Je, wajua kazi zinazofanywa na wanawake zingetengeneza nusu ya ajira?

Je, wajua kazi zinazofanywa na wanawake zingetengeneza nusu ya ajira?

Mema Tanzania

Member
Joined
Feb 23, 2020
Posts
66
Reaction score
65
Wanawake nchini Tanzania hutumia wastani wa zaidi ya masaa 6 kwa siku kufanya kazi zisizokuwa na malipo kama kupika, kuchota maji - ukilinganisha na masaa 3 tu wanayotumia wanaume. Kama kazi wanazofanya zingegeuzwa kuwa za malipo zingetengeneza zaidi ya nusu ya ajira zilizopo. #IWD2020 #EachforEqual

IWD Did You Know.png
 
View attachment 1375365
Kwa hiyo una maanisha mke wako akikupikia chakula anatakiwa alipwe?

NB: naona hapo umeandika eachforequal, huko beijin patawamaliza nyie akina dada. Hatuwezi kuwa sawa, thats nature.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama asilimia 97 ya wanaume wa Afrika wanafahamu kwa nini wanaoa, endapo wanaume wanaoa wanawake kwa sababu ya kupika basi huo ni utumwa.

#IshiKijanja #KaaKijanja
 
Sasa naelewa kwann kulikuwa na koo walikuwa hawana time na kumuelewa au kuendeleza mawazo ya mwanamke.

Wanawake mpo so selfish, yaani mnajiona nyie ndio viumbe ambao mnashikilia mzunguko wa dunia na wanaume hakuna wanalofanya.....

Mwanzo nilikuwa advocate mzuri sana wa kutetea masilahi ya wanawake ila kwasasa naona hawa viumbe kuwapa sauti ni kuifelisha jamii maana kila sehemu wanahisi wanaonewa.....

Sasa hivi kweli mtu ana question roles zake.... Haya na sisi wanaume tukitaka kulipwa kwa kuwahudumia hivi kuna mwanamke ataweza kulipa gharama yake....?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je unafahamu majukumu ya mwanamke kwenye ndoa yanatofautiana kutokana na utamaduni wa sehemu husika?
Hii yote sababu kutokuwepo kwa elimu! Leo hii Maria Sarungi na Asha wa buza hawawezi kuwa sawa - Tupo hapa kumfanya Asha wa buza aache kuweka miguu katika makochi akichunguza chungu jikoni.

#EachforEqual
 
Je unafahamu majukumu ya mwanamke kwenye ndoa yanatofautiana kutokana na utamaduni wa sehemu husika?
Kama shida ni tamaduni! Fanya yafuatayo: 1. Anza kuabudu magome na mawe. 2. Vaa magome, majani na ngozi. 3. Choma vyeti vyako vyote na usisomeshe mtoto shule. 4. Rudi kijijini ukachunge ng'ombe

Hii ndio tamaduni, au unasemaje?
 
Samcezar,
Tatizo ni uelewa uliopo katika jamii! Nawasilisha elimu ifahamike ya kuwa sio mwanamke pekee mwenye jukumu la kufanya shughuli za kifamilia hata wewe ni jukumu lako.
 
Wanawake mnataka nini? Hamuwezi kuwa wanaume, wanaume hawawezi kuwa wanawake, hakuna kitu kinaitwa haki sawa kwenye majukumu. Kuna majukumu ya mwanamke na mwanaume, usawa unaonekana pale kila mmoja anapofanya majukumu yake kwa usahihi.
 
Back
Top Bottom