Je, Viongozi hao kuhudhuria hafla za makanisani ni mpango wa kuwagawa wakristo kwa sababu ule upande wako pamoja kuhusu DP World?

Kwahiyo kondoo, Raisi na Serikali yake wametishika? 😜

Waambie wasiogope bana, lakini na Serikali pia isiwatumie vibaya viongozi wa dini kuwahadaaa kinafiki kwamba kila hafla ya serikali viongozi wa dini hupewa nafasi ya mwanzo kusema au kuomba mpaka ikulu.

😜 Lakini waikiikosoa serikali tu pale ambapo wanaona kunaweza kuhatarisha umoja na amani kitaifa, utaskia ooh wanachanganya dini na siasa 😜.

Kwahiyo mnavowaalika kwenye majukwaa yenu ya kisiasa na dhifa za kitaifa na kuwapa nafasi za mbele kabisa huwa mnachanganya mahindi na mchele au ni nini?

Au mambo yakiwa shwari sio mchanganyo wa dini na siasa ila mkiambiwa ukweli ndio kuchanganya dini na siasa.

Kwani pale Mahakama kanda ya Mbeya ilipotoa hukumu ya kesi ya Mwambukusi kupinga mkataba wa dipi weldi , iliposema mkataba wa uwekezaji wa dipi weldi na Serikali ya Tz hauna shida ila zipo kasoro zinaweza kurekebishwa, je hii tunaitaje?

Kwani hawa viongozi wa katoliki mbona ni kama vile hawana shida na mkataba wenyewe ispokua wanachodai ni hizo kasoro kurekebishwa tu na mambo yaende.....

Na hawa wakatoliki inaonekana ni wasomi mno, wanachofanya ni Maandamano ya kisayansi na kisaikolojia tena yasiyo na na kibali cha mwanadamu bali Mungu. Hii ni hatari sana, na serikali imeshindwa na kamwe haitaweza kabisa kuyazuia. Na naskia yatuendelea kwa majuma 6 zaidi.

Na Viongozi wa Maandamano wamejiorodhesha hadi majina πŸ€“ ni Maaskofu 37, halafu waandamaji ni maparoko, waamini wote wakatoliki waliohudhiria misa Jpili, viongozi wa Jumuiya na familia zote za kikatoliki, dah! akili nyingi bana saa zingine 😜

Sasa utawaweka jela gani, halafu naskia na wao wanajilaumu kutokuchukua nafasi za uongozi chaguzi zilizopita licha ya kuhamasishana kupiga kura.
Wanajutia if you don't want to take part in political administration don't blame to be ruled by a fool.

Safari hii sijui itakuajee 2024-2025....
 
Akili ndogo haiwezi shindana na akili kubwa hata siku moja
 
Ishu ni kuzijibu hoja zao.
Ukitaka kujua nguvu za Imani subiria uchaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…