Wanabodi.
Utambulisho.
Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, yaani freelance journalist, hatutumwi na mtu yoyote au media yoyote. Sisi waandishi tuko wa aina nyingi na tunafanya kazi za aina nyingi, wengine ni maripota, wengine watangazaji, wengine wahariri, na ndani ya makundi hayo, kuna baadhi yetu, kazi yetu ni kuuliza tuu, hivyo hiki ndicho ninachokifanya kwenye bandiko hili, nauliza tu: Je, Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau? Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule? Likibariki, Karma Itawatafuna!
- Vyama vyote vya siasa nchini, vinavyolipwa na ruzuku ya serikali, ni public parties, sio private parties za viongozi na wanachama. Kwa Public Party, paid by taxpayers money, the public has the right to know its conduct, public as private, including its leaders wana surrender, some of their right to privacy. Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!
- Hivyo mtu yoyote asiye Chadema, ana haki ya kuzungumzia jambo lolote kuihusu Chadema, na ndio naitumia haki hii kuishauri Chadema, ushauri wa bure CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani!, S'times the devils does good deeds!.
- Chadema kama chama cha siasa kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria, na kinapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni. Hivyo Chadema pia kina katiba yake, na katiba hiyo imeweka taratibu za nidhamu. Kwanini Chadema haifuati katiba yao?. Elections 2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!
- Pamoja na Chadema kuwa na katiba yake, yenye taratibu za nidhani, katika fukuza fukuza zote za wanachama wa Chadema, CC ya Chadema, huwa inakaa kama a Kangaroo Court, bila kufuata katiba yake na mamlaka yake ya nidhamu, matokeo yake hutoa baadhi ya maamuzi kwa uonevu mkubwa.
- Haya ni baadhi ya maamuzi ya uonevu wa Chadema dhidhi ya wanachama wake Walianza na madiwani wa Arusha Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!" karma yake Chadema ikaparaganyika Arusha, uchaguzi uliofuta ikapigwa chini ubunge wa Arusha Mjini.
- Wakaja kwa kina Shonza Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015! Wote waliopigwa chini, karma ikawafidia, wakaula CCM wengine ni wabunge, mawaziri etc.
- Wakaja kwa Zitto Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!" angalia jinsi karma ilivyowatandika watesi wa Zitto!, angalia sasa Zitto alivyofidiwa na karma!.
- Kitila Mkumbo ndio alikuwa think tank wao, wakamtimua!. kosa lake ni kuwaeleza ukweli kwenye ule waraka wa mabadiliko, Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani Makini? - Prof. Kitila Mkumbo, angalia jinsi karma ilivyomfidia Kitila, angalia Chadema ilivyonyauka!
- Funga Kazi ni kuwatimua mashujaa 19, walioipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu!. CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
- Baraza Kuu likibariki Ukangaroo wa CC ya Chadema... Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu karma yake itakuwa ni hatari tupu!.
- Matokeo ya maonevu hayo, baadhi ya wale walioonewa, karma iliwafidia, leo wako vizuri zaidi kuko walivyokuwa wanapauka tuu Chadema. Angalia wote waliotimuliwa Chadema walipo sasa, na angalia viongozi wa makamanda wa Chadema kilichowakuta!. Usikute hata baadhi ya madhila yanayowakuta viongozi wa Chadema ni karma ya matendo Yao.
- Lakini Chadema nacho kama chama, kimekuwa kikiadhibiwa kwa bakora za karma, kwanza kwa kukitandika chama kama chama, na kuwatandika viongozi wake, individually kutoka na their roles kwenye dhulma na maonevu hayo, hivyo Chadema kikaanza kunyauka kwa kukimbiwa Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?
- Kuna hoja kuwa baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema wako kama nyumbu, hufuata kila kinachofanywa na viongozi wao. Kikao cha CC kilichokaa na kuwafuta uanachama wanachama wake 19, kilikaa kama a Kangaroo court na kutoa maamuzi ya maonevu kwa kuwaonea.
- Sasa kwa vile naamini, wajumbe wa Baraza Kuu, hawawezi na wao wote kuwa ni manyumbu, kubariki maamuzi ya ile Kangoroo Court ya Chadema. Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
- Hivyo hili ni bandiko la swali "Je Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau?. Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule?. Likibariki, Karma Itawatafuna!"
Nawatakia wana Chadema, kikao chema cha Baraza Kuu.
Paskali
Leo hukumu imetoka
Nimeisoma hukumu, 1. Mahakama zetu zinarudia makosa yale yale ya ukosefu wa kutenda haki kwa sababu ya legal technicalities, kuwa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa kitu ambacho hakikuombwa!.
2. Wabunge hawa 19 wa Chadema, walivuliwa uanachama wao kinyume cha katiba ya JMT na kinyume cha haki kwa kutokusikilizwa, kinyume cha katiba ya Chadema kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni!.
3. Kikao cha CCM ya Chadema, kilichowatimua kilikaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kikangaroo!.
4. Katiba ya Chadema inasema mwanachama kabla hajafutwa uanachama, kwanza atatumiwa hati ya mashitaka kwa maandishi by despatch, kisha atapewa siku 14 za kujibu mashitaka. Chadema hawakuandaa hati zozote za mashitaka!. Hili Mahakama ilipaswa ilione!.
5. Baada ya watuhumiwa kupewa hati ya mashitaka, ndipo kikao cha CC kinaitishwa kama mamlaka ya nidhamu, kusoma majibu ya mashitaka, na ndipo kinawaita washikiwa na kuwasikiliza. Hili halikufanyika!.
6. Baada ya wabunge 19 wa Chadema kuapishwa, hapa Chadema waliposwa kufanya kitu kinachoitwa a due process ya nidhamu na sio zile Zimamoto za kikangaroo!. There was no emergency of whatsoever!. Mahakama ilipaswa ilione hili!.
7. Uthibitisho wa hakukuwa na any emergency ya kuitisha CC, ni the time taken, kuitisha kikao cha Baraza Kuu!.
8. Baada ya kuitishwa kikao cha Baraza Kuu, kitu cha kwanza kwa Baraza Kuu Chadema kuangalia ni uhalali wa kikao cha CC, pili jee katiba, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu ya Chadema zilifuatwa?.
8. CC ya Chadema ni mamlaka halali ya nidhamu ya wabunge wa Chadema, lakini CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha!, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu!, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?!. Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa hili kukuona!.
9. Japo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiliitishwa kihalali kama mamlaka ya rufaa ya wabunge wa Chadema, lakini kitendo cha kikao hicho kubariki uamuzi wa CC kuwatimua bila kufanya mapitio yoyote, ni uthibitisho wa Chadema bado ni chama kichanga, mfano kingechukua nchi ile 2015!, it would have been disastrous!.
10. Kitendo cha Baraza Kuu kubariki maamuzi ya kikangaroo ya CC ya Chadema, kilifanya niyaite maamuzi yale pia ni ya kikangaroo, na kitendo cha Mahakama Kuu kuyabari maamuzi ya kikangaroo, Mahakama Kuu yetu nayo has joined the team!.
A Way Forward
1. Kwa vile Chadema imefanikiwa kuwatimua hao 19 sasa Chadema isikate tena rufaa, kupinga uamuzi huu, bali iitishe kikao cha Baraza Kuu , ASAP, kifanye a due process, hili la wabunge 19 liishe, wabunge hao 19 wavuliwe ubunge wao, Chadema wapeleke majina 19 mengine, wateuliwe waapishwe, tuwe na Bunge la vyama vingi!.
2. Chadema wakifanya tuu dillydalling kukaa rufaa, inakula kwao!. By the time rufaa inasikilizwa, ndipo kifuate kikao cha Baraza Kuu, I'm afraid the time left before the next election is too little too late, ikibaki muda wa chini ya miezi 12 kabla ya muda wa uhai wa Bunge kuisha, hakuna uchaguzi wowote wala uteuzi wowote wa wabunge wapya!.
3. Tena nashauri kikao hicho cha Baraza Kuu, pia sasa ndio kimtimue Halima Mdee, kikifuatiwa Mkutano Mkuu kuthibitisha. Hapa najua changamoto ni fedha!, kule kwenye kile chungu, zilikopatikana zile fedha za kugharimia Baraza Kuu lile, kile chungu bado kipo, kitagharimia vikao vyote viwili, na Chadema inaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!.
Paskali.