speedcom
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 320
- 179
Pamoja sana kaka nawe ukituletea unayojua itakuwa safi sana haswa utayogundua kwa mafundi!!!!
Mkuu tatizo la gari langu lilizidi sana, ikawa inazidi kukosa nguvu, na pia spark plugs zikawa zinakufa ndani ya wiki moja, mbili hivi.
Baada ya jitihada nyingi J3 hii tukashusha tenki la mafuta; tukatoa mafuta yote. Ni kwamba chini kabisa kulikuwa na mafuta kiasi cha lita tano ambayo yalikuwa na rangi nyeusi na hayakuchanganyika na yale ya juu. Baada ya kutafakari sana tukaona kama kuna tanker lililokuwa linabeba kitu kama molases na ikabeba mafuta ya petroli kabla ya kufanyiwa usafi. Naona mabadiliko, labda huenda tatizo likaisha.