Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
unaniambia mmie nijibu hoja bila matusi au someone else? rudia post yako hapo juu.

Mama,
Nadhani atakua amechanganya tu.

Duh,halafu mama na hujalala nini? Maanake nimeamka bado upo tu,kaazi kweli kweli.

Jana kumbe uliniuliza kama nina msimamo na kuaga kwangu kwamba naenda kulala,yap! Msimamo nilikua nao. Ndio nimeamka na nikakuta post yako
 
teh teh teh tehhhhhheeeeeeeeeeeeeeee, nina element za uchaga na ninajua yanayosemwa ni kweli. Ukienda likizo chrismas kule Moshi utajua haya pia. Ni connection ka kwenda mbele, chagas wapenda maendeleo lakini tatizo wanapenda waendelee wao tu. Kitu kikubwa ni kwamba hawapendi kutegemewa na hivyo hufanya kila njia kuhakikisha watu wa familia wanajitegemea na pia upate wa kukusaidia pindi unapokwama. Hivyo hujitahidi kusaidia wa kwao na hapo upendeleo wa ukabila ndipo unapokuja. Think about it in a wider sense and be honest on your self, utakubali kuwa ukabila upo huko nyumbani Moshi.
 
na mada hii itaendelea kufunua tu sentiments za kibaguzi badala ya kuzifisha chini chini. It is time to come out everybody who is a chagga-hatter.. njoo na kisingizio chochote kile, ili ile siri ya familia yetu tuwe wa kwanza kuikubali.

......haahahaa ha haha,nilijua tuu hiki ndicho unachotafuta kwenye hii topic lakini waungwana walikuwa hawajakuelewa!
 
Kuna mtu amesema Mramba ndiye mmiliki wa precision Air.

Mimi nadhani inamilikiwa na Michael Ngaleko, somebody Shirima nk. au basi pengine mramba ana share ndogo
 
Kama kwa hiari haiwezekani, Rais anaweza kutoa agizo (executive order) na kutaka wachagga waachie ngazi na wakae pembeni kwa angalau miaka mitano ili watu wa makabila mengine wapate nafasi. Hili linaweza kuwahusu Wanyakyusa na Wahaya vile vile. Kama hawatafanya kwa hiari tunaweza kufanya kwa nguvu hata kwa kutunga sheria maalum ya kuwalazimisha.
Kama vile janga la kitaifa??? Jinsi tulivyolishupalia. Ila mbaya wanayofanya hawa ndugu ni kupendeleana waziwazi inapokuja maslahi fulani fulani hasa nafasi za vyeo kazini. Wana....
 
Mkuu Mtanzania,

Heshima mbele, Chadema ni chama cha siasa kama vingine, na kuna some of us tumekuwa tukiwategemea sana na bado tunaaaminia pia, matatizo ndani ya chama ni kawaida, lakini bado ninalia kuwa hili la Wangwe hawakuli-handle kisiasa, siasa za taifa hupangwa haishitukizwi,

Tatizo kwenye siasa sio kuanguka, ila ni how far umeanguka, Public Opinion ndiyo hasa uti wa mgongo wa Chadema, kwenye hili wameharibu tena sana na bado hawajisadii na hizi kampeni wanazozifanya, Makamba sio siri kuwa kwa sasa hatakiwi kabisa ndani ya CCM, lakini bado analiwa timing ya kisiasa na wanaohusika, so far yuko kwenye life support it is only a matter of time kabla hajasukumwa au kujisukuma mwenyewe, kinachoendelea sasa ni yeye kupewa nafasi ya kujimaliza mwenyewe na he is doing very good kwenye hilo, that is politics za taifa,

No question kuwa the man Wangwe is a thug, lakini ni mwanasiasa mzuri kwa sababu anaweza propaganda, serious ishus yeye anazijibu kama nothing, lakini between the line unaona kuwa ishus ni serious hasa anazoshutumiwa, viongozi wa Chadema wajifunze kuwa kuna siasa za ndani za chama na siasa za bunge na mafisadi, kwa sababu they come accross kama ni very angry leaders, wajifunze kufanya transition between kupigana na ufisadi kwenye taifa na how to deal na matatizo ya ndani ya chama, kuwa ni ishu mbili tofauti, Lisu anarusha very serious accusations ambazo huwezi kum-convince mwananchi kuwa Wangwe amezifanya in only seven months za umakamu wake,

