Tonga,
Mkuu mimi nilisema toka mwanzo kuwa siwezi kuchangia hoja za mada hii kuhusiana na hilo la Wachagga kuachia ngazi! Na nilimfahamu vizuri Mwanakijiji alipoanzisha mada hii baada ya kumuuliza nini madhumuni yake..Aliponipa picha nikamsoma kisawasawa!
Swala hili linahusiana sana na lile la Wangwe na kama umesoma vizuri maandishi yangu nimekuwa nikitoa maelezo yangu kuhusiana na jinsi navyoliona sakata la Wangwe na msimamo wangu umebakia palepale kutoshambuliana watu kwa kuvuana nguo hali tatizo kama lipo mnaliacha likizidi kupamba mafuta.
Wewe kwa mfano ulipokuja na majibu yako ambayo kusema kweli una kila haki ya kujitetea lakini naliona kosa unapotetea kwa niaba ya Wachagga wote..Kisha hasira na uchungu unaoupata ndio ule walioupata baadhi ya wana Chadema yaani wameshindwa kufikiria nje ya box! fikra zao zimefungwa kutokana na mapenzi ya chama akama wewe ulivyofungwa katika mapenzi ya kabila lako..
Kitu kilichonifanya mimi nichangie mada hii ni pale watu walipoanza kutumia ELIMU kama ndio kisingizio cha Wachagga kuwa mbele - nikageukia kwa Chadema kama majibu hayo yanaweza kujenga msingi bora ktk fikra za watu!..Sikuona zaidi ya kugawanyika zaidi.
Na hakika nilitegemea baadhi ya viongozi wa Chadema wanaweza kutumia vigezo kama hivi kuelezea sababu za madai ya Wangwe kuwa ni wivu kwa Wachagga bahati haikutokea.. Nimesoma sana maelezo ya baadhi viongozi wa Chadema na kwa hakika kila nachosoma ni kumzungumzia Wangwe - Mkurya ambaye ana matatizo na Viongozi wote wa Chadema hata wale wasiokuwa Wachagga!.. Hili bado sio jibu hata kidogo kwa wananchi ambao hawana mpango na Wangwe isipokuwa hoja yake!!.. Je, kweli Ukabila Upo?..hata kama ni kichaa ni muhimu tuelewe kwamba wananchi watanunua hoja kama hizi kirahisi sana, cha msingi ni kuelewa kuna maelezo gani kufunika madai ya Wangwe!
Muda mrefu viongozi wa Chadema wametumia majibu sawa na yako, wametumia hasira wakimtazama Wangwe kumbe wazee wa mabaza wanaoweza kutoa hukumu ni wananchi sio Wangwe! majibu yao badala ya kujenga yanazidisha maswali zaidi ktk hoja ya Ukabila...
Ndio maana nasema kwamba ni muhimu tuitazame hoja iliyopo Ubaoni badala ya wahusika.. mathlan wamesema kuna Ukabila ktk Ofisi za TRA, well nia na madhumuni ya hoja kama hiyo ni kuulizia utaratibu gani umetumika ktk kutoa ajira sehemu hiyo ya ULAJI!... Na swala la Wangwe kwa Chadema dhahiri ni ktk kuona kaputwa tonge la wali mkononi!.. Kwa nini kaputwa sababu nyingi zimeelezwa, kisha mkuu Wangwe akatoa madai ambayo yanatisha. na ukitazama kwa haraka unaweza kuamini kama ilivyoTRA lakini kabla hujaamini ni bora tupate maelezo na taratibu za ajira hizo. Kwa bahati mbaya hakuna mwenye ukweli ktk sakata la TRA lakini mimi binafsi nimeridhika na majibu ya Bi. Asha Abdala kwamba Chadema wameteua wabunge wale kwa kupitia kamati ya Wanawake ambayo inaondoa kosa hili toka Utawala - human resorce ya chama hicho. Sasa huko kwa kamati ya wanawake sijui ni utaratibu gani ulitumika nakama lilikuwa kosa kuwapendelea wanawake! hilo sijalisikia toka upande wowote.
Pamoja na yote hayo jibu la Bibie limeondoa dosari na madai ya Chacha kwamba uteuzi wa wabunge hao ulifanywa na viongozi wa Chadema. Pili kati yetu hatufahamu kulikuwepo na majina mangapi ya wanawake ktk uteuzi ule kiasi kwamba tunaweza kudai kuwepo kwa wengine wenye uwezo. Kwa hiyo pamoja na kwamba mada hii ni ya uchochezi lakini ina mantiki sana kama utaweza kutenganisha fikra zako nje ya sanduku la Kabila...
Watazame watu wote wa makabila kama sawa na hakuna kabila pumbavu wala wazembe ambao hawastahili ajira.. Generalizing ndio cheche za wenye kuleta hoja na majibu yenye mtazamo huo huo ndio yametufikisha hapa tulipo..