unamjuaje in personal?
 
Magufuli alizidisha UBAYA.

POLE KWA KUCHELEWA KUYAJUA HAYA MKUU.

MZEE ALIKUWA.
MKALI KUPITILIZA.
MJUAJI KUPITILIZA.
VISASI KUPITILIZA.
UBAYA KUPITILIZA.

Mimi namfahamu kitambo jamaa Alikuwa mtu Mbaya KUPITILIZA.
 
Mvua zimeenda na Magufuli, tangu aondoke na mvua zimeenda. Alianza na mvua nakumbuka wakati ana apishwa mvua ilinyesha uwanjani, na ndani ya utawala wake mvua za vuli na masika zilinyesha kwa wakati na za kutosha misimu yote.
 
Habari!
Mwaka 2014 nikiwa mdanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu chini ya Barrick na baadaye kuwa chini ya acacia niliwahi kutamka jambo mbele za watu kuwa nchi hii ya Tanzania ilipaswa iwe mikononi mwa Magufuli kama RAIS ndio ifike pazuri. Mmoja wapo akanupinga akasema Mimi natokea Chato tena nimesoma shule ya sekondari Tunduru inayomilikiwa na Magufuli. Huyo mtu namjua hafai kuwa Rais.
Mwaka 2015- 2022 nimekutana na ndugu wa damu wa Magufuli, watu aliofanya nao kazi akiwa Waziri wa wizara mbalimbali, watu aliosoma nao primary, sekondari na chuo.
Magufuli alikuwa na roho mbaya sana sana.
Nimeongea na madereva 2 waluomwendesha kabla hajawa Rais, nimekutana na kuongea naye msaidizi wake mmoja alipokuwa wizara ya Ujenzi . Nimeongea na mtu aliyelinda nyumba yake zaidi ya miaka 20.
Nimeongea na aliyekuwa mkuu wa idara fulani wizara ya Ujenzi.
Kwa ufupi yule mzee alikuwa katili na mwenye roho mbaya.
Unaweza kuniuliza hao watu nimewatoa wapi na kwanini niwahoji mambo ya Magufuli?
Ni kwamba tunakutana kwenye kazi na ndipo huanzisha stori za Magufuli hapo ndipo ninawachimba kwa viswali vidogovidogo.

Punguza kidogo chai.unaweza kuwa umeongea ukweli ila chai ni nyingi zaidi,imagine hata mlinzi wa nyumba yake mlikutana kozi
 
Magufuli alizidisha UBAYA.

POLE KWA KUCHELEWA KUYAJUA HAYA MKUU.

MZEE ALIKUWA.
MKALI KUPITILIZA.
MJUAJI KUPITILIZA.
VISASI KUPITILIZA.
UBAYA KUPITILIZA.

Mimi namfahamu kitambo jamaa Alikuwa mtu Mbaya KUPITILIZA.
UNAMFAHAMUJE?Tupe ushuhuda wa jambo alilowahi kukufanya wewe kama wewe
 
1.Chato International Airport
2.Chato National Park
3.Trafic light Chato
4.3 star hotel Chato (TANAPA)
5.Bohari ya kanda madawa Chato
6.Hospital ya rufaa Chato
7.Stadium (proposa)
8.CRDB Chato
Hivyo vyote vilitakiwa vikae makao ya mkoa, Geita mjini lkn yy akapeleka huko Chato.
Apumzike kwa amani.
 
Yani ukweli ni kwamba utawala wa aina ile ndio unafaa kwa taifa hili.

Utawala huu kuna mijitu mibovu🙆, mindoige haswa yani limtu linakula pesa za watu linatangazwa hadi bungeni alaf bado linachekewa, Yani kuna marais ban kama vile sio marais yani ni mambo ya aibu sana.

Kipind kile hiyo migari mikubwa, mibus yote iliagizwa na wale walipa kodi hao wengine wote waliuza hadi kampuni zao na wengine kuzisambaratisha kabisa.

Safari hii tumewezwa walah🙌🙌🙌🙌
 
  • Thanks
Reactions: nao
Siku SGR na Stigers gorge vikikamilika ndio siku ambayo wananchi wa taifa hili wataomba kwa vinywa vyao itengwe siku maalumu kila mwaka ya kumkumbuka kama tunavyofanya kwa Mwalimu Nyerere
Kukamilika ni moja, kutoa huduma iliyokusudiwa ni jambo tofauti.
 
View attachment 1734652
Picha: Hayati Rais Magufuli enzi uhai wake

This is a special thread and a tribute to the late J.P.M.

Najua tupo katika kipindi cha masikitiko kama taifa, Jemedari wetu amefariki dunia, kama lisemavyo neno la Mungu katika kitabu cha biblia kuwa mfalme hawezi kuokolewa kwa na jeshi lake kubwa bali ni Bwana hutuponya na mauti (Zaburi 33:16), yaliyoandikwa yametimia Mungu amlaze mahala pema peponi.

Hakika tutammiss, kama ule usemi usemao umuhimu wa mtu huonekana zaidi asipokuwepo.

Yafuatayo ni mambo aliyonikosha J. P. M (R. I. P).

1. Nidhamu kwenye taasisi za serikali, kuanzia matumizi, utendaji wa kazi na utoaji wa huduma.

2. Msimamo bila kujali nchi nyingine zimeamuaje, kimsingi maamuzi mengi yalifanywa kuzingatia maslahi ya nchi sio mkumbo ( i.e chanjo ya corona).

3. Super-Mega projects zenye maslahi ya muda mrefu, S.G.R, Nyerere, Mwendokasi n.k.

4. Kuwanyoosha majirani zetu walizoea kutuibia na kutuchezea michezo ya ajabu ajabu.

5. Kuleta siasa za kuambiana ukweli na sio za kubembelazana hovyo.

6. Kukomesha ujambazi na matukio ya kihalifu majumbani.

7.

Itaendelea...

PIA SOMA>> TANZIA - Rais John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar
kutuvusha kwenye janga la Dunia covid
kuwanyoosha vyeti feki ambao ndio watz lialia leo hii wakati walidhulumu nafasi za wasomi wetu
kurudisha nidhamu makazini hasa serikalini
 
Tutamukumbuka Kwa Teka Teka (wasiojulikana) siasa afanye yeye wengine uhaini kesi za KUBAMBIKIWA zilikua nyingi tu nunua nunua wabunge me wa upinzani uhujumu uchumi ilikua fashion hata mwandishi wa habali anahujumu Kwa ujumla yapo mengi ya kumkumbua Ashukuliwe sana (Mungu wetu) lefa wa dunia Kwa kipyenga chake pale mzena japo alichelewa kidogo
 
Alitufirisi Mimi na partner wangu alichukua 99% ya hela yetu ikaleta BP kwa partner wangu akaja akapata stroke akafariki! Mwendazake was a devil to me my family and all those close to me.
 
Kwa kweli sijafurahi kabisa kumpoteza kiongozi mahiri kama john pombe magufuli alikua hodari sana katika uongozi wake mianya ya rushwa alikomesha, uonevu, huduma katika taasisi za kiserikali zilikua zikitolewa kwa heshima na bila ubaguzi, kajenga miradi mingi sana nchini, elimu bure, miundombinu, hudumu hospitalini ziliboreshwa, huduma za maji mikoa mbalimbali alitoa fedha miradi ikamilishwe, uwanja wa ndege wa mwl Julius Nyerere aliukarabati kwa ufupi Rais wangu kifo chako John Pombe Magufuli umeniachia simanzi moyoni mwangu.
Kiongozi bora kuwahi kutokea TZ tunakumbuka daima
 
Kabla ya Hayati Magufuli Wananchi tukio wengi tulikwama kwenye tope la umaskini na hatukuona matumaini ya kukombolewa bali tulikuwa tunapata taarifa za ubadhilifu,Wizi, upendeleo na uonezi ambao ulikuwa hauitaji ushahidi.
Wachache walikuwa matajiri wenye DHARAU na dhiaka shopping Dubai NK. KULIKUWA NA kila Aina ya Ufisadi.

Wananchi katika kila majadiliano tulikuwa na hamu ya kumpata mtu wa kututoa kwenye tope hilo na kwakuwa tulikuwa na hasira na wanaotufanya tuishi maisha magumu tulitamani wapate adhabu ili wateseke Kwa kiwango kilekile tulichoteseka.
Tatizo kubwa hatukuwa na uwezo wakuwajua wabaya Wetu wote hivyo Ilikuwa rahisi mtu yeyote kutuaminisha kwamba maadui zetu anawajua na anauwezo wa kuwatia adabu.

Marehemu alionesha Nia ya kututoa kwenye tope lakini naye alipopewa kazi nadhani alipata asichotarajia kazi ikawa ngumu kila alipojaribu kugusa sehemu alijikuta anapambana na matawi makubwa lakini mizizi IKIWA imejichimbia Chini Vita ikawa ngumu akabakia peke yake nasi wanyonge hatukuwa na uwezo wa kumsaidia ingawa kunawakati alihitaji msaada Wetu.

Mpaka Leo bado tunahitaki idea yake ingawa Kuna maeneo yatahitaji MABORESHO.
 
Kitendo cha kuhimiza Ajira zote zipitie PSRS imekuwa n tumaini kubwa sana hasa sisi watoto wa st.kayumba
May your soul to continue to rest in eternal peace ✌🙏
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom