Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
Mkuu,

JOB ADVERTISEMENT ON YOUR Tz-NEWSPAPER IS JUST A FORMALITY! KAMA HULIJUI HILO POLE SANA!

For more factual information, please, give me time. I am doing my Reseach!

Umenipa pole..sina budi kuipokea ila nimeshangaa kidogo maana mpaka nimesema nilichosema..sio kuwa im talking from the abstract..
Ila I wish you luck kwenye utafiti wako..ukikwama uombe tukupe msaada...

Mawazo ya kuwa job adverts ni formalities hata mie kuna kipindi nilikuwa na mawazo kama hayo.Hii ilinikosesha opportunities nyingi.Nilipoamua kuwa objective na kuanza ku compete na wengine...the story changed na ndio maana nashangaa mnavyowabeza wachagga! Jamani ingieni kwenye ushindani na muache majungu... mtaona kwamba hizi kufikirika na kusadikika hazipo tena..at least kwenye ulimwenguni wa ushindani wa kimataifa![/QUOTE]



Mkuu,

Safiri salama... until then!
 
Mkuu,

JOB ADVERTISEMENT ON YOUR Tz-NEWSPAPER IS JUST A FORMALITY! KAMA HULIJUI HILO POLE SANA!

For more factual information, please, give me time. I am doing my Reseach!

Umenipa pole..sina budi kuipokea ila nimeshangaa kidogo maana mpaka nimesema nilichosema..sio kuwa im talking from the abstract..
Ila I wish you luck kwenye utafiti wako..ukikwama uombe tukupe msaada...

Mawazo ya kuwa job adverts ni formalities hata mie kuna kipindi nilikuwa na mawazo kama hayo.Hii ilinikosesha opportunities nyingi.Nilipoamua kuwa objective na kuanza ku compete na wengine...the story changed na ndio maana nashangaa mnavyowabeza wachagga! Jamani ingieni kwenye ushindani na muache majungu... mtaona kwamba hizi kufikirika na kusadikika hazipo tena..at least kwenye ulimwenguni wa ushindani wa kimataifa![/QUOTE]

Ni vema tukaangalia zaidi hali ilivyo ndani ya CHADEMA. Haya ya mitaani ni vigumu kuyatatulia humu ukumbini.
 
quite interesting facts coming out,
so there is pent up anger!! (in some few)
Any plans to overcome it?
 
quite interesting facts coming out,
so there is pent up anger!! (in some few)
Any plans to overcome it?


Haika,
Lets wait for the research that Mkuu has promised..... ila I now see the CHADEMA connection.....so it was all about this?VERY BORING
 
KJ.. tusaidie wewe utuoneshe ukabila wa wachagga, siyo idadi ya wachagga ndani ya Chadema.
 
Haika,
Lets wait for the research that Mkuu has promised..... ila I now see the CHADEMA connection.....so it was all about this?VERY BORING

It seems like there is a call for all CHADEMA people to stay away from the discussions concerning their party. They just vanished all of them and at the same time. What a conincedence.
 
Nyie zungukeni tuu lakini ukweli unabaki pale pale WACHAGGA kiboko akina shimboni mmh! nimewavulia kofia hawa wanajamii si cha mwanaume si mwanamke wote full maarifa.Wanamaarifa sana ya kubebana pindi mtu anakula kitengo.
Angalieni huyo Mrema wa miundo mbinu mkifatilia mizani yote ya TANROAD hawakosi wachagga pale lazima wapo wamekula vitengo.
Wachagga wanapenda sana sector za mipesa sana we zungukia tu utapata jibu.
Kila sector nzuri inawenyewe.
 
Kubwajinga,

..nadhani kinachokusumbua ni mentality kwamba Wachaga wakikosa basi haki imetendeka. hiyo mentality wanayo watu wengi tu.

..serikali inawajibika kwa kila Mtanzania. kwa msingi huo hiki kidogo tulichonacho kitagawanya kwa kila sehemu ili kila eneo lijisikie ni sehemu ya Tanzania.

..kuna maeneo ya Tanzania yako nyuma kimaendeleo kwa hiyo yanahitaji maji,umeme,barabara etc. kwa mfano sasa hivi mkoa wa Kigoma umepewa kipaumbele ktk mpango wa rural electrification. zaidi ya hilo kuna barabara zinajengwa huko na hata Zitto ametoa shukurani bungeni.

