Hivi niulize swali moja hapa!..Natazama pande mbili za hii shilingi pamoja na kwamba haina soko kabisa..
Hivi wazungu walipokuwa wakishika wao madaraka kuendesha nchi ktk nafasi zote muhimu kulikuwepo na sababu gani ya kuwaondoa?..
je, tulipofanya hivyo ilikuwa chuki au?... maanake sioni tofauti kati ya Ukabila na Ubaguzi wa rangi ktk matukio ama uendeshaji wake. Najribu kutenganisha mifano hii miwili lakini nimekwama kwa sababu siwezi kutumia neno wageni kwa Wazungu nikaliacha kwa Wachagga..
Je, kuna jibu lolote ambalo tunaweza kulitumia na likawa halali kwa Wachagga lakini sio kwa Wazungu, waarabu na kadhalika..na kama hakuna je inakuwaje tunahalalisha kumwondoa mzungu madarakani, mzungu ambaye alikuwa na elimu na kila sifa kuliko hata huyo mchagga lakini tunalikataa inapofika kwa mchagga!..kuna tofauti zipi zinajenga ubaguzi wa kabila la ule wa rangi.
Ni swali tu sina jibu, nimeumizwa kichwa changu kwa muda kisha nimeona bora nililete kwa wataalam..