Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #421
Mzee,
Daraja lile lilianza kujengwa wakati wa Mwinyi na nadhani ndiye alienda kuomba fedha kwa wafadhili wa Kiarabu na wengine. Magufuli alifanya "kujipendekeza" kwa Mkapa kwa kulipa daraja lile JINA la Mkapa.
mizizi said:.. Juzi mramba alipokuwa anatoa mchango wake bungeni, alizema ili tanzania tuweze kuendelea tunatakiwa tuwe na miundombinu ya barabara ambayo itaunganisha vijiji, kata, wilaya, mikoa na mwisho nchi nzima. hutu akitolea mfano kwa madoido kwamba, jimboni kwake wamefanikiwa hilo, kwani wanabarabara nzuri. zaidi ya hapo alionyesha hata sehemu ya kupata fedha kujengea barabara hizo. huku akisahau kwamba, alipokuwa akijenga barabara za kwake, huku akiwa waziri katika nchi hii, akiacha sehemu nyingine. je huu sio ubaguzi ambao anaouzungumzia mwanakjj? hatuwezi kuzungumzi hili, kwani bila usawa hakuna haki.
nilikuwa na imani kubwa sana kwako mkuu M.M.M
sasa naanza kuipoteza.Tukumbuke kuna baadhi ya wanaforum na wale guest wanatutegemea sana kwa maoni na ushauri wetu kwa matatizo tunayopambana nayo kama taifa.And when you come will such post mzee....! naishiwa maneno ya kusema zaidi ya kusisitiza kuwa KILA MMOJA WETU AELEWE NAFASI YAKE KATIKA KULIJENGA NA KULIBOMOA TAIFA HILI.Kama huna cha kupost mzee......... siku nyingine uwe msomaji tu.
Kuna baadhi ya wachaga wanaogopa kutumia majina yao ya ukoo kwa kuhofia kutopata kazi kwenye ofisi anayoomba kazi. kwani kwenye hiyo ofisi wachaga wamejaa na wanaogopa kuajiri wachaga wengine. Kama mtu anaitwa Diana Boniface Mushi, anaandika Diana Boniface. usishnagae ukiona mchaga anaukana uchaga kwenye interview.
Ni hayo tu mtu wangu.
Kungurumweupe,
..nilifanya makosa ktk posting yangu ya kwanza na nimekuja hapa na kuyarekebisha na nimeridhika kwamba nilichofanya ni uungwana.
..kama hukuridhika na umepoteza imani na yale ninayoandika hilo haliko ndani ya uwezo wake. pamoja na hayo unaweza kusoma makala niliyokuwa niki-refer kwa kubofya hapa kwenye : Historia ya Mangi Marealle
..umeleta maneno ya mitaani kuhusu relation kati ya wachaga/ujambazi/maisha na mali za wananchi zilizopotea. pia umeeleza kwamba huamini kama madai hayo ni ya kweli. hata mimi naona ni madai ya kipuuzi, kama ulivyoyaona wewe, kwa hiyo nitayaacha kama yalivyo.
Mizizi,WildCard,
..mradi wa barabara ktk jimbo la Mramba ulianza wakati wa waziri John Magufuli. Basil Mramba aliukuta mradi huo ukiwa ktk hatua ya ujenzi.
..miradi hii ya barabara hupitia hatua za upembuzi yakinifu, design, na kuitishwa tenda, na mwisho ndiyo ujenzi huanza. katika kila hatua huwa kuna fedha zinatengwa.
..hatua ya mwisho ya ujenzi ndiyo hutumia fedha nyingi kuliko hizo za awali. katika miradi yenye wafadhili, mara nyingine huwa kunakuwa na makubaliano ya serikali kuchangia kiwango fulani. serikali ikikiuka makubaliano hayo mradi unaweza kusimama.
..Mbunge Selelli alipiga kelele kwamba mradi wa barabara jimboni kwake ulipewa fedha chache na fedha zote zikapelekwa jimboni kwa Mramba. Mbunge Selelli alifanya kosa la "kiufundi." Mbunge hakueleza kwamba mradi wake ulikuwa ktk hatua ya upembuzi yakinifu, au design, na ndiyo maana ukatengewa fedha ambazo zilionekana ni kidogo.
