Mwanakijiji said:JokaKuu.. tatizo la mambo ya Ukabila ni kuwa it is not rational. Mtu mwenye kuona ukabila anaitikia jambo hilo kwa hisia na vionjo na siyo kwa akili, kwani ukimuuliza onesha ukabila yeye atakuonesha namba. kama vile mtu mwenye udini akatavyoonesha namba. Wote wawili mkabila na mdini hawaangalii hoja za kiakili kwani wanaitikia kivionjo na hisia.
Ukiangalia humu utaona jinsi gani watu kwa mbali wanavumbi vumbi la ukabila dhidi ya Wachagga, si kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa wivu wa kwanini wao wamefanikiwa kuliko watu wengine.
Ni kwa sababu hiyo mimi naamini mtu wa hatari sana kwenye suala hili sasa hivi atasikika Bungeni siku moja akimwaga sumu yake ya ukabila.
Mwanakijiji,
..mimi sina tatizo na mtu atakayetuletea number na kutuhumu ukabila.
..lakini baada ya kuwa na number na kutambua ukabila what do we do next? hatujiulizi ni kitu gani kimewezesha kupatikana kwa hiyo number kubwa ya kabila fulani.
..watu wanalalamika uwepo wa, say wahasibu 20 wa kichaga TRA. wanamtuhumu CEO wa TRA kwa ukabila. hilo linafanyika bila kujiuliza hawa wahasibu 20 wamepatikana vipi. it takes at least 18 yrs to train an entry-level accountant.
..zaidi ni kwanini CEO wa Kichaga at any time anaweza ku-recruit wahasibu 20 wa kabila lake, lakini CEO wa Kimakonde hawezi kupata idadi hiyo ya wahasibu hata kama ana nia ya kuwa mkabila?
..kama tuhuma hizi za ukabila zingetolewa pamoja na mapendekezo ya mbinu za kupambana na ukabila huo mimi ningezielewa. tatizo mara nyingi zinatolewa, si kwa nia ya kuwasaidia wale walioachwa nyuma, bali kwa kuwafanya wale wanaonekana kuwa na "maendeleo" wabaya ndani ya jamii yao.
..halafu hii habari kwamba Wachaga wanajiona superior sijui imetoka wapi. au ni pale mmoja wa wachangiaji aliyesema kwamba Wachaga ni very hard working ndiyo imewakwaza wengine? hivi kuna watu hard working kama Wamachinga wanaotembea toka Kariakoo mpaka Masaki kuuza mashati? na kama kuna ushahidi wa waziwazi wa namna hiyo kwanini mtu akwazike na kusema Wachaga wanajiona superior?
..pia hili jina chasaka...nina hakika kila kabila Tanzania wana neno wanalotumia ku-refer watu wasiotoka eneo lao. kwanini mtu akwazike kuitwa chasaka akitembelea Uchagani, lakini hana tatizo na kuitwa foreigner akienda ughaibuni?
..mimi nafikiri badala ya kushindania viti 6 maalum kwa wabunge wanawake, labda tujielekeze ktk kuangalia ni jinsi gani tutaongeza idadi ya wasomi toka kila kabila/wilaya/mkoa Tanzania.
..tujielekeze katika kuhakikisha kwamba tunatoa elimu ya kiwango sawa ktk kila sehemu ya Tanzania. hilo siyo lengo linalotekelezeka kwa awamu moja ya uongozi, it may take a generation.
NB:
..vilevile huu uchumi wetu nao haukui na ajira haziongezeki. kila Mtanzania amepatolea macho TRA, Tanroads, na taasisi nyingine chache. kwa mfano: nilisoma mahali kwamba kuna vijana wa Kitanzania zaidi ya 100 wana PhD degrees. vijana hao wanalilia wazee waondoke pale UDSM ili wao vijana wapewe nafasi.
..kauli hiyo imenishangaza ukizingatia kwamba inatoka kwa wasomi wetu. kwanini tuwe na kilio kama hicho wakati ndiyo kwanza tumeanzisha Chuo kikuu Dodoma?