#COVID19 Je, Viongozi na Watendaji Serikalini wameyapuuza mapendekezo ya Kamati ya kutathmini Covid-19?

#COVID19 Je, Viongozi na Watendaji Serikalini wameyapuuza mapendekezo ya Kamati ya kutathmini Covid-19?

Ni wewe ndio umeleta hoja kwamba kwa sababu Mpango aliugua corona basi alimuambukiza Magufuli, yani unataka kutushawashi kwamba Mpango ndio mtu aliyekuwa karibu sana na Magufuli ndio maana akamuambukiza, japo ungetaja na wengine baadhi ambao nao tungesikia wanaumwa ambao walikuwa karibu na Mpango hapo kidogo ungetushawishi ila et katika watu wote waliyokaribu na Mpango ni Magufuli tu ndio kaambukizwa hapo itabidi ueleze kwanini Magu tu.

Nahisi hujui kusoma, nimekumbia na aliyekuwa katibu Mkuu Kiongozi bwana Kijazi. Ina maana hukuona popotee nilipomtaja ila umemuona Mpango tu kwenye maelezo yangu?
 
Nahisi hujui kusoma, nimekumbia na aliyekuwa katibu Mkuu Kiongozi bwana Kijazi. Ina maana hukuona popotee nilipomtaja ila umemuona Mpango tu kwenye maelezo yangu?
Sasa nani kamuambukiza nani au unataja tu watu? aliyemuambukiza Magufuli ni Kijazi au Mpango?
 
Sasa nani kamuambukiza nani au unataja tu watu? aliyemuambukiza Magufuli ni Kijazi au Mpango?

Nasema hivi, inaonekana una ubongo mdogo ndio maana unajadili kama mtoto mdogo. Unaweza kuambukiza usife ama ukafa. Kwahiyo kufa haijalishi nani kakuambukiza itategemea na kinga yako kupambana na ugonjwa husika.
 
Hoja yangu hata sio kufa ,issue kwanza inaanzia kwa kupata hayo maambukizi na hapo ndio tulipokuwa tunapajadili na ndio ukawa unawataja akina Kijazi na Mpango kwamba walikuwa karibu na Magufuli hivyo ndio wanaweza kuwa wamemuambukiza.
 
Ulifikiria masharti yangeendelea kuweko siku zote? Mbona walisema kabisa kuwa masharti yanawekwa ili hospital zisielemewe na pia waujue ugonjwa vizuri na namna ya kuweza kuutibu na mwisho chanjo ipatikane?
Hakuna mahali nimesema kuwa masharti yangeendelea kuwepo siku zote. Sidhani kama huu ni ugonjwa wa kwanza kutokea duniani.
 
Takriban wiki ya tatu tokea Kamati maalumu ya tathmini ya ugonjwa wa Corona (COVID-19) nchini kukamilisha kazi yake na kukabidhi ripoti kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Tume hiyo ilikuja na mapendekezo zaidi ya 19 ambapo mpaka sasa ukiondoa pendekezo ya kuagiza chanjo ya Corona ambalo serikali imeishalifanya, hakuna pendekezo lingine ambalo limeishafanyiwa kazi kikamilifu.

Hata pendekezo la kuvaa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka au vitakasa mikono halifuatwi achilia mbali kutoa takwimu za maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa wananchi na uhamasishaji wa chanjo kwa wananchi.

Ukichunguza hata uvaaji wa barakoa umebakia Ikulu peke yake na pindi viongozi wanapotoka Ikulu, wanazitupa barakoa kwenye geti za Ikulu! Hakuna cha social distancing hata Ikulu

Ukienda kwenye ofisi zingine za serikali, hakuna cha barakoa au maji ya kunawa/vitaka mikono.

Ukichunguza vizuri hata Rais Samia havai vizuri barakoa bali anafunika mdomo tu huku pua yake ikiwa nje ya barakoa! Ni kama anajilazimisha kuvaa barakoa ili aonekane amevaa lakini kiuhalisia hajavaa.

Mtu mwenye fikra pana atajiuliza, kulikuwa na sababu gani kwa serikali kutumia pesa kama posho kwa kamati ya watu zaidi ya 10 ambayo serikali hiyo hiyo inapuuza mapendekezo yake?

