Je, viongozi kama Mwigulu wanavyoanza kuwaandaa watoto wao kushika madaraka wanatamani uongozi wa kiimla?

Je, viongozi kama Mwigulu wanavyoanza kuwaandaa watoto wao kushika madaraka wanatamani uongozi wa kiimla?

Yaani siku hizi jamii forum limeshapoteza mvuto, kwa mada za kipuuzi Kama hizi, wewe mtoa post huna kazi za kufanya yaani unafuatilia mpaka unajua mtoto mwigulu kila siku alikuwa ana vaa nguo mpya.!
Umeona lakini hadhira aliyokuwa anaitembelea! Yaani ni hadhira iliyochoka mbaya lakini mwangalie sasa mtoto na baba yake. Wewe unaweza ukaona kawaida lakini jicho la kisanaa linaona utofauti! Huwezi elewa wewe uliyekulia kwenye mboga tano family.
 
Dkt Mwigulu Nchemba hivi karibuni alifanya ziara yake Wilayani Iramba na karibia sehemu zaidi ya kumi mwanae Isaac Mwigulu Nchemba alipata nafasi ya kuhutubia.

Sehemu zote hizo mwanae huyo alikuwa amevaa mavazi mazuri sana ya CCM yenye gharama kubwa.

Hakuna sehemu aliyotembelea aliyoonekana akiwa amerudia nguo hizo hizo. Mtoto yupo darasa la tano sijui la sita lakini anaonekana tayari ni mtoto mwenye ukwasi.

Mwanae huyo alijinadi kuwa ni Mwakilishi wa Chipukizi Wialaya ya Iramba Taifa na pia yeye ni Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Iramba. Zaidi ya yote anasema yupo ziarani kuwashukuaru waliomchagua (hadiray yenyewe sasa?) kujifunza.

Anongea hayo yote wakati baba yake Mheshimiwa Mwigulu Nchemba yupo pembeni akiwa ameshika maiki na mikono yake mfukoni. Yaani ni dhihaka kubwa sana unaiona pale, kwani kuna akina bibi wamekaa chini wamechoka na Isac anaenda kuwainua pale. Zaidi ya yote katika speech ya mwanae huyo anamsifia baba yake ati "Dr Mwigulu Nchemba oyee!". Kazi ipoooo!

Hoja iliyopo ninaona kabisa Dr. Mwigulu ni kama anamtengenezea mwanae maadui - mtoto huyu hajafikisha miaka 18, umri ambao pengine angekuwa nao, asingeweza kukubaliana kuambatana vile na baba yake. Lakini privacy yake ipo wapi sasa? Siku baba akiangushwa kwenye uongozi na akapata mascandals makubwa makubwa ninaamini itakuwa ni pigo pia kwa huyo mtoto.

Iramba ilikuwa na Mbunge akiitwa Nalaila Kiula - alishika umaarufu sana na hata kidogo naye apate cheo kama cha doto Biteko kwa sasa lakini alipoporomoka kisiasa, watoto wake wapo salama kabisa, wanakula maisha kwa sababu ya kuficha identity.

Nani amwambie Dr. Mwigulu kuwa anamharibia mtoto wake. Kuna chipukizi gani wa umri ule anatembea kwenye ziara za vile? tena na baba yake! Kwaaahhhh!

Dkt Mwigulu kwa sababu wewe hupita na kusoma njumbe za Jukwaa hili hebu acha kumtangaza mtoto hivyo bhana! Jali haki ake za huko badaye kuliko kuanza kumtengenezea maadui mapema!

Kwa kfupi Tanzania hii uongozi wa kiimla haiupendi, hasa ule ambao mzazi anamtenegenezea mazingira hayo mtoto wake wazi wazi.

Mwishowe mtoto naye sasa anaweza kuanza kuwatisha wenzke wakitaka nafasi zake kuwa "Wasimfuate Mamba kwenye Kima Kirefu" manake atawamaliza.
Andaa mtoto wako kuwa kiongozi ,viongozi wanaandaliwa sio porojo Shetta aka baba Quila kamuandaa mtoto wake kuwa kiongozi baada ya miaka 20 utasikia majina yaleyale .Acha kulalamika andaa mtoto wako
 
Nafikiri tukiweka hoja za u ccm pembeni, ukwel ulio waz ninkwamba kama wazazi, tuna majukumu na wajibu wa kuwaandaa watoto mapema waje kuwa vile tunavyogaka wawe au kuwaongoza na kuwatia moyo wawe kama vile wanavyotaka wao kama endapo ndoto zao ni sahihi na unaona zitakua na manufaa
 
Dogo unafikiri George Bush alikuwa Rais wa Marekani kwa bahati mbaya? Unafikiri mdogo wake Jeb Bush alikuwa Gavana wa Miami kwa bahati mbaya? Chochote unachokiona leo kinaandaliwa tangu awali! Wewe endelea kuficha "identity" ya mwanao kwenye kuendesha bodaboda uone ataishia wapi! Ahahahahaha!
 
Sio vzuri kumnenea mabaya mtoto wa mwenzako, Nani kakwambia atakuwa bodaboda, ww unadhani Ccm itatawala milele? Siku ikianguka hao watoto wanaoandaliwa leo watakuwa viongozi wa taifa gani,
 
Back
Top Bottom