KERO Je, UTT AMIS kuna kitu kinafichwa bila sisi wanachama kujua?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwanachama wa mifuko kadhaa UTT na kwamba UTT wamefanya maboresho ya program ambapo program iliyokuwa inatumika zamani imefungwa tangu tarehe 01/03/2026.

Sasa tatizo lililopo ni kwamba taarifa zetu hazijahamishwa automatic toka kwenye mfumo wa zamani kuja kwenye mfumo huu wa sasa ambapo ili taarifa zako zihamishwe unapaswa kwenda ofisini kwao ujaze fomu ya maombi hayo ili taarifa zetu zihamie kwenye mfumo wa sasa ili tuweze kuona Maendeleo ya akaunti zetu.

Hapa kwenye maombi ya kuhamisha taarifa zako ndipo pamekumbwa na utata Kwasababu watu wengi tuliojaza form za maombi hazijajibiwa ni mwezi sasa na hakuna majibu ya kuridhisha hata ukipiga simu makao yao makuu hazipokelewi jambo ambalo naona sisi kama wanachama pengine tunafichwa baadhi ya taarifa.

Ni vema sasa ofisi itoke hadharani itujulishe ni nini kinakwamisha taarifa zetu kuhamishiwa kwenye program mpya ili hatimaye tujue maendeleo ya fedha zetu.
 
Kwa tuliokuwepo kipindi cha magu tukashuhudia kilichotokea kwenye mifuko ya hifadhi Za JAMII Na acc Za watu binafsi Za Benki tunaamini Tz Bado si salama kwenye kufanya biashara ya uwekezaji Kwa kutegemea faida ya kuweka fedha ili upate Pesa hivo hivo,yaani kuzungusha faida Kwa kutegemea mzunguko was fedha kwenye taasisi Za fedha,,,hata kama siyo leo Ila IPO siku humo UTT kutapasuka
 
Huu m-kitu waΓ³ unaoitwa sijui UTT, kuna kipindi nilitukanwa sana hapa. Ni siku za nyuma kidogo, na kisa ilikuwa ni kuhoji usalama wa fedha za wanaoweka na kuuliza ili nipate kujua zaidi. Mimi tangu siku nyingi, kuna kitu huwa haki-click ninapopitia matangazo na profile yao na wafanyakazi wao. Sisemi ni utapeli ila watu wajaribu kuwa wachunguzi zaidi kabla hawajafanya maamuzi ya uwekezaji.
 
Tumia USSD code *150*82# utapata balance na ministatement ya account yako.
 
Acha upotoshaji mkuu
 
Ulimuhoji nani? Hapa jf kuna wawakilishi wa UTT? Msipende kusambaza uzushi wa aina hyo..

UTT siyo kikoba kiasi kwamba wanakaa na hela yako,ile pesa inawekezwa.

Kama serikali ina nia ya kuondoka na pesa zenu wanaweza hata kubeba huko kwenye accounts zenu za benki,ama kwenye simu ama hata kwenye hisa...ama hata kwenye Bonds za serikali.

Unaijua Gov bonds wewe ama hati fungani ya serikali?? Huko serikali kupitia BOT hukusanya pesa ya kutosha kupitia minada mbalimbali..mbona hamjawahi kuhoji usalama wa hizo pesa??
 
Umemaliza kila kitu
 
Kwahiyo Mkuu ni lazima uende ofisini kwako kwa ajili ya updates au ? Mtu yupo Namtumbo inakuwaje?
 
Kwamba UTT ni Kalinda na DECI iliyo changamka sio...πŸ˜‚

Muda wowote parapanda inalia. Mzigo unanyakuliwa.
 
Kwamba UTT ni Kalinda na DECI iliyo changamka sio...πŸ˜‚

Muda wowote parapanda inalia. Mzigo unanyakuliwa.
Unashangaa kila ukigusa mfumo haufunguki watu wanatokomea na kibunda πŸ˜‚πŸ˜‚
Mara pap BOT inawakataa mnaaambiwa ule ulikuwa Mpango wa CEO msitaafu na haukupita kwenye mifumo harali ya manunuzi ya umma

Utan tuπŸ˜‚πŸ˜€πŸ€­
 
Unashangaa kila ukigusa mfumo haufunguki watu wanatokomea na kibunda πŸ˜‚πŸ˜‚
Mara pap BOT inawakataa mnaaambiwa ule ulikuwa Mpango wa CEO msitaafu na haukupita kwenye mifumo harali ya manunuzi ya umma

Utan tuπŸ˜‚πŸ˜€πŸ€­
Hahaha usinikumbushe upatu kha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…