..hata katika mazungumzo yale utaona kwamba ili kumpoza Mramba alimhakikishia kwamba atahangaika kumtafutia WAFADHILI watakaosaidia kutoa fedha za UJENZI.
..lakini pamoja na hayo Basil Mramba amekuwa waziri wa Ujenzi na miundo mbinu kwa kipindi cha kisichozidi miaka 3. pia sina kumbukumbu za karibuni za waziri wa ujenzi/miundo mbinu anayetokea Uchagani. sasa kwanini hizi lawama zinaelekezwa kwa Wachaga?
..kuna barabara ya Dodoma-Singida-Mwanza ambayo fedha zake zilifujwa na Nalaila Kiula na George Mlingwa. nashangaa hawa hawalaumiwi anakuja kulaumiwa Mramba.
..serikali ya Japan ilitoa msaada wa vifaa kujenga barabara ya kusini. iliamuliwa jeshi ndiyo wangefanya kazi hiyo baada ya kujenga kipande cha barabara ya makambako. Kawawa[mtu wa kusini] kama waziri wa ulinzi did not take action na vifaa vikaharibika. leo hii tunamjengea Kawawa makumbusho kwa utumishi wake uliotukuka. wakati huohuo -tunamlaumu Mramba na Wachaga kwamba ndiyo waliodhulumu mpaka mikoa ya kusini ikakosa barabara.
mizizi.. ili tulinganishe hebu tuoneshe rekodi za Mawaziri wengine walifanya nini kuhusu maeneo ya kwao? Mkapa si amejenga daraja kwenda kwao ambalo linaitwa na jina lake na hadi leo hawajajenga daraja la kuvuka Kigamboni, au kujenga daraja la kisasa kupita Kamanga, pale Mwanza? Je huo ni ubaguzi wa Wamakonde wote? (kama unaweza kuita ubaguzi).
Je Mawaziri wengine wamefanya nini in relation to their areas, ukisema Mkapa tu angalau tuwekee data za kulinganisha. Halafu, iweje vitendo vya waziri mmoja alivyofanya (aidha kwa upendeleo au vinginevyo) vibebeshwe Kabila zima au jumuiya nzima ya watu?
Kikwete hivi sasa ni Rais je kuna miradi yoyote inayofanyika Pwani ambayo ingeweza kufanyika mahali pengine na tunaweza kuiita upendeleo? Kuna Uwanja wa Kimataifa unatarajiwa kujengwa huko, kwanini usijengwe Morogoro au Tanga, au Lindi au Dar yenyewe? Hivi sasa Kuna uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mbeya ambao nadhani umefikia mwisho, je mradi ulianza lini na aliyekuwa waziri wa Ujenzi Mwandosya alihusika vipi? Je kila kiongozi ambaye anapeleka mradi kwenye maeneo ya kwao anafanya hivyo? au kila kiongozi anayetoka eneo fulani asiwajibike kuleta maendeleo jimboni mwake kwa hofu ya kuitwa mkabila?
Kungurumweupe,
..lakini hayo maneno ya mtaani uliyoyaleta kuhusu ujambazi/maisha yaliyopotea/mali zilizopotea/na chuki dhidi ya uchaga, ni maneno ambayo umesema huyaamini. sasa labda ungetueleza kwanini huyaamini.
..zaidi nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri na msisitizo kuhusu umuhimu wa habari za mitaani.
Kungurumweupe said:Nilichokisema mimi ni kwamba siyaamini na wala sikusema kwamba ni maneno ya kipuuzi! Siwezi kusema kwamba ni ya kipuuzi kwani sijafanya research yoyote.
Kama jamii ni lazima tupinge kwa nguvu zetu zote wale wanaoeneza sumu ya ukabila, udini, urangi kwa ajili ya kupata manufaa ya kisiasa au ya kinamna yoyote ile. Wakati huo huo tusije kufanya mambo yetu bila kuangalia jinsi gani mambo hayo yanaweza kutafsirika vibaya.