..Kilimanjaro kutokana na hatua waliyofikia tatizo lao kubwa ni barabara. serikali haipeleki umeme huko, au maji kwasababu tayari yapo.

..wakati wowote ule unaweza ku-argue kwamba kuna eneo linastahili mradi fulani kuliko eneo lingine. kwa hali ilivyo Tanzania sasa hivi huwezi kukosa mradi wa kukosoa. tatizo ni kwamba watu wemeelekeza macho na masikio yao Kilimanjaro tu.

..picha unayojaribu kujenga hapa ni kana kwamba serikali imesimamisha ujenzi wa barabara zote nchini na kuamua kujenga barabara moja tu ya Tarakea,Rombo. kuna barabara nyingine nyingi tu zinajengwa na zimepewa kasma kubwa.

..narudia tena huu mradi ulianza kujengwa wakati wa John Magufuli. upembuzi yakinifu na design zilifanyika tangu mwaka 1998 tena wakati huo Mramba alikuwa ameshindwa ubunge.

Mwanakijiji,

..kuna watu wanafaidika na hizi chuki dhidi ya Wachaga.

..kuna viongozi walioshindwa kazi na badala ya kubeba lawama wameamua kuwatupia Wachaga na wananchi wa Kilimanjaro.

..hebu chukulia huo mfano wa Msuya "kuiba maendeleo" na kupeleka Mwanga. ungelijua ukubwa wa jimbo la mwanga ungecheka kweli. hivi Msuya ataiba fedha kiasi gani? atahamisha barabara kilometa ngapi? atajenga shule ngapi?

..jimbo la mwanga halifiki watu laki 3. sasa watu milioni 40 wanaaminishwa kwamba kuwepo kwao nyuma kimaendeleo kumesababishwa na mtu mmoja Cleopa Msuya, au Basil Mramba, au waziri yeyote toka Kilimanjaro, na wameamini.

..ni hali hiyo hiyo uliwafanya Watanzania waamini ule mpango wa elimu wa quota-system. mpango ule uliamua kuweka pass-mark ya juu Kilimanjaro ili kuzuia mkoa huo kutoa wanafunzi wengi kuingia sekondari za serikali.

..Wananchi waliufurahia sana, waliaminishwa kwamba Wachaga wakikosa basi haki imetendeka. lakini mwanasiasa anapokwambia anakupa pass-mark ya chini maana yake hata elimu anayokupa ni ya kiwango cha chini. sasa hakuna aliyehoji kuhusu masuala ya kiwango cha elimu.

..to cut the story short, karibu miaka 20 tangu quota-system ianzishwe Dean wa Faculty of Engineering Prof.Masuha alishangaa kwamba kuna maeneo ya Tanzania hayapeleki wanafunzi ktk kitivo chake. lakini muda wote huo wananchi walikuwa wameridhika kutokana na mentality kwamba Kilimanjaro wakikosa haki imetendeka.

NB:

..Wachaga ni kabila dogo sana kiasi kwamba hata wakinyimwa kila kitu bado hali ya maisha ya Watanzania haitobadilika significantly.

..halafu wakati Wachaga wanatuhumiwa kupendelewa na serikali na chama tawala, bado wapo mstari wa mbele katika kuunga mkono vyama vya upinzani.
 
Nafikiri tumeanza kuishiwa hoja, au labda ni commercial break
 
Joka Kuu.. watu wakishaelewa hili na kujichunguza wao wenyewe ndio watatambua kuwa tatizo la Tanzania siyo wachagga.
 
For that case , therefore, wachaga wengi wanaoshikilia nafasi kubwa kubwa ama za kiutawala ua za kiuongozi katika asasi na taasisi mbalimbali za kijamii na serikali ya tz, huwa wakwanza kupata au kusikia fununu au habari za ukweli na za ndani kuhusu kazi ndani ya hizo NGOs za kimataifa, kisha "hujitahidi" ama kwa makusudi au kwa kulazimika, kuzifikisha kwa wale wanaotaka kuwapendelea. Ikibidi, hutumia influence yao kuhakikisha kuwa hizo nafasi zinakaliwa na watu wao. Hawa watu(viongozi wa ...) hufanya connection hizi na marafiki zao ama weusi au weupe walioko ndani na nje ya tz na hasa wale ambao tayari wamo kwenye mtandao huo wa kiupendeleo wa kimataifa.