Kama hoja ilikuwa ni kuagiza chanjo ya Corona, haikuhitaji mpaka kuunda kamati ya watu zaidi ya 10 ambayo imekuja na vitabu vikubwa kama misahafu vinne vyenye mapendekezo ambayo ni pendekezo moja tu mpaka sasa ndilo limefanyiwa kazi. Ni kama ulikuwa ni usanii fulani ambao matokeo yake yalikuwa yanajulikana bali kilichokuwa kinatafutwa ni uhalalisho wa kuagiza chanjo ya corona na kukopa pesa za kukabiliana na ''janga la Corona''.

Kuagiza chanjo hakukuhitaji tume ya watu zaidi ya 10 bali kilichohitajika kwanza ni elimu ya corona kwa watanzania.

Ni ukweli kuwa mapendekezo ya Kamati ya Corona yamepokelewa kwa hisia hasi na watanzania wengi.

Kwa sasa tunakuwa na serikali ambayo inatoa ishara zisizoeleweka kwa wananchi kwa sababu viongozi hawana ujumbe/mwelekeo mmoja kwa wananchi kuhusu suala la Corona.

Serikali wanatakiwa watuambia kama Corona ipo na tujiandae kwa chanjo au watuambia corona haipo na chanjo iwe kwa wasafiri wa nje ya nchi.

Serikali kukaa kimya hakuwezi kuondoa ''tatizo'' ambalo kiuhalisia wameliasisi wao wenyewe baada ya kuunda Kamati ya Corona.
Kiuhalisia corona bongo cio serious kiviiile! Tunatishana tuu kwa kuwaogopa wazungu ! Tangu siku ile waliposema Chanjo ya Hiari nikajua HAMNA kitu apa
 
Haikutakiwa kufanya usanii kwa suala ambalo linajulikana.

Suala chanjo kuwepo nchini ni lazima kwa sababu huwezi kusafiri bila kuchanjwa.

Hoja ni kwa watanzania wengi kama watakubali kuchanjwa kwa hiari yao! Inavyoonekana wengi hawajakubali!
Kama mtu anajiona hana sababu ya kuchanjwa asiende kuchanjwa it is that simple mkuu. Swala la wengi wajakubali lisikuumize kichwa kwa sababu Wapo watu ambao wanaihitaji sana hiyo chanjo kutokana na sababu zao binafsi.

P.S. Binafsi siipingi chanjo, ila sina sababu yoyote ya msingi ya kuchanjwa hivyo sitaenda.
 
Hakuna mahali nimesema kuwa masharti yangeendelea kuwepo siku zote. Sidhani kama huu ni ugonjwa wa kwanza kutokea duniani.
Sasa concern yako au point yako hasa ilikuwa ni nini hasa ukizingitia unajua huu siyo ugonjwa wa kwanza kutokea duniani?
 
Haya ni mawazo pia yanafikirisha bila kututoa kwenye mstari. Rais alipokea taarifa ila utakelezaji umekuwa ukisuasua. Nafikiri ile ya India yaijafika vizuri ila ipo injiana.
 
Chanjo ni hiari ila haitakuwa hiari kwa watakaokuwa wakisafiri nje ya nchi hata Macca lazima uchanjwe period.
 
Sasa concern yako au point yako hasa ilikuwa ni nini hasa ukizingitia unajua huu siyo ugonjwa wa kwanza kutokea duniani?
Acha upuuzi. Kama hukunielewa ungepita kimya kuliko kuonyesha upunguani wako hapa.
 
Acha upuuzi. Kama hukunielewa ungepita kimya kuliko kuonyesha upunguani wako hapa.
Unaona umeshindwa hoja halafu unaleta viroja? Wewe ni zaidi ya mpumbavu. Sasa uliposema huu siyo ugonjwa wa kwanza kutokea duniani ulikuwa unadhani ni ujanja. Nilishakusoma na nikajua ujuha ndiyo unakusumbua. Nia yako ni kujenga hoja mfu kwa kutumia ujinga mliokaririshwa na mwendazake. Idiot!
 
Inaelekea TAKOSA linakuwasha.
 
Kwa unayoandika itoshe kusema una upunguani wa kiwango cha PhD.
Punguani wa PhD nadhani unamjua. Ni yule alikuwa anadai ana PhD lakini mawazo yake ni ya hovyo hovyo kama ya kwako.
 
Back
Top Bottom