Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?

Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi.

Utambulisho.

Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, yaani freelance journalist, hatutumwi na mtu yoyote au media yoyote. Sisi waandishi tuko wa aina nyingi na tunafanya kazi za aina nyingi, wengine ni maripota, wengine watangazaji, wengine wahariri, na ndani ya makundi hayo, kuna baadhi yetu, kazi yetu ni kuuliza tuu, hivyo hiki ndicho ninachokifanya kwenye bandiko hili, nauliza tu: Je, Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau? Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule? Likibariki, Karma Itawatafuna!
  1. Vyama vyote vya siasa nchini, vinavyolipwa na ruzuku ya serikali, ni public parties, sio private parties za viongozi na wanachama. Kwa Public Party, paid by taxpayers money, the public has the right to know its conduct, public as private, including its leaders wana surrender, some of their right to privacy. Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!
  2. Hivyo mtu yoyote asiye Chadema, ana haki ya kuzungumzia jambo lolote kuihusu Chadema, na ndio naitumia haki hii kuishauri Chadema, ushauri wa bure CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani!, S'times the devils does good deeds!.
  3. Chadema kama chama cha siasa kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria, na kinapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni. Hivyo Chadema pia kina katiba yake, na katiba hiyo imeweka taratibu za nidhamu. Kwanini Chadema haifuati katiba yao?. Elections 2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!
  4. Pamoja na Chadema kuwa na katiba yake, yenye taratibu za nidhani, katika fukuza fukuza zote za wanachama wa Chadema, CC ya Chadema, huwa inakaa kama a Kangaroo Court, bila kufuata katiba yake na mamlaka yake ya nidhamu, matokeo yake hutoa baadhi ya maamuzi kwa uonevu mkubwa.
  5. Haya ni baadhi ya maamuzi ya uonevu wa Chadema dhidhi ya wanachama wake Walianza na madiwani wa Arusha Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!" karma yake Chadema ikaparaganyika Arusha, uchaguzi uliofuta ikapigwa chini ubunge wa Arusha Mjini.
  6. Wakaja kwa kina Shonza Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015! Wote waliopigwa chini, karma ikawafidia, wakaula CCM wengine ni wabunge, mawaziri etc.
  7. Wakaja kwa Zitto Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!" angalia jinsi karma ilivyowatandika watesi wa Zitto!, angalia sasa Zitto alivyofidiwa na karma!.
  8. Kitila Mkumbo ndio alikuwa think tank wao, wakamtimua!. kosa lake ni kuwaeleza ukweli kwenye ule waraka wa mabadiliko, Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani Makini? - Prof. Kitila Mkumbo, angalia jinsi karma ilivyomfidia Kitila, angalia Chadema ilivyonyauka!
  9. Funga Kazi ni kuwatimua mashujaa 19, walioipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu!. CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
  10. Baraza Kuu likibariki Ukangaroo wa CC ya Chadema... Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu karma yake itakuwa ni hatari tupu!.
  11. Matokeo ya maonevu hayo, baadhi ya wale walioonewa, karma iliwafidia, leo wako vizuri zaidi kuko walivyokuwa wanapauka tuu Chadema. Angalia wote waliotimuliwa Chadema walipo sasa, na angalia viongozi wa makamanda wa Chadema kilichowakuta!. Usikute hata baadhi ya madhila yanayowakuta viongozi wa Chadema ni karma ya matendo Yao.
  12. Lakini Chadema nacho kama chama, kimekuwa kikiadhibiwa kwa bakora za karma, kwanza kwa kukitandika chama kama chama, na kuwatandika viongozi wake, individually kutoka na their roles kwenye dhulma na maonevu hayo, hivyo Chadema kikaanza kunyauka kwa kukimbiwa Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?
  13. Kuna hoja kuwa baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema wako kama nyumbu, hufuata kila kinachofanywa na viongozi wao. Kikao cha CC kilichokaa na kuwafuta uanachama wanachama wake 19, kilikaa kama a Kangaroo court na kutoa maamuzi ya maonevu kwa kuwaonea.
  14. Sasa kwa vile naamini, wajumbe wa Baraza Kuu, hawawezi na wao wote kuwa ni manyumbu, kubariki maamuzi ya ile Kangoroo Court ya Chadema. Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
  15. Hivyo hili ni bandiko la swali "Je Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau?. Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule?. Likibariki, Karma Itawatafuna!"
Nawatakia wana Chadema, kikao chema cha Baraza Kuu.

Paskali
 
Yaani huwa najiuliza kuwa huyu Pascal alisoma kweli Ilboru sekondari au alikuwa msoma magazeti? Hata Mimi niliyesoma shule ya kayumba najua mbivu na mbichi Sasa huyu mchumia tumbo anakuwaje jinga kiasi hiki.

Pascal ni janga la kitaifa yaani tukiwa na wachumia tumbo Kama hawa hta wakiwa wawili ni hatari kwa usalama wetu.

Pascal anatafuta uteuzi kwa damu za watu na ni mzandiki shetani kuliko hata Ibilisi.
 
CHADEMA kinapaswa kujenga taswira chanya kwa jamii. Pamoja na mambo mengine political branding ya chama cha siasa inajengwa na udihibiti wake katika misimamo na maamuzi yake. Hakuna jinai yoyote Kutowafukuza wabunge 19 kama walingia kinyume cha utaratibu ni uvunjivu wa katiba ya chama.

Kwa kuwa umeshasema CHADEMA ni public party paid by taxpayers ungehoji vilevile ilikuwa halali wabunge wale 19 kutumia pesa za umma? Je ilikuwa halali kufoji nyaraka za chama? Na ilikuwa sahihi kwa bunge chini ya Ndugai kuwalipa fedha za umma? Bila hivyo unaweza kuitwa mchambuzi kanjanja tu kutafuta maslahi yako binafsi.
 
Hivi ni nani mwenye nguvu ya kumtoa mtu aliendani gerezani usiku usiku na kesho yake akaapishwa kua ni mbunge?!! Tena wakaapishiwa garage, sio ndani ya ukumbi wa bunge!!

Yaani CHADEMA ipeleke jina la mtu ambae yuko gerezani zaidi ya miezi miwili na imtoe usiku?!!

Ifike sehemu tuache unafiki na uhuni!!
 
Mkuu Pascal Mayalla

Umekuwa unazunguka sana kuhusu Wabunge 19 kiasi cha kujiuliza kulikoni!

Unaonyesha kuna Kangaroo court, hujaonyesha vifungu gani vimekiukwa

Unaelezea 'Karma' kama mwongozo wa chama badala ya katiba unayosema inakiukwa

Mwisho unauliza swali, je, ni kangaroo court?
Halafu una conclude kwa ? kabla ya jibu, ''Baraza kuu litabariki'

Kila mtu ana haki ya maoni, kwangu, kusimama na misingi ya chama iwe CCM, CDM etc ni kitu muhimu sana kuliko personality. Nilikataa wakati wa Maalim RIP na kila chama.

Hawa 19 ni Wasaliti,hawana Karma inayowalinda bali inayowawinda.

Watu wamepoteza damu, ni vilema n.k. wakipigania haki zao, hawa wanawasaliti kwa Ubunge wakishirikiana na Ndugai, Bushir etc.

Ni waovu na Wasaliti tu! Hawasafishiki mkuu Pasco

JokaKuu
 
Back
Top Bottom