Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
"kuna suali niliuliza mwanzo na sikujibiwa na mtu yeyote..... ni kuwa ukiachilia mbali serikalini au mashirika ya umma..ambako huenda kuna possibility ya kupendeleana.. je how do you explain dominance ya hawa wenzetu kwenye international orgs kama UN, bilateral agencies, private companies... je huko pia kuna ndugu zao wanawavuta? mimi nimekuwa nashangaa ni kwanini wamejaa huko kuliko makabila mengine na inajulikana wazi kuwa kazi hizo zinapatikana through a due process na ni meritocrity ndiyo inayoamua upate au ukose kazi.[/COLOR]....im still waiting to get people's views on this".

Yeap, there you go hapa umenena (am refering to the above paragraph), kama hao wachagga wanapendeleana katika mashirika ya umma na serikalini, hebu Mkjj na supporter wengine mjibu swali lililoulizwa hapo juu, nanukuu sehemu hii "how do you explain dominance ya hawa wenzetu kwenye international orgs kama UN etc...." ninasubiri majibu ya wakereketwa ili nijue siri ya hawa wachagga.
All the best.[/QUOTE]

Tonga,
Thanks for raising y0ur voice on this maana nimeuliza zaidi ya mara tatu in different posts lakini hakuna aliyejibu....
It will be interesting to hear what people have to say..esp tha anti-chaggas
 
Huo ni ukweli. Sio kwa sababu wako Wachaga wengi kwenye hiyo ofisi bali Wachaga wanajua rohoni mwao kuwa hawapendwi simply kwa sababu ni Wachaga.
Wengi wameacha majina halisi ya ukoo ili kuwafix wasiojua.

Ajabu ni kuwa nilikutana na Mhindi mmoja Director wa Kampuni kubwa, ya magari akaniambia anatafuta kijana wa Kichaga katika nafasi fulani. Nilishangaa kweli maana ni nadra kwa Msukuma au Mnyamwezi kufanya hivyo. Kuna sababu maalumu nadhani ,japo alikataa kuniambia kwa nini preference yake ni Mchaga. Nikisoma na hapa JF watu walioonyesha chuki za wazi na hili la Mhindi nabaki mtupu. Labda wahindi tu ndio hawawachukii Wachaga .Do'nt know.....

Yeap, there you go hapa umenena (am refering to the above paragraph), kama hao wachagga wanapendeleana katika mashirika ya umma na serikalini, hebu Mkjj na supporter wengine mjibu swali lililoulizwa hapo juu, nanukuu sehemu hii "how do you explain dominance ya hawa wenzetu kwenye international orgs kama UN etc...." ninasubiri majibu ya wakereketwa ili nijue siri ya hawa wachagga.
All the best.

Tonga,
Thanks for raising y0ur voice on this maana nimeuliza zaidi ya mara tatu in different posts lakini hakuna aliyejibu....
It will be interesting to hear what people have to say..esp tha anti-chaggas
[/QUOTE]

Womenofsubstanc you have a very strong point there, kudos to you . Ila ukiona kimya ujue hawana la kusema au kwa maneno mengine wameishiwa na BS. Mi nimeuliza kama kuna data ambazo zinaonyesha huo wingi wa wachanga almost everywhere in Tz as they claimed in this forum, lakini sijaona any answer or data so far! ila wanaendelea kupigilia misumari kwenye topic ambayo haina ushahidi wowote. Na sasa hakuna anayetaka kukujibu swali ulilouliza kwasababu hakuna mwenye jibu la msingi! Watuambie kama huko UN boss wao ni mchagga, tunafanya kazi na watu ambao hata hawajui mchaga ni nani, ila wenye roho ya korosho wakisikia wanaraise eyebrow. Ndio maana nilisema; "kelele za chura huwa hazimnyimi mwenye nyumba usingizi".
 
Swali la dominance is iherently misleading. Unaposema kuna dominance ya wachagga kwenye mashirika ya kimataifa you are assuming everybody accept that (pseudo-obviousness).

Ili niweze kujaribu kutoa jibu naomba ufanye vifuatavyo:

Chagua makampuni manne au matano tu ambayo yana Watanzania halafu tuone wachagga wana namba gani, ili angalau tukubali hoja yako posteriori.
 
Tee teeeee, naona hamtaki tu kumaliza. Mie napendekeza kila mtu achukue Kalashnikov au AK-47 na tukutane KAHE. Hapo tuanze BIG PARTY. Kalashnikov zikianza KUTOA moshi wa kutosha, tutaona kweli madhara yale makubwa ambayo Madaktari siku zote wanasema kuwa SMOKING KILL. Hiii, hiiiii, yangu itakuwa inatema Moshi kama KIKO cha Mzee Muro wa pale KWA SADALA..
 
kubwajinga,

..mradi unaozungumzia umeanza wakati wa Magufuli, haukuanza na Mramba.

..mkandarasi huanza kazi na baadaye kulipwa kama consultant ameidhinisha alipwe.

..nimekuonyesha barabara zote ambazo vw bettle ingeweza kupita. ni sikuona kama una shida nazo ila hiyo iliyoko rombo tu.

Ndio maana nikakuambia ulinganishe umuhimu barabara ya Rombo na hizo ulizotaja, kwa mfano Chalinze-Segera.

Hata tu ukifanya traffic count, huwezi kuhalalisha investment tuliyofanya Rombo vs say kama tungeifanyia Kigoma - Tabora, Dodoma - Shinyanga. Au kuunganisha mikoa miwili/ mitatu mizima mmoja ukiwa na bandari kubwa tu ambayo hivi sasa haifikiki. Eti ukitaka kwenda Mtwara, njia nzuri ni meli ya sijui 1st or 2nd world war. This is non-sence.

..kuna suala la maintenance vilevile na kuna barabara nyingi tu zinafanyiwa maintanance wakati kuna maeneo mengine hayana hata barabara.