Wale bongolala msiolijua hili, AMKENI kumekucha![/QUOTE]

(I am responding to the above paragraph)
I can see this rediculous discussion is going over and over,I can't believe what am reading yaani mmefikia hatua ya kusema kuwa kweli wachagga wanapendelewa hata kwenye hizo International Organizations!!
Hebu acheni uongo, hivi hamjui kwamba uongo ni dhambi? (Ila sishangai kuna mtu ambaye si mtz ila aliishi Tz kwa miaka 6, alisema kuwa watz kwa uongo ndio wenyewe, i kinda believe her now). Ok, ina maana hizo NGO huwa kila zikitafuta mfanyakazi it happen kwamba zinawaconsult mabosi ambao ni wachagga ili wawafanyie connection ya wachaga wenzao? Lets be serious here, we don't have to argue for the sake of arguing we have to be honesty,,kweli mwenye akili timamu alifikirie hili, I don't buy this at all, piga ua!
Ila kama hili ni kweli basi wana hizo qualifications zinazotakiwa ama la, hizo kazi za UN, NGO sio za kupeana kama uko ziro upstairs!Nachojua mimi utendaji wako wa kazi is the best quality na sio vinginevyo.
Je hebu niambie inakuwaje wachagga wanapata ajira mahali ambako wanachohitaji ni CV yako na wala hawaitaji kumconsult mtu yeyote aliyeko TZ, wala hawajui kwamba wewe ni mtz let alone mchagga? mahali ambapo wala hawajui kama kabila hili linaexist? FYI ninafanya kazi mahali ambapo kuna wachagga 4 na wala ajira zao hazina connection yoyote na TZ na wala hatukuwa tunajuana kabla ya kukutana kazini. Je una jibu la hili au utasema tena wanapendelewa na watu hata wasiojua TZ iko wapi kwenye ramani ya Dunia? ndio kwanza ukiwatajia Tanzania wanachosikia ni Tasmania Australia.
I think I have to stay away from this discussion is getting on my skin now, is unbearable. All in all tupunguze uongo, wivu na majungu havitatupeleka popote,kama wengine walivyokwisha pendekeza ukitaka kujua siri ya mwenzako uliza, sio ukae chini unamake all wrong assumptions, it wont help anything! At the end of the day the holy bible says " Mwenye nacho ataongezewa"
You all have a relaxing weekend.
 

JokaK,
Tatizo lako wewe unaangalia mambo yote kwenye misingi ya sisi against wao. Hiyo haifai kama unaongelea ufisadi na national interests. Ufisadi ukifanywa hata na ndugu yako ni lazima uupige vita.

Kilimanjaro kila makao makuu ya wilaya zake yanafikika kwa barabara nzuri sana zote zikiwa za lami kasoro ile ya Rombo tu wakati huku kwingine tunaongelea makao makuu ya mikoa tena yenye umuhimu sana kiuchumi, Kigoma, Rukwa, Kagera, Shinyanga, Lindi, Mtwara n.k. yote haifikiki kirahisi.

Lakini leo hii waziri anatumia hizo hizo resources kidogo zilizopo kujenga barabara kwenda kijijini kwake ambayo tayari ilikuwa nzuri sana kwa level ya gravel, na kuongezea hata kipande kinachoenda porini Kenya ambako hakuna anayepatumia zaidi ya walanguzi wa dawa za miswaki, kweli hii ni akili sawia au ubinafsi sasa umetufika makooni??


Hiyo ya kusema tunataka onyesha kuwa waziri aliifanyia kazi Rombo peke yake ni wewe unayeisema. Ya kwangu mimi ni kuwa kuna baadhi ya Mawaziri, Mramba akiwa ni mmojawapo, wamekuwa wabinafsi sana kiasi kuwa jinsi wanavyopanga miradi ya maendeleo kiupendeleo inazorotesha maendeleo ya nchi.

