Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?

haya mabo ya gender equality si yamekuwa initoated na hao hao wazungu? kama sio wao hata viti maalumu visingekuwepo,japo havisaidii
Hakuna siku wazungu wamelazimisha gende equality kama wanavyolazimisha kutambuliwa kwa mashoga. Hadi nchi zinawekewa sunction! Sijawahi sikia wakiweka sunctions kwa nchi isiyoheshimu haki za akina mama kama watakavyo. Ni unafiki tu! Wakifanya upuuzi ni maendeleo, Afrika tukifanya mila zetu eti ni kinyume cha haki.
 
hope it is proportional representation! ama 1:1 au 1:2 kutegemea na ratio yao.
 
Gender equality haikupata resistance kama la homosexuals, lilikubalika tu fasta, tz haijawahi kukubali ushoga tangia enzi za nyerere na haijawahi kuwekewa vikwazo kwa ajili ya hilo
 
Gender equality haikupata resistance kama la homosexuals, lilikubalika tu fasta, tz haijawahi kukubali ushoga tangia enzi za nyerere na haijawahi kuwekewa vikwazo kwa ajili ya hilo
Baada ya kuruhusu uvutaji bangi baadhi ya majimbo ya US, inakuja kulazimishwa kuruhusu kuvuta bangi ktk nchi zetu. Maana, naona kuna watu munaamini binadamu wa maana wako US na ulaya.

btw. ni nchi ngapi dunia hii ziliruhusu ushoga, miaka ya enzi ya Nyerere unayoitaja?
 
Hakuna haja hata ya awamu moja. Wanaume na wanawake wana usawa. Wabunge ikiwezekana tupunguze. Hivi kazi ya mbunge ni nini kwa utawala kama huu unaotenda makubwa miradi ya kimkakati.

So far mbunge hana kazi anayoifanya zaidi ya kwenda kulipwa pesa nyingi zinazokatwa sie wananchi wa kawaida.

Kinondoni kila mtaa sasa hivi unapigwa rami sababu serikali ilishaandaa mradi wa uendelezaji jiji la dsm Dmdp. Mbezi beach hakuna lami sababu labda haikuwemo kwenye maombi ya fedha toka kwa wahisani.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbona unarukia kwingine na kupindisha hoja, nimesema tz haijawahi kuwekewa vikwazo kisa kutokuruhusu ushoga, enzi za nyerere, mwinyi, mkapa hadi leo. yapo mambo mengi tu ambayo ynaruhusiwa Ulaya na USA kama vile utaoaji mimba lakini Tz haturuhusu na hayajawahi kusababisha kuwekewa vikwazo
 
Kama ulimaanisha hivyo, hukuandika hivyo. Soma unachoandika kabla ya kupost.
You wrote;
Gender equality haikupata resistance kama la homosexuals, lilikubalika tu fasta, tz haijawahi kukubali ushoga tangia enzi za nyerere na haijawahi kuwekewa vikwazo kwa ajili ya hilo
 
Tangia inamaana ya kuanzia kipindi kilichotajwa hadi kipindi cha sasa, haijalimit kwa hicho kipindi kilichotajwa tu.

Ni sawa na neno since kwa English Since meaning in the intervening period between (the time mentioned) and the present.
 
Yaelekea Makinda anasoma jf, hili aliliona humu
last week

Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?

Wanawake Tanzania ni Duni/Dhaifu Kiongozi , Kama Si Duni/Dhaifu na Wana Uwezo Sawa na Wanaume, Viti Maalum Vya Nini?

P
 
Mkuu Freddie Matuja, kwanza nimefurahi kwa reference yako ya Mhe. Lolensia Bukwimba, ni kweli mwanzo kwenye ule uchaguzi mdogo alitoboa kwa kubebwa na JPM, tena kampeni ziliendeshwa kwa lugha ya Kisukuma mwanzo mwisho, bila hivyo asinge toboa haswa kwa kuzingatia Wasukuma ni moja ya makabila yenye male chauvinism na kudharau wanawake. Lakini baada ya kuingia Bungeni, akajenga uwezo, 2010 na 2015 akasimama mwenyewe na akatoboa.

Hivyo Mama Makinda ana hoja ya msingi sana, lengo la viti Maalum liwe ni kujenga tuu uwezo kwa a single term, kisha waende jimboni na sio kubebwa na kuendelea kubebwa tuu!.
P
 
Hivi hao Wabunge wa viti maalumu wanatija gani kwa Taifa? Mimi nashauri wangefutwa tu wabaki wa kuchaguliwa.
Wanatoa hoja mjarabu,mfano mmoja alitaka zifungwe machine za kupima nini sijui za wanaume wasiotahiliwa Ila hitimisho hakutoa,kimsingi bado sana.
 
Kwa nini usifutwe?
Lengo lilikuwa kuonyesha njia ba kuwashirikisha wanawake katika kutunga sheria na kuisimamia serikali.

Labda mnisaidie lengo lililobaki kwa viti ba viti vya rais ambavyo kimsingi vinaficha madudu ya wabunge WA majimbo, kwa kuwa wengi hawazungumzi katika vikao vingi vya bunge na wapo wapo tu.
Mnisaidie, maana sasa mnajadili kuwawekea ukomo na wakati takwimu nyingi zinaonesha tayar wanawake ni 75% katika uchumi inashindikana nini kwenye siasa? Hasa uchaguz maana lengo lilikuwa kubadilisha mind set ya jamii juu ya wanawake katika maamuz
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo siku ya wanawake duniani, vipi wabunge hawa waendelee kubebwa?.
P
 
Wajameni, kama uwezo wa kujieleza wa baadhi ya wabunge wanawake wa viti maalum ndio huu!.
Bora hivi viti vifutwe!.
P
 
View attachment 1365325

Yani hawa wanawake wanao pewa ubunge wa upendeleo wanamaliza hela za walipa kodi bure kabisa, Kwenye bunge letu wapo 113 wanakula mishahara na posho za bure, kazi yao kusifu juhudi na kuwapamba viongozi wa vyama vyao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…