Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Mwanakijiji,
..halafu watu wako too obssesed na wachaga wa tra na chadema.
..kuna Wachaga wengi tu wanashona viatu,mafundi welding, mechanics, wauza bucha, wachoma mishkaki, madereva wa daladala,....husikii wananchi wakiwalalamikia hao.
Joka,
Sidhani kuwa watu wako too obsessed na wachaga kwenye TRA na CHADEMA tu, hizo mbili ni zile tu ambazo tu zilizokuwa mbele hivi karibuni. Lakini ukweli ni kuwa sehemu nyingi serikalini na hata kwenye biashara binafsi, hayo malalamiko yapo wazi.
Lakini sidhani kuwa hayo malalamiko hayana ukweli, hasa ukichukulia simple statistics ulizoonyesha. Tanzania kuna graduates kutoka makabila karibu yote kwenye kila taaluma ingawa kuna makabila yenye namba kubwa zaidi kuliko wengine. Kwa hiyo inapotokea wahasibu wengi wa TRA wanapokuwa kabila moja na bosi wao, hiyo ina haki ya wengine kulalamika hata kama hilo kabila wana 15% au zaidi ya graduates wa BCom au Adv. Dipl. in Tax Management za IFM.
Tuachane na kupigilia misituni, ukweli unajulikana kuwa, yapo makabila Tanzania yenye tabia za kujipendelea bila hata ya kuona aibu na yamejulikana kufanya hivyo tokea nchi yetu ilipoanzishwa. Tulipasue hili jipu ili maumivu yake yawe ni ya muda tu otherwise litazua mengine.
La muhimu ni kwa hayo makabila kujiangalia wenyewe katika matendo yao na waTanzania kutofungia macho huo upendeleo unapotokea ili uangaliwe ukweli wake.