..hii mantiki yako kwamba kwasababu barabara inaweza kupitisha vw bettle basi haipaswi kutengewa fedha ktk mazingira yoyote yale ina walakini.

Hicho ni kipimo kizuri sana cha kuonyesha kama barabara inapitika na haina uharaka wa lami, unless kuwe kuna bandari au airport huko. Mtwara huthubutu kwenda na hata Toyota Staut na hivyo hata bandari haitumiki.

..mimi naomba utusaidie kwa kutuonyesha kwamba serikali ktk miradi ya barabara imekuwa ikidhulumu mikoa ya kusini.

Sidhani kama unahitaji msaada wangu kwenye hili. Kama uko bongo, panda basi uende Mtwara uone cha moto.

..Kenya is one of our biggest trading partner na hata investor, kwa hiyo ndiyo barabara ya zinazoelekea huko zina umuhimu wake. na kuna hili suala la Afrika Mashariki.

Huu sio mpaka wa maana na ndio maana umetumika zaidi kwenye magendo badala ya biashara halali. Kama ni mipaka muhimu inayohitaji barabara nzuri ni kama ile ya Namanga, Arusha au Horohoro, Tanga. Yote hii barabara zake sio nzuri hasa Horohoro. Huu ulikuwa ni upendeleo wazi na huhitaji kuwa rocket scientist kujua ni nani aliyeufanya.
 
Kubwa Jinga.. ni kwa kiasi gani Waziri ana nguvu ya kuamua fedha ya maendeleo iende kwenye jimbo lake au jimbo lolote lile? Na inawezekana vipi mtu mmoja (Mramba) kuwa na nguvu ya kuamua kupeleka fedha hiyo yote kwenye Bunge ambalo lina watu wa makabila mbalimbali, lenye Rais kutoka mikoa isiyo na barabara nzuri, na Waziri Mkuu ambaye kwake pia si kuzuri? Unataka tuamini kuwa aidha Mramba is the most convincing and conning politician in Tanzania au tuna mawaziri na Rais mbumbumbu kuliko yeyote aliyewahi kutawala!

Hii nguvu mnayompa Mramba ndiyo inasema mengi kuhusu watu wengine kuliko yeye. Lakini kwanza, jibu hilo la Waziri ana nguvu gani za kisheria na kiutendaji zinazoweza kumfanya aamue peke yake kufanya maamuzi ya kupeleka fedha kwenye jimbo lake? Maana kama ni fedha, ziliombwa Bungeni na Bunge la watu wa makabila mengi tu zikapitisha! why blame Mramba?

MMJJ,
Unless kama umefanya kazi serikalini, then huwezi jua nguvu za mawaziri na hata baadhi ya wabunge.

Budgeting zinafanywa wizarani na unless kuwe kuna vitu anavyohitaji raisi vifanyike, waziri ndie muamuzi wa yote. Hawa wanao uwezo mkubwa kupendelea mahali popote maana system yetu haiko wazi. Niambie ni nani anayefahamu miradi ipi ya barabara inayohitajika kutekelezwa mwakani 2009 na ipi ni ya muhimu zaidi ya mingine?? Upi ni wa kwanza, pili, tatu n.k. kulingana na umuhimu wake na hivyo pesa itafuata huo mtiririko?? Haya ni maamuzi wanayofanya mawaziri wenyewe wakishirikiana na waziri wa fedha.

Msuya alipokuwa waziri wa fedha aliweza kupeleka miradi mingi tu wilayani kwake na kupaneemesha. Mmoja kati ya miradi hiyo ulikuwa diverted badala ya kwenda Mbeya, ukapelekwa Kilimanjaro.

Mramba alikuwa na karata zote kwenye mradi wa Rombo, Mawasiliano na baadaye Fedha.
 
Umekuwa ukizungumza vitu vya msingi, lakini katika hili umedhihiria hufahamu jinsi gani serikali inafanya kazi. No sir.. kila kitu kinachofanyika ndani ya mwaka ujao kinapitishwa na wabunge kwenye Bunge la Bajeti. Siku moja ukae chini uangalia Bunge linapokaa kama Kamati na kupitia bajeti kifungu kwa kifungu.

Msuya alipokuwa waziri wa fedha aliweza kupeleka miradi mingi tu wilayani kwake na kupaneemesha. Mmoja kati ya miradi hiyo ulikuwa diverted badala ya kwenda Mbeya, ukapelekwa Kilimanjaro.

Kama hilo lilifanyika na hakukuwa na mtu aliyenyosha mkono kupinga au kukataa hilo si la kumlaumu Waziri ni hao waliofahamu juu ya jambo hili na wakakaa kimya kubariki jambo hilo. Ile ungetoa mfano wa mradi huo ili wanaojua watupe data.

Mramba alikuwa na karata zote kwenye mradi wa Rombo, Mawasiliano na baadaye Fedha.

Nani alimpa nafasi hizo zote katika Uwaziri, kwa hakika hakujipachika. Na kama Baraza la Mawaziri lilifanya kama alichofanya Karamagi na TICTS kwanini tumlaumu Karamagi tu. Kwanini mzigo wa lawama wasibebeshwe serikali nzima?
 
Tee teeeee, naona hamtaki tu kumaliza. Mie napendekeza kila mtu achukue Kalashnikov au AK-47 na tukutane KAHE. Hapo tuanze BIG PARTY. Kalashnikov zikianza KUTOA moshi wa kutosha, tutaona kweli madhara yale makubwa ambayo Madaktari siku zote wanasema kuwa SMOKING KILL. Hiii, hiiiii, yangu itakuwa inatema Moshi kama KIKO cha Mzee Muro wa pale KWA SADALA..

I am on my way!
 