Kama hii pesa ya kujengea barabara ya Tarakea ingepelekwa barabara ya Kigoma au Mtwara n.k., tungekuwa tumejenga 100km na kuanza kutumia resources za hiyo mikoa kama Bandari ya Mtwara na ya Kigoma. Niambie sasa hivi tumepata nini toka Rombo baada ya kujenga ile barabara ambacho tulikuwa hatupati zaidi ya mikogo ya Mramba bungeni?? Hiyo ndio kero yangu. Kama kuna watakaoona alichofanya Mramba ni ukabila hilo sio juu yangu, my point is clear.


Nafikiri picha zinaelezea vizuri hali halisi kuliko maneno. Angalia hizo hapo chini ujiburudishe.











Hii ndiyo hali ya barabara kuu ya kuunganisha mikoa ya Kigoma na Shinyanga. Watumishi wa serikali wakihamishiwa huku wanaenda kwa viboko.
 

Joka,
Tatizo lako ni kuwa unaangalia sana mambo yote katika misingi ya kuwa lolote linalofanyinka katika kutawanya resources za nchi kwa kila mwananchi, lina nia ya kuwanyima waChagga kwa vile hapo awali walikuwa beneficiary wakuu. Huu ni ujinga wa hali ya juu kwani hata hivi sasa bado kuna resources nyingi kupita kiasi zilizoelekezwa Mkoani Kilimanjaro kupita Mikoa mingine mingi.

Kwa hiyo kama ulitaka Msukuma ambaye kwao hakuna aliyewahi kwenda shule au kuona shule ashindane na mmachame wa pale maili 20, ambaye kijiji kizima kinajua tayari umuhimu wa shule for the past 50+ yrs, then hufikirii kwa misingi ya kujenga nchi bali kwa misingi ya mimi kwanza wengine watajijua wenyewe. Kiongozi wa nchi anatakiwa kumpa kila mtu nafasi ya kushiriki katika kujenga nchi na kujijenga, hata kama itakuwa at the expence ya mwingine aliyenacho. Ila watu wa mentality ya aina yako ya kujipendelea sidhani kama wanafaa kuongoza nchi.
 
Joka Kuu.. watu wakishaelewa hili na kujichunguza wao wenyewe ndio watatambua kuwa tatizo la Tanzania siyo wachagga.

Tokea lini wachaga wakawa ni tatizo la Tanzania? Kwani wao sio wananchi? Hapa zinazopingwa ni tabia za baadhi kwa nia ya kuwakerebisha.
 
Mwaka 2006/2007 akiwa ni Waziri wa Miundo Mbinu Bw. Basil Mramba aliwakilisha Bungeni makadirio ya Wizara yake. Alielezea wamefikia wapi na mipango ya mbeleni iko vipi. Akasema hivi:


Akafafanua suala hili kwa kusema jinsi gani wamepanga kulitekeleza:


Akafafanua kidogo kuhusu hizo kanda:


Na kwa upande wa Ukanda wa Tanga akasema hivi:


na akafafanua kuhusu Ukanda wa Mtwara kwa kusema hivi:


Sasa utaweza kuona kuwa kwanza kabisa ni kuwa ujenzi wa barabara ya Tarakea haukuwa siri. Ulitajwa Bungeni na Wabunge ambao wana jukumu la kupitisha fedha hizo walipewa nafasi ya kuamua kufinance au la. Waliamua kufinance licha ya majadiliano makala kama yalivyoripotiwa na gazeti la Tanzania Daima:


Mapema mwaka huu, ukaguzi wa maendeleo ya bara bara hiyo uliripotiwa hivi na gazeti la Daily News:


Sasa katika yote ni wazi kuwa suala la ujenzi wa barabara ya Tarakea limetolewa na baraka na kuanzia serikali ya Mkapa, na ya Kikwete na limefanywa hadharani pasipo kificho likihusisha mjadala wa Bunge. Ni wazi pia kuwa wabunge wa CCM na wabunge wa mikoa ambayo ina matatizo ya barabara waliridhia shs bilioni 17 kutumika katika ujenzi wa barabara hiyo. Kama hayo yote ni kweli (ushahidi uliopo unasema ndiyo), basi Mramba siyo mwenye kosa na kitendo cha kusema amejipendelea hakina msingi. WALIOMPENDELEA (kama tunaweza kuita kupendelea) NI WALE WALIOIDHINISHA FEDHA ZA MRADI HUO NA KUZIPITISHA ZITUMIKE. Ujanja kila wakati siyo kuwahi, ni kupata.
 