Ndio maana kwa upande wangu linapokuja suala la Chadema kwa mfano, tatizo ninaloliona lilitokea katika suala la wagombea wa viti maalumu ni suala la utaratibu na mchakato wa jinsi gani hao wanapatikana. Jambo hilo nasikia hata wao wanafahamu ndio maana baada ya mabadiliko ya Katiba yao ya 2006 waliamua kubadili jinsi wanavyofanya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.
Hili pia linatokea katika nafasi mbalimbali za uongozi au utumishi ambapo ninachokiona kama tatizo kubwa si ukabila bali undugunization uliokithiri kutokana na utaratibu mbaya wa kupata ajira na madaraka nchini. Ni kwa sababu hiyo utaona mngoni aliyepata nafasi atahakikisha watoto wake na wenyewe wanaingia kwenye eneo hilo, au akawapa habari za ndani zenye faida watu wa "kwao" na wakapata unfair advantage ya mambo fulani. Hili linatokea kwa karibu makabila yote.
Tusikubali kuongozwa na hisia kinyume (negative emotions) kwa sababu hatuoni tunachotaka kuona. Tusilazimishwe kuona kitu ambacho hakipo kama alivyofanya Wangwe hivi karibuni.
Lakini ukweli utaendelea kubakia Watanzania siyo binadamu tofauti na wengine kiasi kwamba hawana mawazo ya kibaguzi ati tu kwa vile ni wa Tanzania. Mawazo haya yapo, yanachochewa na wakati mwingine yanatukuzwa. Ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha siyo tu anapinga mawazo ya kuchochea ukabila, lakini pia kupinga dalili zozote za ukabila zinapojitokeza hata kama zinahusu kabila lake au watu wa jamii yake.
Ni tutakapofanya hivyo ndipo tutakuwa kweli tunajenga Taifa la watu "walio huru, sawa, na wenye kufurahia haki zote za msingi sawasawa katika Taifa lao".
Kubwajinga,
..ujenzi wa barabara ya kusini umeanza wakati wa Raisi Mwinyi, na Waziri Kiula.
..off course kilio cha barabara ya kusini ni cha muda mrefu na ndiyo maana ujenzi wake ukaanza kabla ya ujenzi wa barabara za Tarakea,Marangu,Rombo.
..ninavyoelewa mimi barabara ya kusini siyo ndefu kama hizi nyingine isipokuwa ujenzi wake ni mgumu na wa gharama kubwa kutokana na nature of the terrain it is passing thr'.
..ugumu wa ujenzi wa barabara ya kusini na ukubwa wa gharama ndiyo umesababisha wafadhili wengi wasite kutusaidia. serikali ilibidi ifanye kazi ya ziada mpaka kuwapata Saudi na Kuwait Fund, lakini hawa "wafadhili tuliowazoea" walikuwa wagumu kuwashawishi kutoa msaada.
Kubwajinga,
..hatua zote mpaka kufikia kuanza ujenzi zilifanyika kabla Mramba hajafika miundombinu.
..kuna hatua nyingi zinaweza kuendelea bila kusubiri bajeti kupitishwa.
..sasa ina maana Mramba alikuwa na influence kwa Magufuli na Makongoro Mahanga?
..pia naomba ufahamu kwamba contractor huwa anatumia fedha zake kabla hajaanza kulipwa na serikali. kwa hivyo hoja yako ya contractor kuwa site na kuanza kazi inabidi uirekebishe.
..mara nyingine pia hufikia contractor akakopwa na serikali ikiwa haina fedha.
..barabara ya kusini ina historia ndefu sana tangu wakati wa Mbunge Maalim Nabahan.
..tena ukitaka niko tayari kukufahamisha ni juhudi zipi zilifanyika na serikali. kuzorota kwa mradi huo hakutokani na kina Basili Mramba.
..kuna barabara[chalinze-segera,songea-makambako, dsm municipal,mwanza municipal...] nyingi tu zimejengwa kabla ya barabara za kusini. kwanini unahoji barabara ya Tarakea,Rombo, peke yake?
..labda nikuulize swali hili: hizi sentiments dhidi ya Wachaga ziko deep rooted, hata serikalini kuna watu wenye usongo kama wewe. je, ni kitu gani kinachowazuia kuwashughulikia kwa namna ambayo umependekeza hapa?