Umekuwa ukizungumza vitu vya msingi, lakini katika hili umedhihiria hufahamu jinsi gani serikali inafanya kazi. No sir.. kila kitu kinachofanyika ndani ya mwaka ujao kinapitishwa na wabunge kwenye Bunge la Bajeti. Siku moja ukae chini uangalia Bunge linapokaa kama Kamati na kupitia bajeti kifungu kwa kifungu.

Nimeifanyia kazi serikali ya TZ na serikali nyingine mbalimbali na nimeona tofauti zake. Mipango yetu TZ inabadilika kila mwaka kulingana na ni nani yuko ofisini wakati huo. Nilichomaanisha hapa ni kuwa, ukiondoa ile miradi iliyopitishwa kwenye bajeti ya mwaka huu, mingine yote inayofuatia miaka ijayo haina utaratibu unaoeleweka ki-umuhimu wake. Waziri wa wakati huo ndiye mwenye maamuzi ya kipi kifanyike na kipi kilale.

Kama hilo lilifanyika na hakukuwa na mtu aliyenyosha mkono kupinga au kukataa hilo si la kumlaumu Waziri ni hao waliofahamu juu ya jambo hili na wakakaa kimya kubariki jambo hilo. Ile ungetoa mfano wa mradi huo ili wanaojua watupe data.

Kwa nini asilaumiwe waziri aliyetenda kosa walaumiwe walioshuhudia tu baada ya kosa kutendeka? Hao mawaziri wote waliojiletea upendeleo bila kuangalia maslahi ya taifa ndio wanatakiwa kuwajibika au kuadhibiwa kama ikiwezekana.

Nani alimpa nafasi hizo zote katika Uwaziri, kwa hakika hakujipachika. Na kama Baraza la Mawaziri lilifanya kama alichofanya Karamagi na TICTS kwanini tumlaumu Karamagi tu. Kwanini mzigo wa lawama wasibebeshwe serikali nzima?

Angalau umekumbuka mfano mwingine wa Karamagi kuonyesha jinsi mawaziri wanavyoweza kujipendelea. Mramba, Karamagi n.k., kwa wao kupewa nafasi za kulihudumia taifa haina maana kuzitumia nafasi hizo kwa manufaa binafsi.
 
Nimeifanyia kazi serikali ya TZ na serikali nyingine mbalimbali na nimeona tofauti zake. Mipango yetu TZ inabadilika kila mwaka kulingana na ni nani yuko ofisini wakati huo. Nilichomaanisha hapa ni kuwa, ukiondoa ile miradi iliyopitishwa kwenye bajeti ya mwaka huu, mingine yote inayofuatia miaka ijayo haina utaratibu unaoeleweka ki-umuhimu wake. Waziri wa wakati huo ndiye mwenye maamuzi ya kipi kifanyike na kipi kilale.

Hiyo nguvu unayoizungumzia haina msingi wa kisheria. Kama kuna jambo lolote linafanywa nje ya sheria ni uvunjaji wa sheria na siyo nguvu halali. Sasa kama Mramba alikuwa anafanya mambo ya sheria na watu walikuwa wanamkodolea macho bila kumwajibisha basi ni watu hao na Mramba wa kubeba jukumu hilo. Kwa sababu kwanza siamini kama Mramba aliweza kufanya mambo yote peke yake bila kushirikiana na mtu mwingine, na kama kuna overwhelming evidence kuwa alivunja sheria Mramba ajiandae kwa pingu.

Lakini bado nakataa kuwa Waziri ana nguvu za kufanya anachotaka alimradi yeye ni waziri. Hiyo ni nguvu ambayo wafanyakazi wa serikali wamewaachia na kama wewe umefanya kazi serikalini (nimefanya kazi pia, so I know very well what I'm talking about), utaona kuwa kuna nguvu za kisheria na nguvu za kujipachika. Ukiangalia ripoti ya mkaguzi mkuu utaona kuwa ndani yake mambo mengi yamefanywa kwa sababu viongozi wanafikiri au wanaamini kuwa wana nguvu za namna hiyo. NI mpaka pale tutakapowawajibisha watu ndipo watakapoelewa na kuanza kufuata sheria.

Siku si nyingi Mramba atatolewa mfano (japo si kwa suala la barabara). Lakini hilo la Mramba halihalalishi hata kidogo the demonization of the whole people kwa sababu ya kosa la mtu mmoja. Hakuna hilo, kila mtu anahukumiwa kivyake vyake.

Kwa nini asilaumiwe waziri aliyetenda kosa walaumiwe walioshuhudia tu baada ya kosa kutendeka? Hao mawaziri wote waliojiletea upendeleo bila kuangalia maslahi ya taifa ndio wanatakiwa kuwajibika au kuadhibiwa kama ikiwezekana.

Agreed, endapo alichofanya ni kinyume na sheria na nje ya nguvu zake. Na hadi sasa hujaonesha mahali popote ambapo Waziri anatakiwa asilete maendeleo jimboni kwake. Unaweza kuonesha hivyo kwa kutuambia chini ya Mramba hakuna barabara hata moja ya mkoa mwingine au sehemu nyingine zilizotengenezwa isipokuwa za Kilimanjaro, now that would be a very strong case ya matumizi mabaya ya madaraka au hata upendeleo.

Angalau umekumbuka mfano mwingine wa Karamagi kuonyesha jinsi mawaziri wanavyoweza kujipendelea. Mramba, Karamagi n.k., kwa wao kupewa nafasi za kulihudumia taifa haina maana kuzitumia nafasi hizo kwa manufaa binafsi.[/QUOTE]

Je ni mawaziri tu wanaojipendelea na kupendelea watu wa kwao? Je kwa kufanya hivyo inamaana basi makabila yao yanabeba dhambi zao? Wangapi ambao wanajenga makwao? Ni wangapi ambao wenye mabasi wanaotoka Iringa ambao wana mabasi yanayoenda Iringa? Je kwa kufanya hivyo tunaweza kusema wahehe wana ukabila kwa kujipendelea? Tujifunze kuwawajibisha watu kwa makosa yao wao wenyewe badala ya kuhukumu kabila au jamii nzima ya watu.