Mkuu MMJJ,
Nilikuonya kuwa kwa kuinvest kwako kwingi kwa Mbowe/CHADEMA hatimaye utakuwa zombie, na inasikitisha kuona kuwa unaelekea huko.

Sasa angalia unafanya analysis na reporting kama za Rweyemamu na JK. Haya ni maigizo.

Ina maana kwenye hizo quotes zote ulizotafuta na kubandika hukuona kuwa zote zinashindwa kuhalalisha ujenzi wa hiyo barabara ukilinganisha na mahitaji mengine?? Sikiliza hata mwandishi wa habari Deo Mushi alivyoandika;




Ukisoma hapo juu unaona Mushi anajaribu kukuelezea nini? Endelea hapo chini ili ujue wazi kuwa huu mradi ulilazimishiwa tu wabunge?


Hivi akina Zitto na Dr.Slaa walikuwa wapi haya yakifanyika hasa Zitto ambaye anatokea huko huko kusiko na barabara?

<-----> “Mheshimiwa Spika, natarajia kwenda ng’ambo kutafuta wafadhili kwa ajili ya kupata fedha za kutengenezea barabara alizozizungumzia Mheshimiwa Selelii,” alisema (Mramba).

Baada ya mjadala ikafuata danganya toto. Wabunge wamefanywa kama watoto wadogo. Huko nje ya nchi pesa zinaokotwa?? Kwa nini wasingetafutia basi pesa zile barabara muhimu kwanza kama huo ndio utaratibu???

Kama utachunguza hata sababu ya ujenzi wa hiyo barabara inakosekana na badala yake wanaweka sababu kuu ikiwa kuunganisha na Kenya. Inabidi kila wakati isisitizwe maana ki-ukweli ni kuwa hapakuwa na sababu yoyote zaidi ya upendeleo wa wazi.



Hizi ndio sababu za kumpelekea Mramba a super highway. Hivi hiyo population inazidi zile za mikoa ya Shinyanga na Kigoma?? Mpaka upi unahitaji barabara kwa haraka, ile ya kupeleka containers Congo, Burundi, Rwanda n.k., au kile kituo cha kuingizia sabuni na dawa za miswaki kimagendo kutokea Kenya??

Hivi ni kweli haya MMJJ huyaoni au umefall kiasi cha kuona chongo = kengeza?? Wake up, kumtetea Mramba haina maana kuitetea CHADEMA, hapa unatetea kitu kingine kabisaa.
 
KJ.. simtetei Mramba kama unavyoona wewe; kwa sababu inaonekana unaniangalia kwa misingi ya kumtetea mtu. Ninachotetea ni principle.

a. Je uamuzi wa kujenga barabara ya Tarakea ulifanywa na nani?
b. Je pesa zilipitishwa na nani?
c. Je ujenzi huo ulikoma baada ya Mramba kuondoka?
d. Je serikali kuu ilikuwa inafahamu mpango wa kujenga barabara hiyo ya Tarakea?
e. Je Mramba kwa kutekeleza mradi ulioamuliwa katika Ilani ya CCM anakuwa anajipendelea?
f. Je fedha zilizotengwa zilichukuliwa toka mradi mwingine, kazi nyingine au ndizo zilizopangwa katika bajeti na kupitishwa na Bunge?

Ninachojaribu kukuonesha ni kuwa watu wenye kubeba jukumu la maamuzi ya ujenzi wa barabara ya Tarakea ni CCM na wabunge wake ambaye Mramba ni mmojawapo. The bucks stops with CCM na naona unaona kazi sana kunyosha kidole hicho kwacho japo nimejaribu kukuelekeza toka kwa mbali. Ndugu yangu ni CCM waliiweka kwenye Ilani, ni CCM waliipigia kura, ni CCM wameisimamia na ni CCM yenye wajibu huo wote. Kumpa uzito huo mtu mmoja ni kukwepa ukweli. Kama CCM isingetaka lisengekuwepo. Period. Lakini mwenzangu naona hutaki kuiangalia CCM wala kuinyoshea kidole kwenye hili. I won't speculate why.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…