Wanabodi,
Kuna vitu mimi huwa navisema humu na watu wanavichukulia poa, ila vikija kutokea ndipo wenye uelewa wanaanza kuelewa nilikuwa nazungumzia nini.
Hivi ni baadhi ya vitu nilivyovisema na kweli vikaja kutokea
- Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
- Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums
- Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii - JamiiForums
- Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG? - JamiiForums
- Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba - JamiiForums
Sasa ninachokisema leo ni kuwa sio wengi wanajua kuwa hatma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Wilfred Lwakatare?. Chadema imepakua ugali kwa kila mtu kupewa ugali kwenye sahani yake, Kamati Kuu ya Chadema, wakaamua kuipindua sahani ya ugali wa Lakwatare, na kuumwaga ugali ili Lwakatare asile, huku wengine wote wakiwa na ugali wao kwenye sahani zao, wakisubiri bakuli la mboga litetwe, huku haku mwenye kumbukumbu ni nani aliyetumwa jikoni kwenda kuleta bakuli ya mboga, watu wapakuliwe ndipo wale!.
Mara aliyeibuka jikoni na bakuli ya mboga ni Mhe. Wilfred Lwakatare!, Amelishika bakuli la mboga za moto kwa mikono yake, huku mikono yake inaungua lakini amestahimili na kuvumilia huku akitokwa machozi, jasho na damu, kwa ajili ya Chadema!. Kabla hajalitua bakuli la mboga ili watu watu wapakue wote wale, akandua kuwa ugali wake umemwagwa!.
Wakati wanamwaga ugali wake, hakuna aliyekumbuka kuwa anayesubiriwa kuleta mboga watu wale ni Lwakatare, hivyo sasa wote wamenyamaza kimya kusubiria Lwakatare, atafanya nini baada ya kubaini Chadema wamemwaga ugali wake, huku mwenye bakuli ya mboga ni yeye!, sasa hatima ya kama Chadema watakula ama hawali, ikomikononi mwa Lwakatare, baada ya wao kumwaga ugali, Lwakarare akiamua kumwaga mboga, then wanakosa wote!, Chadema ndio inakuwa kwishney!.
Ili uelewa mimi nazungumza nini, ni lazima kwanza ukijue kisa, ambacho ndio bakuli ya mboga.
Kisa chenyewe ni hiki.
Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare - JamiiForums
Chadema ni chama cha ajabu sana!, kuna watu unaweza kuwatimua lakini sio Lwakatare, na sababu ni moja tuu, ameipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu!.
Chadema inapaswa kumyenyekea Lawakatare na kwasababu aliishatangaza kustaafu, Chadema walipaswa kumuacha tuu astaafu kwa amani, haswa kwa kuzingatia wamemfukuza wakati ambao Bunge hili limebakiza wiki3 tuu limalizike rasmi.
Umuhimu wa Lwakatare kuachwa tuu hata afanye nini au aseme nini, ni kumzuia asije kufungua mdomo wake!.
Ikitokea Lwakatare akaamua kufungua mdomo wake na kuyataja madudu ya ajabu Chadema inayoyafanya nyuma ya pazia, ikiwemo ile video mimi niliyoita hapo kuwa "bonafide genuine", Chadema Watakuwa mgeni wa nani?.
Mtu kama Lwakatare anafukuzwaje?.
Kufuatia hiyo video niliyoitaja kule juu, nilipokuta na Msajili wa vyama alisema
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...! - JamiiForums
Sasa hiyo endapo katika bandiko hilo, ndilo bakuli la mboga, Lwakatare amelishikilia, licha ya yeye kunwagiwa ugali wake, anaweza kuamua yeye ndio akose na kulala njaa, hivyo atalitua tuu hilo bakuli la mboga na wengine wote wale, na yeye tuu ndio akafie mbele, ila akiamua kuonyesheana ubabe, na mambo yanakuwa ni ubabe ubabe tuu, maadamu wamemwaka ugali, na yeye anamwaga mboga...
yatakuwa mengine!.
Lets keep watching tukisubiria Lwakatare ataamua nini, ila amini usiamini, hatima ya Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Lwakatare!, kubali, kataa!.
Paskali
P.