That is the only point I'm making, do we agree?
 
Hiyo nguvu unayoizungumzia haina msingi wa kisheria. Kama kuna jambo lolote linafanywa nje ya sheria ni uvunjaji wa sheria na siyo nguvu halali.

Are you serious or you are jocking?? Kwenye ulaji au maslahi binafsi TZ, who cares about sheria?? Sheria inapindwa mpaka ifuate yanayotendeka, ikishindikana inarukwa. Muulize mwanasheria mkuu wa zamani Chenge atakuelimisha.

Sasa kama Mramba alikuwa anafanya mambo ya sheria na watu walikuwa wanamkodolea macho bila kumwajibisha basi ni watu hao na Mramba wa kubeba jukumu hilo. Kwa sababu kwanza siamini kama Mramba aliweza kufanya mambo yote peke yake bila kushirikiana na mtu mwingine, na kama kuna overwhelming evidence kuwa alivunja sheria Mramba ajiandae kwa pingu.

Lakini bado nakataa kuwa Waziri ana nguvu za kufanya anachotaka alimradi yeye ni waziri. Hiyo ni nguvu ambayo wafanyakazi wa serikali wamewaachia na kama wewe umefanya kazi serikalini (nimefanya kazi pia, so I know very well what I'm talking about), utaona kuwa kuna nguvu za kisheria na nguvu za kujipachika. Ukiangalia ripoti ya mkaguzi mkuu utaona kuwa ndani yake mambo mengi yamefanywa kwa sababu viongozi wanafikiri au wanaamini kuwa wana nguvu za namna hiyo. NI mpaka pale tutakapowawajibisha watu ndipo watakapoelewa na kuanza kufuata sheria.

Ukiwa waziri TZ unatoa tu amri na walio chini wanaitekeleza. Kwa hiyo unaweza kuitafsiri vyovyote utakavyo, either kuwa hajafanya mwenyewe au la. Cha kufahamu hapa ni kuwa amri yake ndio iliyotekelezwa. Umesahau zile amri za Lowassa au za Mrema zilivyowatetemesha hata mawaziri?? Kama huamini nguvu walizo nazo mawaziri, muulize Masha, mara tu baada ya kuupewa ukuu, alionaje nguvu ya amri zake??

Sheria zipo, lakini nani asiyejua kuwa wasemacho wakuu TZ nacho kinakuwa sheria by default??

Siku si nyingi Mramba atatolewa mfano (japo si kwa suala la barabara). Lakini hilo la Mramba halihalalishi hata kidogo the demonization of the whole people kwa sababu ya kosa la mtu mmoja. Hakuna hilo, kila mtu anahukumiwa kivyake vyake.

Huyo aliyesema kuwa aliyofanya Mramba ndio wanayofanya warombo wote ni mpuuzi. Hili ni la upendeleo wa mtu mmoja kwa jimbo lake. Inaweza ikawa ni elements za ukabila au ametumia nafasi kujijenga kisiasa au both. Unfortunately, it just happened kuwa Mramba naye ni mchaga lakini alichofanya ni wrong.

Agreed, endapo alichofanya ni kinyume na sheria na nje ya nguvu zake. Na hadi sasa hujaonesha mahali popote ambapo Waziri anatakiwa asilete maendeleo jimboni kwake. Unaweza kuonesha hivyo kwa kutuambia chini ya Mramba hakuna barabara hata moja ya mkoa mwingine au sehemu nyingine zilizotengenezwa isipokuwa za Kilimanjaro, now that would be a very strong case ya matumizi mabaya ya madaraka au hata upendeleo.

Kama yule mbunge, nafikiri alikuwa ni Seleli, aliyelalamika wakati Mramba anapeleka pesa kwao hakuona kuwa kuna upendeleo, basi tupo wengi wenye makengeza.

Hapakuwa na umuhimu wa kuweka lami kwa zaidi ya km 100 za barabara to no where (Tarakea) wakati Rombo ilikuwa less than 50km kutoka kwenye barabara kuu ya lami ambapo pia kuna zaidi ya km 600 za kwenda Mtwara zitakazoweza kuifungua bandari yake, au km 500 kwenda Shinyanga -Kigoma za kuifungua hii wild west ambazo zingehitaji pesa hiyo hiyo.

Alichofanya Mramba ni upendeleo unaozorotesha maendeleo. Rombo hadi Tarakea siku zote kumekuwa kunapitika vizuri sana licha ya idadi ndogo ya magari yanayoenda huko. Huku kwengine hakuendeki kabisaa, angalia hizo picha hapo chini.

Je ni mawaziri tu wanaojipendelea na kupendelea watu wa kwao? Je kwa kufanya hivyo inamaana basi makabila yao yanabeba dhambi zao? Wangapi ambao wanajenga makwao? Ni wangapi ambao wenye mabasi wanaotoka Iringa ambao wana mabasi yanayoenda Iringa? Je kwa kufanya hivyo tunaweza kusema wahehe wana ukabila kwa kujipendelea? Tujifunze kuwawajibisha watu kwa makosa yao wao wenyewe badala ya kuhukumu kabila au jamii nzima ya watu. That is the only point I'm making, do we agree?

Hili tumeshaliongelea hapo juu. La muhimu kwangu ni kuwa alilofanya Mramba ni kosa ambalo limeirudisha nchi nyuma na hatakiwi hivi sasa alitambie bungeni. Pesa ya ujenzi wa barabara inafanyiwa kazi watu wote.

NJILI_pics%2B072.jpg

NJILI_pics%2B069.jpg

Hii ndiyo hali ya barabara kuu ya kuunganisha mikoa ya Kigoma na Shinyanga. Watumishi wa serikali wakihamishiwa huku wanaenda kwa viboko.
 
Ukitaka kujua MAWAZIRI wa NCHI hii wana nguvu kiasi gani someni tena sakata la RICHMOND.
 
Ukitaka kujua MAWAZIRI wa NCHI hii wana nguvu kiasi gani someni tena sakata la RICHMOND.

MMJJ atakubali kuwa hao walikuwa na nguvu lakini Mramba mhh! mhh! Anakaugonjwa kake kanakohitaji tiba.
 
Kungurumweupe,

..nashukuru tena kwa ufafanuzi wako kuhusu haya madai ya ujambazi yanayohusisha Wachaga.

..je, habari za mitaani zinahusisha ujambazi na jamii nyingine yoyote Tanzania, au ni Wachaga peke yao?

..sasa labda huo ni upande mmoja wa shilingi, kwa upande mwingine kuna habari za mitaani zinazohusisha sifa yeyote nzuri na Wachaga?

Kubwajinga,

..ujenzi wa barabara ya kusini umeanza wakati wa Raisi Mwinyi, na Waziri Kiula.

..off course kilio cha barabara ya kusini ni cha muda mrefu na ndiyo maana ujenzi wake ukaanza kabla ya ujenzi wa barabara za Tarakea,Marangu,Rombo.

..ninavyoelewa mimi barabara ya kusini siyo ndefu kama hizi nyingine isipokuwa ujenzi wake ni mgumu na wa gharama kubwa kutokana na nature of the terrain it is passing thr'.

..ugumu wa ujenzi wa barabara ya kusini na ukubwa wa gharama ndiyo umesababisha wafadhili wengi wasite kutusaidia. serikali ilibidi ifanye kazi ya ziada mpaka kuwapata Saudi na Kuwait Fund, lakini hawa "wafadhili tuliowazoea" walikuwa wagumu kuwashawishi kutoa msaada.

Mkuu JokaKuu,

Kuhusu 'sifa nzuri' niliyowahi kuisikia ni kwamba, wao wana UPENDO sana kwa mtu yeyote wanayemjuwa kwa kina na hasa kwa yule mtu ambaye anatokea maeneo ya kwao, bila kujali familiya au ukoo anaotoka!

Kwa mfano, kama mimi ni wa ukoo wa MWAKASUNGURA au MWAKAPESA basi 'nitajitahidi' kwa hali yoyote ile niwe na UPENDO wa hali na mali kwa mtu yeyote anayetoka UKOO wa MWAKAJINGA au MWAKAFUKARA.

Swali: Mkuu JokaKuu, mbona unamtetea sana huyu mrambo na useri yake?! Kwani unaubia naye?! Unaifahamu vizuri funding process ya hiyo barabara ya USERI??!!
 
Ukitaka kujua MAWAZIRI wa NCHI hii wana nguvu kiasi gani someni tena sakata la RICHMOND.

Nafikiri si RICHMOND tu. Walipomwambia Mramba asinunue NDEGE ya Rais kwani ni pesa nyingi sanaa, alijibu vipi? Ila wakati huo huo wao wanakusanya pia 10% za Rada na Ndege.
Seleli alikuwa analalamika kuwa Mwaka jana, "kaka yake" Spika Sita alimwambia "Bwana mdogo hili lalamiko la Barabara Tabora liache hadi mwakani.." Mwaka huu kapigwa tena goli jingine akaona ujinga huu. Kalalamika ila sijui yameishaje. Mie nashindwa kuelewa hivi siku zote wanasema mto atatoa Shillingi hadi kieleweke ila huwa yanaisha hivihivi. Hivi hii ndiyo hua inaishia mtu kupelekwa Chemba? Huko kunatokea nini? Mmoja sijui nani KAMZILIA Waziri barabara maana anasema hata tembo hawawezi kuvuka hayo Mahandiki.
Nafikiri MMK hili la kusema SHERIA kwa Mawaziri kidogo unatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kuwa "ETI Wanafuata sheria." Miaka ya 80 Wapare wa MWanga walikuwa wakijivuna OPENLY jinsi Msuya anavyofanya mavituz huko na kuwa Majimbo mengine TULIE TU.

Mramba alisema "Ikibidi kula nyasi na mle, ila ndege itanunuliwa."
Malecela alisema " Wanaosema Tanzania kuna shida ya usafiri they can go to hell.." Kweli, sisi huku Sikonge/Tabora, Kigoma tuko HELL.
 
A MODEST PROPOSAL

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna vumbi la chuki, fitina, wivu, kisasi, na hisia za kibaguzi dhidi ya jamii ya Wachagga nchini. Kuna kila dalili kuwa jamii ya Wachagga nchini siyo tu inaanza kutengwa lakini uwepo wake katika nafasi mbalimbali za uongozi inazua hoja ya ukabila kwa haraka zaidi yawezekana kuliko kabila jingine lolote nchini. Katika Tanzania yetu, wachagga wameanza kunyoshewa kidole siyo kwa siri tena bali kwa wazi kabisa tena na watu ambao wakati mwingine hawapati hata kigugumizi.

Ubaguzi huo msingi wake mkubwa ni idadi ya wachagga katika nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kuhusiana na elimu yao. Kuanzia mara tu baada ya uhuru jamii ya wachagga mojawapo ya jamii ambayo watu wake wengi wamesoma sana na kufanikiwa kielimu na kiuchumi imekuwa ikinyoshewa kidole cha kupendelewa.

Mtu yeyote ambaye anaweza akafanya uchambuzi yakinifu hatoshangaa kukuta wataalamu wa kichagga katika nafasi mbalimbali za uongozi au taaluma nchini. Kwenye vyuo vikuu, kwenye idara za serikali na hata kwenye taasisi binafsi kumejaa watu wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hususan watu wa jamii ya Kichagga.

Endapo itatangazwa nafasi yoyote ya kitaalamu usishangazwe ukiona kuwa waombaji wengi wana majina ya "Kichagga".

Ni kwa sababu hiyo basi kuna kila dalili kuwa kutokana na wingi wao katika nafasi muhimu na vyeo mbalimbali (hata ndani ya Jeshi la Polisi) Wachagga siyo tu ni wengi lakini wanaonekana kufanikiwa zaidi. Hili ni tishio kwa baadhi ya watu. Ni tishio kwa watu ambao hawako tayari kuangalia jitihada za watu katika kufanikiwa kwao na matokeo yake kushutumu ukabila kila idadi ya Wachagga kwenye kitengo fulani inazidi mmoja.

Ushauri wangu ni kuwa, kwa vile Wachagga wameshasoma sana na kuendelea katika biashara karibu mikoa mingi nchini. Na kwa vile wanaendelea kufanikiwa pia katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini, basi itakuwa vizuri kama watajitolea kuachilia nafasi hizo ili kuwapa nafasi watu wa makabila mengine.

Kwa vile ni wao wanaonekana kulalamikiwa kutokana na mambo ya kifisadi aidha kwa moja kwa moja au kwa kuashiria basi ni vizuri wawape watu wengine nafasi hizo hata kama watu hao hawajasoma sana. Hii yote itakuwa ni katika kudumisha mshikamano, umoja na udugu wa Taifa letu.

Endapo Wachagga wataachilia nafasi mbalimbali kama UCEO, Ukurugenzi, Ukuu wa Idara n.k watasababisha watu wawapende na kuwakubali kuwa ni wazalendo wa kweli. Sitoshangaa kuwa ndugu zetu wa Jamii ya Kichagga wakikaa pembeni, basi ufisadi utakoma serikalini, idara zitaongozwa na watu wazuri, na mara moja na daima Tanzania itaanza kukua katika uongozi.

Kwa kupendekeza nashauri wabunge wote ambao ni Wachagga au wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro kuachia ngazi mara moja ili watu wa makabila mengine wapewe nafasi hizo. Siyo wao tu bali pia wabunge ambao wameoa au kuolewa uchagani vile vile wafuate nyazo hizo.

Wakishamaliza hao, wakuu wote wa idara za serikali ambao wana asili ya mkoa wa Kilimanjaro na hasa wa jamii ya kichagga (wamarangu, wamachame, wa Rombo, na wa Kibosho) na wao waamue kuachilia nafasi hizo kwa ndugu zao Wamakua, Wamwera, Wa Ndali, Wadigo n.k Katika hili Wapare hawahusishwi.

Tukishamaliza wakuu hao wa idara za serikali ningependekeza madaktari wote wenye kumiliki hospitali binafsi ambao ni wachagga au wameoa/kuolewa uchagani na wenyewe waamue kuingia ubia na watu wa makabila mengine kama wangengereko, wambuu, na wanjiro ili hayo makabila madogo na wenyewe wapate nafasi ya kujifunza fani hizi muhimu.

Zaidi ya yote, majaji na mahakimu wote ambao wana asili ya Uchaggani na wenyewe waamue kujitoa katika nafasi hizo kwani wingi wao pia unaonekana sana na hivyo kuwa kikwako kwa watu wa makabila mengine kufanikiwa zaidi katika nyanja ya sheria. Kwanza kabisa wale majaji wa Kichagga wa mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu wawe wa kwanza kuweka manyanga chini.

Katika kufanya hivyo jamii ya Watanzania ambao inaona ukabila wa wachagga katika sehemu nyingi itaridhika kwani kwa mara ya kwanza tutakuwa tumeshughulikia chanzo cha matatizo yetu mengi.
Mwanakijiji!
Naomba nikuunge mkono katika wala hili, na wakati huo huo naomba nikupinge katika hojahiyo ya Wachaga!
1. Swala la viongozi kuwa wezi halina uhusiano sana na ukabila bali maadili mabovu ya viongozi yanayo tokana na kutokuwa na "accountability" katika utendaji wa serikali ( Management structure). Kwa watu wataalamu wa mambo ya utendaji wanajua kunakitu kinaitwa "controls" ambazo lazima ziwepo kilamaali katika mashirika binafsi na hata serikali. Mfano mzuri watu waliochukua pesa za EPA hawakujua kama "control measures" zingechukulia kukagua mahesabu.
2. Swala la wachaga kufanikiwa lina mambo mengi kuliko ulivyo liangalia, Mfano; Kila mwezi wa Kuminambili wakati wa Krismas, wachaga huwa wanarudi nyumbani kusalimu wazee, ndugu jamaa na marafiki. Wanapo fika nyumbani kwao (kijijini), mwnaume hujigamba na kuonyesha nijinsi gani alivyo fanikiwa kimaisha, na jinsi alivyo tunza familia yake, mke lazima awe amenawiri (mduara) na watoto wawe kwenye afya njema. Ndio maana watafanya kilaaina ya biashara kuhakikisha kwamba watafanikiwa ili wakirudi nyumbani wenzao wasiwacheke.
3. Kuhusu ukabila katika nafasi za kazi liko kila mahali. Wahaya wameshalaumiwa sana kutokana na swala hilo. Ukienda jeshini, watu wa kanda ya ziwa wakua "Synonymous " na neno afande nadhani hata wewe unajua hilo. Kwahiyo hilo swala lipo katika makabila yote.
4. Swala la wabunge kupendelea watu wao halina tatizo. Kumbuka wajubu wa wabunge ni kuwakilisha hoja na matakwa ya watu wanao wawakilisha. Kama leo mtu ata mlaumu mheshimiwa Cleopa Msuya kwa kuweka lami upareni na kujenga posta na shule nzuri, je si hivyo ndio vitu wabunge wanatakiwa kufanya kwa wanachi wao?
Swala nakuhakikishia sio ukabila. Watu wa pwani wako "layback" wakati Wachaga wako " aggressive" kwahiyo hili swala nadhanni inabidi liangaliwe kwa uangalifu zaidi.
Mbambo ya wizi kuzibitiwa ni rahisi kuliko watu wanavyo fikiri. Serikali inabidi kubadili utendaji wa sekta zake zote, kuweka "control systems and implement computerized accounting". Kufukuza watu wanao iba. Kuna watuwengi wanaoweza kuziba nafasi zao, maana watu wana bidi wajue kwamba anaweza kuondolewa wakati wowote. That is the only way forward.
Swala la ukabila jamani naomba tuwe very careful tunapo lizungumzia.
 
Yeap, there you go hapa umenena (am refering to the above paragraph), kama hao wachagga wanapendeleana katika mashirika ya umma na serikalini, hebu Mkjj na supporter wengine mjibu swali lililoulizwa hapo juu, nanukuu sehemu hii "how do you explain dominance ya hawa wenzetu kwenye international orgs kama UN etc...." ninasubiri majibu ya wakereketwa ili nijue siri ya hawa wachagga.
All the best.

Tonga,
Thanks for raising y0ur voice on this maana nimeuliza zaidi ya mara tatu in different posts lakini hakuna aliyejibu....
It will be interesting to hear what people have to say..esp tha anti-chaggas
[/QUOTE]

Wakuu wote,

Ikumbukwe kuwa, UPENDELEO wa makusudi hauko ndani ya tz pekee. Hata nje ya mipaka ya tz, kama vile ulaya na marekani huwa kuna UPENDELEO wa KIJINGA kama huo!

Kwamfano, miaka michache iliyopita DUNIA ilishuhudia UPENDELEO wa KIJINGA na wa-MAKUSUDI uliofanywa na KIONGOZI au MKUU mmoja wa taasisi kubwa ya KIFEDHA duniani. Aliyefaidika na UPENDELEO huo ni mwana-mama mmoja aliyekuwa na UHUSIANO wa KIMAPENZI na huyo kiongozi husika.

Ni ukweli uliowazi kwamba, mashirika ya kijamii ya ndani(local NGOs) au ya kimataifa(international NGOs) hayawezi kuanza operations zake zozote zile ndani ya tz bila mawasiliano yoyote yale kati yake na serikali yetu kupitia idara au taasisi yoyote ile ambayo kwa njia moja au nyingine inahusika ama kisheria au kimasilahi katika swala zina la jamii husika juu ya ile huduma inayotolewa au itakayotolewa na hiyo NGO, be it national(local), international or multinational.

For that case , therefore, wachaga wengi wanaoshikilia nafasi kubwa kubwa ama za kiutawala ua za kiuongozi katika asasi na taasisi mbalimbali za kijamii na serikali ya tz, huwa wakwanza kupata au kusikia fununu au habari za ukweli na za ndani kuhusu kazi ndani ya hizo NGOs za kimataifa, kisha "hujitahidi" ama kwa makusudi au kwa kulazimika, kuzifikisha kwa wale wanaotaka kuwapendelea. Ikibidi, hutumia influence yao kuhakikisha kuwa hizo nafasi zinakaliwa na watu wao. Hawa watu(viongozi wa ...) hufanya connection hizi na marafiki zao ama weusi au weupe walioko ndani na nje ya tz na hasa wale ambao tayari wamo kwenye mtandao huo wa kiupendeleo wa kimataifa.

Wale bongolala msiolijua hili, AMKENI kumekucha!
 
Tonga,
Thanks for raising y0ur voice on this maana nimeuliza zaidi ya mara tatu in different posts lakini hakuna aliyejibu....
It will be interesting to hear what people have to say..esp tha anti-chaggas

Wakuu wote,

Ikumbukwe kuwa, UPENDELEO wa makusudi hauko ndani ya tz pekee. Hata nje ya mipaka ya tz, kama vile ulaya na marekani huwa kuna UPENDELEO wa KIJINGA kama huo!

Kwamfano, miaka michache iliyopita DUNIA ilishuhudia UPENDELEO wa KIJINGA na wa-MAKUSUDI uliofanywa na KIONGOZI au MKUU mmoja wa taasisi kubwa ya KIFEDHA duniani. Aliyefaidika na UPENDELEO huo ni mwana-mama mmoja aliyekuwa na UHUSIANO wa KIMAPENZI na huyo kiongozi husika.

Ni ukweli uliowazi kwamba, mashirika ya kijamii ya ndani(local NGOs) au ya kimataifa(international NGOs) hayawezi kuanza operations zake zozote zile ndani ya tz bila mawasiliano yoyote yale kati yake na serikali yetu kupitia idara au taasisi [/Byoyote ile ambayo kwa njia moja au nyingine inahusika ama wa kisheria au kimasilahi katika swala zina la jamii husika juu ya ile huduma inayotolewa au itakayotolewa na hiyo NGO, be it national(local), international or multinational.

For that case , therefore, wachaga wengi wanaoshikilia nafasi kubwa kubwa ama za kiutawala ua za kiuongozi katika asasi na taasisi mbalimbali za kijamii na serikali ya tz, huwa wakwanza kupata au kusikia fununu au habari za ukweli na za ndani kuhusu kazi ndani ya hizo NGOs za kimataifa, kisha "hujitahidi" ama kwa makusudi au kwa kulazimika, kuzifikisha kwa wale wanaotaka kuwapendelea. Ikibidi, hutumia influency yao kuhakikisha kuwa hizo nafasi zinakaliwa na watu wao. Hawa watu hufanya connection hizi na marafiki zao ama weusi au weupe walioko ndani na nje ya tz na hasa wale ambao tayari wamo kwenye mtandao huo wa kiupendeleo wa kimataifa.

Wale bongolala msiolijua hili AMKENI kumekucha![/QUOTE]

Hii discussion nilidhani imekwisha..kumbe inaendelea!
Basi hao wachaga ni kiboko..wako influential kiasi hicho ilhali wao ni kabila dogo tu! Na je how do you explain professional positions ambazo hutangazwa na watu wakaapply..achilia mbali hizo za kuuliziwa..( do your homework properly!)
Nitakupa hint uanzie wapi... kama uko Bongo... nenda kaulizie mfano UNDP,ILO,WORLD BANK,MCC etc na taasis nyingine ambapo kazi hazigawiwi kama pipi au sadakalawe! na kazi zote hizo zimetangazwa magazetini na watu wakaaplytataizo watu wamekalia kusoma magazetu ya udaku na siyo serious newspapers kama the Guardian, Daily News, Economist etc.
 
Wakuu wote,

Ikumbukwe kuwa, UPENDELEO wa makusudi hauko ndani ya tz pekee. Hata nje ya mipaka ya tz, kama vile ulaya na marekani huwa kuna UPENDELEO wa KIJINGA kama huo!

Kwamfano, miaka michache iliyopita DUNIA ilishuhudia UPENDELEO wa KIJINGA na wa-MAKUSUDI uliofanywa na KIONGOZI au MKUU mmoja wa taasisi kubwa ya KIFEDHA duniani. Aliyefaidika na UPENDELEO huo ni mwana-mama mmoja aliyekuwa na UHUSIANO wa KIMAPENZI na huyo kiongozi husika.

Ni ukweli uliowazi kwamba, mashirika ya kijamii ya ndani(local NGOs) au ya kimataifa(international NGOs) hayawezi kuanza operations zake zozote zile ndani ya tz bila mawasiliano yoyote yale kati yake na serikali yetu kupitia idara au taasisi [/Byoyote ile ambayo kwa njia moja au nyingine inahusika ama wa kisheria au kimasilahi katika swala zina la jamii husika juu ya ile huduma inayotolewa au itakayotolewa na hiyo NGO, be it national(local), international or multinational.

For that case , therefore, wachaga wengi wanaoshikilia nafasi kubwa kubwa ama za kiutawala ua za kiuongozi katika asasi na taasisi mbalimbali za kijamii na serikali ya tz, huwa wakwanza kupata au kusikia fununu au habari za ukweli na za ndani kuhusu kazi ndani ya hizo NGOs za kimataifa, kisha "hujitahidi" ama kwa makusudi au kwa kulazimika, kuzifikisha kwa wale wanaotaka kuwapendelea. Ikibidi, hutumia influency yao kuhakikisha kuwa hizo nafasi zinakaliwa na watu wao. Hawa watu hufanya connection hizi na marafiki zao ama weusi au weupe walioko ndani na nje ya tz na hasa wale ambao tayari wamo kwenye mtandao huo wa kiupendeleo wa kimataifa.

Wale bongolala msiolijua hili AMKENI kumekucha!

Hii discussion nilidhani imekwisha..kumbe inaendelea!
Basi hao wachaga ni kiboko..wako influential kiasi hicho ilhali wao ni kabila dogo tu! Na je how do you explain professional positions ambazo hutangazwa na watu wakaapply..achilia mbali hizo za kuuliziwa..( do your homework properly!)
Nitakupa hint uanzie wapi... kama uko Bongo... nenda kaulizie mfano UNDP,ILO,WORLD BANK,MCC etc na taasis nyingine ambapo kazi hazigawiwi kama pipi au sadakalawe! na kazi zote hizo zimetangazwa magazetini na watu wakaaplytataizo watu wamekalia kusoma magazetu ya udaku na siyo serious newspapers kama the Guardian, Daily News, Economist etc
.[/QUOTE]

Mkuu,

JOB ADVERTISEMENT ON YOUR Tz-NEWSPAPER IS JUST A FORMALITY! KAMA HULIJUI HILO POLE SANA!

For more factual information, please, give me time. I am doing my Reseach!
 
Hii discussion nilidhani imekwisha..kumbe inaendelea!
Basi hao wachaga ni kiboko..wako influential kiasi hicho ilhali wao ni kabila dogo tu! Na je how do you explain professional positions ambazo hutangazwa na watu wakaapply..achilia mbali hizo za kuuliziwa..( do your homework properly!)
Nitakupa hint uanzie wapi... kama uko Bongo... nenda kaulizie mfano UNDP,ILO,WORLD BANK,MCC etc na taasis nyingine ambapo kazi hazigawiwi kama pipi au sadakalawe! na kazi zote hizo zimetangazwa magazetini na watu wakaaplytataizo watu wamekalia kusoma magazetu ya udaku na siyo serious newspapers kama the Guardian, Daily News, Economist etc
.

Mkuu,

JOB ADVERTISEMENT ON YOUR Tz-NEWSPAPER IS JUST A FORMALITY! KAMA HULIJUI HILO POLE SANA!

For more factual information, please, give me time. I am doing my Reseach![/QUOTE]

Umenipa pole..sina budi kuipokea ila nimeshangaa kidogo maana mpaka nimesema nilichosema..sio kuwa im talking from the abstract..
Ila I wish you luck kwenye utafiti wako..ukikwama uombe tukupe msaada...

Mawazo ya kuwa job adverts ni formalities hata mie kuna kipindi nilikuwa na mawazo kama hayo.Hii ilinikosesha opportunities nyingi.Nilipoamua kuwa objective na kuanza ku compete na wengine...the story changed na ndio maana nashangaa mnavyowabeza wachagga! Jamani ingieni kwenye ushindani na muache majungu... mtaona kwamba hizi kufikirika na kusadikika hazipo tena..at least kwenye ulimwenguni wa ushindani wa kimataifa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom