Je, Vyoo vya Shule za Serikali vinajengwa hivi?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Haya ndio mafanikio ya sera ya Force Account ya Awamu ya Tano.
Kila mtu anaruhusiwa kutotumia akili, toka kwa Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, ma DED wa Halmashauri.

Ila wanatakiwa wamuamini fundi Maiko, na hapo kafanya vitu vyake.
 
Inasikitisha sana. Ina maana tozo tunazolipa ndiyo zinatumika hovyo kiasi hicho??!!
 
Tena hiyo imejengwa na mkandarasi chini ya usimamizi wa mhandisi mwenye Phd
 
Mara mia wangekuwa wanatupa kwenye hiyo miradi vijana waliomaliza vyuoni wamehitimu mambo ya ujenzi ingesaidia sana kuliko huo upuuzi...

Kazi za force account n KIAZI CHA MOTO kwa serikali
 
Bongo kila mtu msemaji kaka....
Kiukweli force account ni upuuzi
 
Mkuu wewe unsona septic tank pale?
 
Tatizo siyo kufukia pekee. Hakuna chemba ndogo za kupokea mzigo na kuunganisha kwenye chemba kubwa. Hapo harufu itawasumbua sana na ikitokea kumeziba sijui watayakata hayo mabomba kuzibua na kuyaunga tena?

Mitano tena kwa mkandarasi
Kuna jambo hujalijua ila inajifanya kujua swala la ujenzi waachieni wajenzi wao ndio wanajua kwa mazungira yapi kijengwe nini.
 
Naomba kujua hii shule gani na ipo mkoa gani na wilaya gani.
 
Hivi kweli hata kama hujui kusoma hata picha huioni< hao unaowatetea wanaweza kujenga vyoo vya namna hiyo majumbani kwao? Je huyo Mkandarasi na mafundi wake hawaoni hata aibu kwa kitendo hicho?
 
Waziri Ummy na DED wa hiyo Wilaya tunaomba maelezo..

Hata hivyo tunamshukuru uhuru wa kutoa maoni na kuibua uozo maana awamu ya Mwendazake ulikuwa marufuku kuonyesha madhaifu ya serikali bali sifa za bwana Magu kiongozi wa malaika na wanyonge.
Wanafunzi wanakua na kuona utendaji wa kazi wa namna hii unadhani unawajengea utamaduni gani
Mambo kama haya tena shuleni ndio baadae tunaendelea kupata viongozi wanaojijali wao tu
 
Kuna jambo hujalijua ila inajifanya kujua swala la ujenzi waachieni wajenzi wao ndio wanajua kwa mazungira yapi kijengwe nini.
Receiving mini-chamber ina umuhimu mkubwa sana kwa sewarge system yeyote.

Mimi siyo mtaalam wa ujenzi lakini kwa kuangalia tu hapo wamemchukua fundi gereji kufanya huo ujenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…