Je, vipofu huota ndoto?

Je, vipofu huota ndoto?

Haya Uzi ufungwe
Screenshot_20240101-120422.png
 
Hahahahahaha mkuu,
Ukiwaona wakipita utahisi wapo wapo tu. Ila ukikaa nao,kwa karibu,utagundua kuna watu wenye macho,lakini hata akili zao hazifikii za hawa unaoulizia.
Binafsi nilichogundua,sehemu ya macho,walipewa sensi nyingine na inafanya kazi. Kwani unadhani mfano ukiingia ndani bila kubisha hodi haelewi kwamba kuna mtu kaingia?
Wapo vizuri sana. Wanasoma,yupo mmoja ana PHD. Sasa kwenye ndoto,huongea na watu,husimuliwa na wanavutaga picha ya simulizi. Kwa hiyo,kasoro tu macho,maisha mengine ni kama ya watu wa kawaida. Japo hawa viumbe hasa walioelimika,ni wabaguzi sana. Kama huna tatizo kama lao,kukuamini ni ngumu. Jiulize inapofikia hatua ya kuoana wao kwa wao
Kwa tulio soma na hawa watu they are very special añaweza kujua huyu
Nani kwa kushika mkono tu darasa la watu 160
 
Ndio lakini huwezi uliza maswali ya kitoto kama haya...upofu unaishia kwenye macho tu jamani
Usiyaite ya kitoto,kwa sababu kuuliza kwake ni kwamba hana maarifa. Wengi wetu hujiuliza vitu kama hivo. Ni mfano wa mtu anaeamini kwamba akiiba,akachomoa laini kwenye simu na kutupa,atakuwa amemaliza.
Kikubwa tu ni kwamba mpaka anauliza,ujue amekaa nalo mda sana. Watu wengi akimuona kipofu kwanza kabisa anamuona kama omba omba. Je,ni kwamba hawapo wenye uwezo mkubwa kuwazidi wenye macho?
 
Kwa tulio soma na hawa watu they are very special añaweza kujua huyu
Nani kwa kushika mkono tu darasa la watu 160
Ndo maana nimesema kama hujakaa nao,ni ngumu kuwaelewa,ila wewe fumba macho,mguse tu mama yako mzazi,tuone kama utamtambua.

Na kama unataka kujua binadamu alivyo kiumbe wa ajabu, tafuta viziwi waiosikia na kuongea,na waweke sehemu moja, af uangalie watakavyopiga sitori au kukuteta. Ndo utajua hujuiii
 
Tutawapata wapi au ccbrt
Sijajua kwa mawasiliano ya kiswahili,
Ndiyo maana waliosoma wengi utakuta wana simu za Iphone. Kuna program zao, hutafsiri maandishi kwa sauti. Na kukujibu,ataandika kiswahili kwa sababu kila herufi anayotaka kuandika sauti husikika. Kwa asiejua,atajiuliza anachatije huyu!
Ila,bahato mbaya ikutokee uchungulie simu yake wakati anachat! Nadhani itakuwa mara yako ya mwisho kuchungulia. Hakika hata humu wamo,ila mpaka akubali kuongea,lazima apelekwe taratibu.
 
Yes kwanza ukiwa unaota macho na masikio yako huwa hayafanyi kazi wakati huo unaweza kuota umekufa au upo vitani na kadhalika vitu ambavyo hujawahi hata kuviona au unaota unapaa na kadhalika thats brain sio macho au masikio
Kwani ndoto inatengenezwa kwenye Ubongo au Akili?
 
Wapo humu, wataleta tu ufafanuzi tuongeze Maarifa.

Pia ikiwa Kuna member humu anaishi na kipofu wa tangu Kuzaliwa asaidie kumhoji na kuleta majibu.
Ni kama vitu gani unatamani kujua kwao labda mkuu? Ninavyojua ntakuelewesha haina shida. Japo nina imani najua karibia 95%
 
Ni kama vitu gani unatamani kujua kwao labda mkuu? Ninavyojua ntakuelewesha haina shida. Japo nina imani najua karibia 95%
Nataka kujua ikiwa kipofu anaota ndoto au la!!

Na ikiwa aota ndoto, ni za aina Gani?

Yaani nataka kujua ikiwa anaota ndoto, anatumia mfumo upi, ni tofauti kiasi Gani na mfumo wetu?

Maana WANADAMU sometimes huota vitu ambavyo kamwe hatujawahi kuviona duniani, so na vipofu ni hivyo hivyo?
 
Unajua nini darcity , kwa mtu asiewaelewa ni haki kuwaza wanaishije.
Tofauti na watu wenye macho, ni kwamba kila kitu huwachukua mda kukamilisha. Wanafua nguo, wanadeki,wanapika balaa. Humenya viazi mwenyewe,atawasha jiko au gesi,atapika na atakupakulia.
-Humimina maji kwenye glass na hamwagi
-Huweza kutambua rangi ya nguo anayoenda kuvaa(anakuwa ameshakalili,ila ukimpa nguo yake atakwambia ina rangi gani)
Hapo ndio utaamini uwezo wa Muumba.
 
Nataka kujua ikiwa kipofu anaota ndoto au la!!

Na ikiwa aota ndoto, ni za aina Gani?

Yaani nataka kujua ikiwa anaota ndoto, anatumia mfumo upi, ni tofauti kiasi Gani na mfumo wetu?

Maana WANADAMU sometimes huota vitu ambavyo kamwe hatujawahi kuvionya duniani, so na vipofu ni hivyo hivyo?
Kwanza uelewe kitu kimoja. Hao watu walio wengi na walioweza kuelimika,hawana shida na kuwa na macho. Kwa sababu,walishakubaliana na hiho hali,na hawawezi kutamani kitu ambacho hakitakaa kiwezekane katika maisha yao.
Sasa basi,
Wao watakwambia kwamba macho mliyo nayo nyie,ni ya kuona tu vitu vya ovyo hayana umhimu kwenu.
Nakupa mfano wa wazinzi. Mtu akitembea na mwanamke/mwanaume,hawezi kumuota siku hiyo. Ila akimtamani,huweza kumuota. Na wakati mwingine,ataota tu anatongozwa/za, na kugegedana,lakini sura ya aliyemgegeda kamwe haijui.
Sasa,hapo ndo utajua ndoto si picha ya kitu ulichokiona. Bali ni ubongo kurudia matukio ya mda flani ukiwa bize na kuwaza.
Unaweza ukaota demu/mwanaume uliyemuona. Uwezo ulio nao wa kuchagua mwenza, hata wao wanao. Unajua inakuwaje? Wana watu wa karibu. Atakuuliza ulivyomuona,alivyokua amevaa(kama ni kachumbali au kama yuko smart). Kimuonekano. Na yeye atavuta hiyo picha ndo itakayomkaa akilini.
Sasa majibu yako:
1. Ndio, kipofu huota ndoto
2. Aina ya ndoto zao,ni sawa na za kwako. Hapa kwanza,wewe elewa kwamba tofauti yako na yeye ni macho tu.
3. Mfumo wao wa ndoto, ni sawa na mfumo wetu tunaoona.

Si kweli kwamba ndoto ni vitu ambavyo hujawahi viona. Ni mchanganyiko wa maisha tunayoishi. Jiulize mfano gaidi anaota ndoto gani. Kahaba anaota ndoto gani.
Si kuna wakati unaweza jikuta una uoga bila sababu! Hasa kama kuna kitu kimetokea lakini bado hujapewa taarifa? Lakini nafsi itakusumbua na utakosa amani! Na wao ni hivyo hivyo.
Kwanza kuna kitu unaweza kushangaa. Mchanganyie milioni moja ya noti tofauti tofauti. Af muulize ni kiasi gani. Amepewa uwezo wa kujua noti kwa kuigusa tuu.
Kwa waliosona, wana apps ya kuhesabia pesa.
Kwa kifupi, maisha yao ni sawa na yetu. Tofauti tu ni watu ambao wapo makini sana kwa kila kitu
 
Kwani ndoto inatengenezwa kwenye Ubongo au Akili?
Sasa akili inatoka kwenye ubongo ndio maana ubongo ukifa na mtu kisayansi anakuwa amekufa brain controls everything movement hisia na kadhalika
 
Back
Top Bottom