Endapo Magufuli angetawala hadi 2025 au 2030 kama ilivyokuwa ikitamkwa na wapambe wake wa kisiasa, bhasi Watanzania walikuwa wanapelekwa kuzimu.
Hebu fikiria Magufuli katawala miaka 6.
1. Miaka 6 Hakuna mtumishi yeyote alopata hata shilingi ya nyongeza ya mshahara ilihali gharama za maisha zilikuwa zinapanda kila uchwao
2. Miaka 6 Hakuna watumishi walopandishwa vyeo
3. Miaka 6 hakuna ajira mpya kwa graduates ilihali wastaafu waliongezeka na upungufu wa watumishi ulikuwa mkubwa
4. Makampuni kufunga biashara Tanzania na kuhamia nchi zingine ilianza kuwa jambo la kawaida
5. Watanzania kukimbia nchi yao ikawa kawaida, wapinzani wakaminywa pumzi na hakuna alohema
6. Uhuru wa vyombo vya habari tayari ulishanusa kuzimu, baadhi ya vyombo vikafungiwa na wanahabari wengine wapo kuzimu hadi leo
7. Hakuna project yeyote ya binafsi iliendelea kipindi cha magufuli, hata kujenga nyumba watu waliacha kama sio kuogopa, hakuna hata kituo cha mafuta kilidiriki kufunguliwa ispokuwa puma.
Kama sio kuzimu Magufuli alikuwa anatupeleka wapi???