Otherswise, ninawatakia Chadema mafanikio mema on how to deal na Wangwe, lakini wasimu-undermine huyu, kwa sababu wengi wao wanaonekana kujawa sana na hasira, sasa anaweza kuwafikisha mahali wakameguka na ni lazima wawe waangalifu sana na ishus za hela kwani zinaonekana kuwa ndio hasa kitovu cha matatizo ya Wangwe, sasa ni rahisi sana kuwashawishi wenye shida ya hela huko kuwa ana hoja,

Halafu pia ni lazima ukweli usemwe kuwa nimeshitushwa sana na charge ya Wangwe kuwa wafanyakazi wengi huko HQ ya Chadema ni kutoka mkoa mmoja, kama ni kweli hii ni ngumu sana kuisafisha lakini only kama ni kweli, ninarudia kuwa viongozi karibu wote wa Chadema walioongelea hii ishu wanaonekana kuwa na hasira sana, to the point kwamba wanarusha serious accusations ambazo in the end zinawafanya wajiweke kwenye mtihani mgumu wa kujibu swali zito kwamba how did the guy became makamu wa Chama kikuubwa kama Chadema?

Ahsante Wakuu!


Kaka kwanza nashukuru umeliona hilo la kuwa Wangwe is a thug. Lakini kumbuka kuwa CCM imefika ilipo kutokana na kosa la kudhani wanaweza kuwatumia thugs bila ya athari na sasa unaona gharama za mtazamo huo kwa chama na Taifa kwa ujumla.

Unaposema kuwa CHADEMA wamefanya makosa ni sawa na kuunga mkono JK na wenziwe wanavyodeal na issue ya mafisadi CCM. Ni kweli litakuwa na athari kwa CHADEMA na hata kuleta mpasuko lakini uthubutu wa kufanya maamuzi kama haya katika hali kama hii na scenarios kama unazozisema ndio uongozi unaotakiwa katika nchi yetu. Siasa za political management ambazo kwa miaka sasa CHADEMA wamekuwa wakizituimia kuhusu Wangwe na ambazo CCM ndizo wanazoaamini zitawatoa katika zahama hii ya sasa ni hatari zaidi.

CHADEMA watatereka kwa muda mfupi lakini watakuwa wamelinda maslahi ya muda mrefu ya CHAMA chao na ya wapenda demokrasia ya vyama vingi. Kumbuka CHADEMA ni kesho na keshokutwa. Sasa ni kubanana tu na CCM wakati kikipumua pumzi za mwisho.

Vilevile kumbuka kuwa CHADEMA kwa sasa wana masikio ya watanzania. Hivyo ni rahisi sasa kwa uongozi wa CHADEMA kujenga ajenda kuliko wangelimwachia hadi hapo baadae CCM watakapoweza kuvuta masikio ya watanzania tena. CHADEMA wana advantage kwa mazingira ya propaganda.

Mimi wangwe alinitoa imani siku ya kwanza tu nilipomwona na suti yake ya kimtandao kama ile aliyovaa PINDA wakati wa KUAPISHWA kama PM huku akiwa ameshika kifimbo kama cha NYERERE. Baadae nilipoona vikaratasi vya propaganda zake za uchaguzi ndipo nikaanza kuhofia mwenendo wa CHADEMA. Mara yakaja ya kukutana na kina Kaborou kupanga mikakati ya uchaguzi na kupokea pesa za kina Rostam na Barricks kwa campeign. Aliponimaliza ni pale alipokuja na ajenda ya kuwanyima CCM nafasi ya kuongoza manispaa ya Dodoma akidi kuwa dawa ya uhuni wa CCM ni kuwafanyia siasa za kihuni.

Kwa kifupi Wangwe ni mwanasiasa na anajitahidi kwa propaganda chafu lakini CHADEMA sio aina ya chama anachopaswa kuwepo. Namshauri ajiunge na MTIKILA ama arudi nyumbani CCM.

Tanzanianjema
 
A MODEST PROPOSAL

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.

Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.

Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.

Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".

Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.

Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.

Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.

Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.

Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.

Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.

Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.

Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.

Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi.



Nashukru kwa kutuletea huu mjadala. Ni ukweli ulio wazi kwamba watu kutoka makabila mengi hapa nchini hawawapendi wenzao wa kabila la kichaga.

Sababu kubwa na ya pekee wanayodai ni kwamba, wachaga waliweza kusoma na kuendelea kutokana na pesa waliyokuwa wakipata wakati ule vyama vya ushirika vilikuwa vinapata RUZUKU kutoka SERIKALINI. Ruzuku hiyo ilitokana na pesa za serikali ambazo hasa zilitokana na aidha MASHIRIKA YA UMMA au KODI za watanzania waliokuwa wanalipa KODI YA KICHWA au KODI WALIYOKUWA WANAKATWA KWENYE MISHAHARA YAO WAKIWA WAFANYAKAZI WA HAYO MASHIRIKA YA UMMA.

Nikutokana na hiyo elimu waliyoipata katika mazingira hayo, makabila mengi yanadai kuwa, wachaga waliweza kunyakua kazi zile zenye kipato cha juu na hasa serikalini na kwenye mashirika ya umma. Huko serikalini na kwenye mashirika ya umma, Wachaga waliweza kunyakua nafasi kubwa kubwa na za kiutawala ambazo ziliwawezesha KUWAVUTA WATOTO WA WAJOMBA NA SHANGAZI ZAO nao wakapewa nafazi za upendeleo zenye ulaji.

Kwa mfano, makabila mengi yanadai kwamba, wachaga waliweza kuingiza watoto wao wengi kwenye jeshi la polisi ati kwa vile tu chuo cha jeshi hilo la polisi kilijengwa nyumbani kwao moshi. Nia na sababu kubwa ni kuwa na access na silaha yaani bunduki ambazo wangeweza kuzitumia wapendavyo!

Haya ni madai ya watu wengi niliowahi kukumbana nao katika mijadala mbalili mbali hasa mashuleni, vyuo vyetu vya hapa nchini na katika vikao vya kijamii na hata kwenye mikutano ya kidini, japo mimi binafsi sidhani kama yana ukweli asilimia 100.
 
teh teh teh tehhhhhheeeeeeeeeeeeeeee, nina element za uchaga na ninajua yanayosemwa ni kweli. Ukienda likizo chrismas kule Moshi utajua haya pia. Ni connection ka kwenda mbele, chagas wapenda maendeleo lakini tatizo wanapenda waendelee wao tu. Kitu kikubwa ni kwamba hawapendi kutegemewa na hivyo hufanya kila njia kuhakikisha watu wa familia wanajitegemea na pia upate wa kukusaidia pindi unapokwama. Hivyo hujitahidi kusaidia wa kwao na hapo upendeleo wa ukabila ndipo unapokuja. Think about it in a wider sense and be honest on your self, utakubali kuwa ukabila upo huko nyumbani Moshi.

Ukabila na ubaguzi umejikita katika tamaduni za watanzania wote lakini inaonekana zaidi kwa wachaga kutokana na wingi wao, rasilimali walizoweza kujikusanyia ambazo zinawawezesha kuwa washindi wa mpambano wa chinichini wa kikabila na zaidi wao wana very organised institutions za "ushindi" ikiwemo safari za nyumbani krismass, role modeling, enterprenuership character na mitandao ya kimaslahi waliyonayo.

JMushi, elimu ya wachaga imekuwa zaidi baada ya uhuru kuliko wakati wa mkoloni. Na hii ilitokana na efforts za wazee wa kichaga waliopata nafasi za juu ikiwemo uwaziri wa elimu kuanzisha mtandano wa mashule kila kona ya kilimanjaro. Enzi za ukoloni waliokuwa wamesoma hawakuwa wachaga. Hata Wazanzibari walikuwa mbele zaidi yao. Wengine walikuwa mbele ni watu wa kusini na Wahaya. lakini sio wachaga.

Huu ni mdahalo hatari lakini muhimu kuuzungumzia kwa uwazi na umakini.....

Tanzanianjema
 
Mkuu hivi kweli kuna makabila HAYAPENDI maendeleo?

Hapana, awe mchagga au msukuma wa kwetu..mtu ukiwa muhangaikaji una stahili kupata unachokipata. Sema kama watu wanapendeleana au hawana vigezo, you can rise an eyebrow. Ila all in all nakubali, WACHAGGA WENGI NI HARDWORKING and most of them they deserve to be where they are. Just like every body! Wasukuma wenzangu..tulikalia kuchunga ng`ombe..ndo hivyo wakina Masanja walio kwenye system ni wachache mno!

Honestly speaking, Mimi siyo Mchagga, but I admire them, wanajua kuhangaika kuliko makabila mengi ya Tanzania. Harafu bwana tunaona wachagga kama wako kwenye nafasi nyingi kwa sababu ya umaskini....kama tungekuwa na uchumi imara..ni kwamba wengi wetu tungekuwa absorbed kwenye sectors nyingine. haya malalamiko yangekuwa hayapo..lakini angalia sector zenye "ulaji" za jamhuri ni TRA na BOT...kila mtu macho yake yako pale! Sasa jamani tufanyeje? tuungane wote tuchape mzigo...maana raia million 40 hiyo BOT na TRA hazitutoshi!

Suluhisho: Kama mtu amekuwa hired kwa mlango wa nyuma, lets condemn that and report it where possible. Lakini haifai kulaumu mtu mwenye kisomo chake ati alipendelewa! Harafu ukishajenga mentality kwamba unaonewa..ndo hivyo utaonewa kweli.

All I know is: we live in a very unkind world where it is man eat man. NA HIYO HAITAISHA LEO WALA KESHO, NI KUCHAPA JOB TUU NDO SULUHISHO MAKINI!


Hakuna asiyependa maendeleo..its true..ila kupenda tu bila kuchukua hatua hakutamfikisha mtu popote..
If wishes were horses everyone would ride one..
Tatizo la makabila yetu mengine ni kuogopa kuumia leo ili upate ahueni kesho...kuanzia shuleni mtu hajibidiishi..ana play truancy kwenda kuwinda ndege wakati wa masomo... au kama ni vyuoni..ikifika saa mbili mtu anavuta shuka hataki kukosa usingizi wake... inapofika kutafuta kazi...hajibidiishi kusoma magezeti ya maana aone opportunities zinazotangzwa bali ni kukusanya magazeti ya udaku kusoma umbeya! Akiona " mchaga" kapata kazi nzuri anaanza..oooh kapendelewa, ohh..kazi haikutangazwa...excuses haziishi... kama ni biashara..basi atakula mtaji na kuwabeza wachagga ati ni stingy...( soma the Rich daddy poor daddy principles au Donald Trump on how to be rich)

I for one have observed how aggressive the chaggas are in striving for a better life. Mtu anajiwekea malengo yake ya maisha.. na anachukua hatua huyafikia..THATS THE ONLY WAY! UKISUBIRI MCHAGGA AKUONYESHE SIRI YA MAFANIKIO UTASUBIRI SANA.. NA PIA HATA AKIKUONYESHA so long as huna the right attitude towards work, utakwama tu!
 
teh teh teh tehhhhhheeeeeeeeeeeeeeee, nina element za uchaga na ninajua yanayosemwa ni kweli. Ukienda likizo chrismas kule Moshi utajua haya pia. Ni connection ka kwenda mbele, chagas wapenda maendeleo lakini tatizo wanapenda waendelee wao tu. Kitu kikubwa ni kwamba hawapendi kutegemewa na hivyo hufanya kila njia kuhakikisha watu wa familia wanajitegemea na pia upate wa kukusaidia pindi unapokwama. Hivyo hujitahidi kusaidia wa kwao na hapo upendeleo wa ukabila ndipo unapokuja. Think about it in a wider sense and be honest on your self, utakubali kuwa ukabila upo huko nyumbani Moshi.

Mama,

Mama hapa ni kama vile sijaelewa,sasa kwa mfano katika ukoo wetu au familia yangu nikitaka kuhimiza uchapaji kazi na kutotaka mtoto kunitegemea kwa kumfanya aanzishe miradi ya Mboga mboga,kuuza karanga nk hapo patakua na tatizo la ukabila kweli?

Maanake mimi naona tatizo la ukabila litakuja pale ambapo nitatumia resources za umma wenye mchanganyiko wa kabila langu unfairly to favour my tribe au tribemates

Ni kweli pia kule moshi wanapenda kuita watua ambao si makabila mengine kuwa ni chasaka kumaanisha wa mbali au pori,kutokana na wao kuona tabia za makabila tofauti kijadi walionyesha laziness zaidi kitu ambacho kimeendelea kuonekana hivyo na wachache.Sasa kwa mfano kule Rombo,Marangu,uru,kibosho,machame nk wanafikiria kama ni mtoto wa kike lazima ajue kulima,kumenya ndizi,kukata majani nk.

Kwa mtoto wa kiume lazima ajue kukwea juu ya mti,kulisha ng'ombe,kukata ndizi na kuwa na ujasiri wa kwenda kutafuta mbali na nyumbani ili mradi sikukuu imkutanishe na familia yake.

Na kwa watu wanaohusisha uchaga na ufisadi au ujambazi,hakuna maadili yoyote huko uchagani yanayomfundisha mchaga awe mtoto wa kike au wa kiume kuiba kama njia mojawapo ya kutafuta.Hizo ni character za mtu binafsi au kuiga na kuonekana ni kudumisha mila
 
Ben,

you have a very good point. Nilimaanisha kuwa mchaga kama angekuwa na uwezo angewafanya wachaga wote wawe na positions nzuri, yaani well paying. Hivyo hujitahidi kuchomeka watu wao kwenye hizi posts well paying. Na kama sio kupewa nafasi ya kazi basi hata ni kutoa tenda ili tu mwenzie afanikiwe. Na pia hupenda sana cha juu (10%).

Kumweka ndugu au jamaa utaua ndege wengi kwa jiwe moja. Kwanza utapata cha juu bila kelele wala kokoro. Then utakuwa umeondoa utegemezi, yaani kuja kuliliwa shida kila siku na kukubidi kutoa za mfukoni mwako na pia hata ukidondoka una mtu wa kukunyanyua, kwani uliowasaidia kuwaweka kwenye nafasi hawawezi kukuacha ukaadhirika. Watafanya vikao kukutafutia kazi na kama ni mtaji wako radhi hata kuchangishana. It is a good sprit, ila tatizo linalopigiwa kelele ni wao kujilimbikizia hizo nafasi ambazo zilitakiwa ziwe za mgawanyo sawa kwa watanzania wote wenye qualifications.

Hawa ndio walioanzisha mchezo wa technical know who. In what sense, yaani kigogo wa kichaga atafanya awezalo kucreate position ambayo itamsuit mtu anayemfahamu. Sasa hapo interviewee vigezo vyote nakuwa anavyo kupata kazi husika.
 
Mtandao wa Wachaga kwenye TAASISI na IDARA za UMMA umekomaa na kuimarika sana kama CCM ilivyojikita kila mahali Tanzania hii ya leo. Maoni yangu ni tuendelee kuilinda IKULU yetu tu ili IBAKI kuwa MALI ya WATANZANIA wote. HILI, CCM wameliweza.
 
Ninachojua mimi ni kuwa jukwaa hili ni la watu wachambuzi wa mambo kwa umakini sana.

Mwanakijiji ameamua kuwasilisha maumivu yake aliyonayo kuhusu namna wachaga wanavyobaguliwa na kuonyesha jinsi ilivyo ujinga kuwa na fikra hizo. Mbinu aliyotumia katika STYLISTIC inaitwa Ironic au satirical.
We normal present our idea satirically when they might be ambiguous and their weights are so big that it can risk harmony of the community.


Ahaa!!!!!!!!!
 
Ukitaka kwuona ukabila haswa nenda pale NIC life house kisha cheki ubao unaoonyesha nani yuko wapi kwenye ofisi hipi... ni "Mwa...." kwenda mbele...
 
Mwanakijiji,

Naomba nikushukuru kwa kuwa na uwezo mzuri wa kuspin na kuwapata baadhi ya watu humu.

Hongera, ila sisi wakulu wa kale huwezi kutupata.

Tukubaliane kutokubaliana.

Asante

FairPlayer
 
Ben,

you have a very good point. Nilimaanisha kuwa mchaga kama angekuwa na uwezo angewafanya wachaga wote wawe na positions nzuri, yaani well paying. Hivyo hujitahidi kuchomeka watu wao kwenye hizi posts well paying. Na kama sio kupewa nafasi ya kazi basi hata ni kutoa tenda ili tu mwenzie afanikiwe. Na pia hupenda sana cha juu (10%).

Kumweka ndugu au jamaa utaua ndege wengi kwa jiwe moja. Kwanza utapata cha juu bila kelele wala kokoro. Then utakuwa umeondoa utegemezi, yaani kuja kuliliwa shida kila siku na kukubidi kutoa za mfukoni mwako na pia hata ukidondoka una mtu wa kukunyanyua, kwani uliowasaidia kuwaweka kwenye nafasi hawawezi kukuacha ukaadhirika. Watafanya vikao kukutafutia kazi na kama ni mtaji wako radhi hata kuchangishana. It is a good sprit, ila tatizo linalopigiwa kelele ni wao kujilimbikizia hizo nafasi ambazo zilitakiwa ziwe za mgawanyo sawa kwa watanzania wote wenye qualifications.

