Acheni hoja za kikabila zinaingiza chuki kubwa katika jamii na ni tool ya pili katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ya kwanza ni Udini. Lakini ngoja niguse kidogo, hebu tujaribu kutafiti ni namna gani mtu anapata kazi. Kwanza tangazo la kazi linatolewa katika gazeti, mbao za matangazo nk kama hao jamaa wakiamua lifike huko otherwise some body known by someone ktk utawala atapewa kazi hata kama shule hajamaliza bado na kazi haiwezi acheni kushangaa hii ndio hali halisi. Then watu wataaply na wachache sana watakuwashortlisted wengiwao ni walewale kamlete na labda kina kapeto wachache wakuzugia si unajua ukitaka kumuua nyani mfiche uso. Haya wakianza kazi most of them are not compitent na kazi yao kulalamikia mishahara na safari za nje bila kujipima wanaingiza kiasi gani. Kujuana kunatuangamiza wabongo naona sasa jf tujitahidi kushauliana ili tupate njia ya kuondoa kujuana hasa katika ajira.