michu03
Senior Member
- Dec 1, 2018
- 132
- 95
Nimekutana na kauli nzito ya mjasiriamali wa teknolojia Isaya Yunge kuhusu changamoto wanazokutana nazo wabunifu wa Kiafrika katika zama mpya za Artificial Intelligence (AI).
Amesisitiza kuwa AI ni fursa ya kizazi hiki – inaweza kuleta mageuzi katika uongozi, uchumi, usalama, na hata Universal Basic Income (UBI). Lakini anasema wazi kuwa vijana wa Afrika hawana msaada wowote wa ndani ya bara, hawapewe nafasi ya kuunda suluhisho za AI zilizo localized kwa lugha au mazingira yao. Wanaishia kupewa tuzo, lakini si mikataba au uwekezaji wa kweli.
Yunge anadai viongozi wa Kiafrika hawataki kujihusisha na mabadiliko haya, na badala yake huwakatisha tamaa wabunifu wa kweli. Anashauri vijana "kutoka Afrika" na kuwa raia wa dunia ili waweze kufanikisha mawazo yao bila kukandamizwa.
Maswali ya msingi kwa wanajukwaa:
1. Je, kauli ya Isaya Yunge ni ya kweli? Kwa nini ndiyo au hapana?
2. Tuna mifano gani ya mafanikio au kushindwa kwa wabunifu wa Kiafrika katika AI au teknolojia ya kisasa?
3. Je, viongozi wetu wanafahamu au wanapuuza umuhimu wa mapinduzi haya?
4. Vijana wabunifu wa Afrika wanatakiwa kweli kuhama bara au kuna matumaini ya kufanya ndani ya Afrika?
5. Tunawezaje kuleta mabadiliko halisi kwa mazingira ya ubunifu nchini?
Naambatisha pia picha ya ujumbe wenyewe kwa muktadha.