Hawa ndio walioanzisha mchezo wa technical know who. In what sense, yaani kigogo wa kichaga atafanya awezalo kucreate position ambayo itamsuit mtu anayemfahamu. Sasa hapo interviewee vigezo vyote nakuwa anavyo kupata kazi husika.

Mama,

Naona umezidisha utaaalamu. sasa mpaka hapo tuko pamoja,tukubalianae kulimbikiziana posts kwa point ya uchaga bila kujali usawa wa Watanzania wenye qualification sawa Ni ukabila.

sasa mama utakua na right ya kuuzungumzia huu uakabila wa aina hii,lakini sasa hizi chuki zinakuzwa mno kwa malengo ya kisiasa.nasema huko tunakoenda ni disaster kama hatua madhubuti hazitachukuliwa.


Pia,kuhusu haya masuala ya maendeleo natamani kama jamii ya makabila mengine kama ingeiga hii spirit ya kuchangishana.kwa mfano ukienda kule uchagani utakuta watu wamejenga kutokana na kuwa na vikundi vya kuchangishana,wenyewe kama huko Rombo wanaita 'kiarano' yaani kusaidiana.Hivi vikundi viko organised katika basis za wafanyabiashara,waalimu,ukoo nk ambapo hukutana kila mwezi kwa mzunguko kuchangishana fedha,au mabati ya kujengea nyumba na ni sharti kila mtu aende na mkewe au mmewe kwa wale waliooa au kuolewa na Mbege ni mila yao kuu inayoandaliwa wakati wanapokutana(maanke kule mbege hata mlokole anakuambia si pombe).Sasa unaona hata kama mtu anafanya shughuli zake Arusha au Moshi Mjini ni lazima aende kwao kuchangia katika maendeleo.wengine hadi wameanzisha vikundi vya kusaidiana katika msiba.
 
Mtandao wa Wachaga kwenye TAASISI na IDARA za UMMA umekomaa na kuimarika sana kama CCM ilivyojikita kila mahali Tanzania hii ya leo. Maoni yangu ni tuendelee kuilinda IKULU yetu tu ili IBAKI kuwa MALI ya WATANZANIA wote. HILI, CCM wameliweza.

Mkuu,

Unamaanisha nini? Sasa kwa mantiki hiyo sitaki kulazimika kuamini kwamba unamanisha kuilinda ikulu isiongozwe na Mchagga? Sasa hapo mkulu si utakua umeendekeza ukabila at the highest level?

Kuna hii statement ya kwamba Mchagga hawezi kuingia ikulu,hii ni ya ubaguzi wa hali ya juu na ni statement ambayo imekua ikihusishwa na role model wa Watanzania wengi.Huu ni ukabila uliopita vipimo vyote hata zaidi ya ubaguzi wa kikaburu.NALAANI KWA NGUVU ZOTE HII KAULI!
 
Mwanakijiji,

Naomba nikushukuru kwa kuwa na uwezo mzuri wa kuspin na kuwapata baadhi ya watu humu.

Hongera, ila sisi wakulu wa kale huwezi kutupata.

Tukubaliane kutokubaliana.

Asante

FairPlayer
Na bado ngoja aendelee kuwachanganya.....si unaoan watu wanavyojichanganya.....utakuja kusikia kitu baadae
 
Ikulu si iko sawa kwa ajili ya watanzania wote? Na kama kutumia raslimali au vyeo vya uma kwa upendeleo na kwa kigezo cha ukabila,Ni ubaguzi au UKABILA;je,si UKABILA kuzuia mtu kushika ofisi fulani ambayo ni haki ya kila mtanzania kwa kutoa hukumu kwa kundi fulani lenye tabia zenye uhusiano wa kinasaba na kabila Fulani?
 
Mwanakijiji,

Naomba nikushukuru kwa kuwa na uwezo mzuri wa kuspin na kuwapata baadhi ya watu humu.

Hongera, ila sisi wakulu wa kale huwezi kutupata.

Tukubaliane kutokubaliana.

Asante

FairPlayer


.....suspicions, accusations towards Chagas is real mzee,nilifikiri is just story za kijiwe tuu lakini mmmmhhhhhh,we need tolerance for equal and united TZ la sivyo we'll all perish like fools,lakini sentiments za watu humu nimeogopa sana!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom