Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!

Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!

Mkuu kwa hao wachangiaji wa Chadema unaona kuna chama hapo? Chadema kimeishakufa, wao wanadai haijafa. Wabunge zaidi ya ishirini wameondoka au wamefukuzwa. Madiwani zaidi ya mia wameondoka. Viongozi wa Wlaya, Mikoa na Kanda wameondoka. Wao wapo nyuma ya keyboards zao eti Chadema haifi! Sawa, hata Mzee Rungwe yupo na chama chake hakijafa!
Sasa Kama kimeshakufa kwanin unahangaika nacho yaan unahangaika na marehemu serious
 
Pascal tangu aseme amejiunga na CCM hata thinking capacity yake imekuwa low sana. Analeta issue ambayo mahakamani walishindwa kuithibitisha? Ila kweli mayala mbaya sana.
Tuache kuongozwa na mahaba ya kitoto na wingi wa maandishi, Pascal nakuhehimu sana na ukweli unaujua, CHADEMA is there to stay, mark my word, hata akiondoka Mbowe, hakuna wa kuimaliza CHADEMA na unaujua ukweli.

Kuandika kwa kirefu sana na reference za thread ambazo mwandishi ni wewe mweyewe hakusaidii chochote kile ndugu yangu. aliondoka Zito mkaandika weeee, akaondoka Slaa mkachonga sana, lakini pata picha ya uchaguzi serikali za mitaa mwaka jana, wote tunajua nini kilitokea. Tusijidanganye wala kujifariji kwa mambo ya kitoto. Tujadili issues muhimu. Chadema IFE huku mnamuogopa Mdude Chadema? Hahhahaahaha

Leo hii Wapinzani wametoka Bungeni, Bunge zima limewageuza kuwa mjadala! Why? kwasababu wako strong. kwasababu uwepo wao una mtetemo mkubwa. Tusijifungie Dar na kuandika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe uelewa wako ni mdogo sana nenda kasome anguko la NCCR lilikuaje. Chadema sasa imebaki na wabunge 15 toka 60+ huoni ni anguko la kasi ya ajabu subiri bunge livunjwe 30/06/2020.
Hao wabunge walioondoka ni wangapi? Hebu wataje hapa tujue idadi yao na sio porojo tu.
Kama CDM imekufa,mbona mnahangaika nayo kila siku? Hata press ya chadema tu inawatisha
 
Hakuna kitu hapo bali propaganda kutafuta huruma kwa watawala. Kama CHADEMA haijafa baada ya Dk Slaa na haijafa miaka 5 bila siasa na haijafa kwa bunduki na mabomu na jela na mapanga na jela, ni nani wa kuipoteza CHADEMA? Lwakatare sisimizi ndo aipoteze CHADEMA? Kweli ww njaa imekupanda kichwani kama lilivo jina lako.


Chadema ni imani, chadema sio majengo...chadema iko sisiemu...chadema iko kwenye utawala.
Ukabila umempofusha kawa mjinga kuliko wale wapiga vigeregere wanaolipwa na chakubanga
 
Kama Chadema inakufa kweli, kama tuna uhakika na hili basi turuhusu yafuatayo
Tuwe na Tume huru, Tuwe na Wasomamizi huru, tuwe na Free and Fair campaigns, Jeshi la Polisi lisijihuishe na siasa kama ilivyo sasa, kuwe na Katiba huru (wenye akili wameelewa), turuhusu mikutano ya siasa. hayo machache tu. Then baada ya hapo turudi tukae mezani tuone kama inakufa au inaishi
Mkuu, achana na hawa wapiga ramli wa Lumumba.
Hizi ramli sio mpya,ziliasisiwa na mzee Wasira
 
Nipetia comment nyingi hapa naona wengi wamemnanga paskali,mimi najua paskali atapita ila haya maandishi yake yatabaki,kama yatatokea tuwe na utamaduni wa kurudisha nyuzi za nyuma zenye kumbukumbu za yale mapovu yenu!
 
Wanabodi,
Kuna vitu mimi huwa navisema humu na watu wanavichukulia poa, ila vikija kutokea ndipo wenye uelewa wanaanza kuelewa nilikuwa nazungumzia nini.

Hivi ni baadhi ya vitu nilivyovisema na kweli vikaja kutokea
  1. Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
  2. Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam - JamiiForums
  3. Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii - JamiiForums
  4. Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG? - JamiiForums
  5. Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba - JamiiForums
Sasa ninachokisema leo ni kuwa sio wengi wanajua kuwa hatma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Wilfred Lwakatare?. Chadema imepakua ugali kwa kila mtu kupewa ugali kwenye sahani yake, Kamati Kuu ya Chadema, wakaamua kuipindua sahani ya ugali wa Lakwatare, na kuumwaga ugali ili Lwakatare asile, huku wengine wote wakiwa na ugali wao kwenye sahani zao, wakisubiri bakuli la mboga litetwe, huku haku mwenye kumbukumbu ni nani aliyetumwa jikoni kwenda kuleta bakuli ya mboga, watu wapakuliwe ndipo wale!.

Mara aliyeibuka jikoni na bakuli ya mboga ni Mhe. Wilfred Lwakatare!, Amelishika bakuli la mboga za moto kwa mikono yake, huku mikono yake inaungua lakini amestahimili na kuvumilia huku akitokwa machozi, jasho na damu, kwa ajili ya Chadema!. Kabla hajalitua bakuli la mboga ili watu watu wapakue wote wale, akandua kuwa ugali wake umemwagwa!.

Wakati wanamwaga ugali wake, hakuna aliyekumbuka kuwa anayesubiriwa kuleta mboga watu wale ni Lwakatare, hivyo sasa wote wamenyamaza kimya kusubiria Lwakatare, atafanya nini baada ya kubaini Chadema wamemwaga ugali wake, huku mwenye bakuli ya mboga ni yeye!, sasa hatima ya kama Chadema watakula ama hawali, ikomikononi mwa Lwakatare, baada ya wao kumwaga ugali, Lwakarare akiamua kumwaga mboga, then wanakosa wote!, Chadema ndio inakuwa kwishney!.

Ili uelewa mimi nazungumza nini, ni lazima kwanza ukijue kisa, ambacho ndio bakuli ya mboga.
Kisa chenyewe ni hiki.
Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare - JamiiForums

Chadema ni chama cha ajabu sana!, kuna watu unaweza kuwatimua lakini sio Lwakatare, na sababu ni moja tuu, ameipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu!.

Chadema inapaswa kumyenyekea Lawakatare na kwasababu aliishatangaza kustaafu, Chadema walipaswa kumuacha tuu astaafu kwa amani, haswa kwa kuzingatia wamemfukuza wakati ambao Bunge hili limebakiza wiki3 tuu limalizike rasmi.

Umuhimu wa Lwakatare kuachwa tuu hata afanye nini au aseme nini, ni kumzuia asije kufungua mdomo wake!.

Ikitokea Lwakatare akaamua kufungua mdomo wake na kuyataja madudu ya ajabu Chadema inayoyafanya nyuma ya pazia, ikiwemo ile video mimi niliyoita hapo kuwa "bonafide genuine", Chadema Watakuwa mgeni wa nani?.
Mtu kama Lwakatare anafukuzwaje?.

Kufuatia hiyo video niliyoitaja kule juu, nilipokuta na Msajili wa vyama alisema
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...! - JamiiForums

Sasa hiyo endapo katika bandiko hilo, ndilo bakuli la mboga, Lwakatare amelishikilia, licha ya yeye kunwagiwa ugali wake, anaweza kuamua yeye ndio akose na kulala njaa, hivyo atalitua tuu hilo bakuli la mboga na wengine wote wale, na yeye tuu ndio akafie mbele, ila akiamua kuonyesheana ubabe, na mambo yanakuwa ni ubabe ubabe tuu, maadamu wamemwaka ugali, na yeye anamwaga mboga...
yatakuwa mengine!.

Lets keep watching tukisubiria Lwakatare ataamua nini, ila amini usiamini, hatima ya Chadema, iko mikononi mwa Mhe. Lwakatare!, kubali, kataa!.

Paskali
P.
Tatizo hata akija alisema Chadema Ni chama Cha Ibilisi, akaleta na Picha hatumwamini...Huu ndio msingi wetu!😋😋
 
Wengine tunajua mapungufu ya sasa ya Chadema lakini hatukutegemea Mbowe kuamua kumpoteza Rwakatare kiurahisi.

Shortly Chadema ni sikio la kufa ... kama tulivyosema kabla ya uchaguzi 2015 tusubiri baada ya 2020 tutarudi hapa na hadithi mpya na chama kikuu kipya cha upinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema imejaa mashabiki ambao uamini kila linalofanywa na viongozi wao ni sahihi wakati wakibeza kuondoka kwa Dr Slaa wanajifanya hawaoni pengo lake maya zaidi wale waliowaamini na kuwapokea toka CCM wamesharudi walikotoka tunapizungumzia kufa kwa chama hatumaanishi kitatoweka bali kitakuwepo lakini si kwa nguvu iliyokuwepo awali
 
Mkuu uko sawa 100%, inaonekana unaona mbali sana. Tunaomba tuambie na hili ambalo la kitaifa zaidi kuliko hilo la kikundi cha watu.

Inasemekana koona haiishi leo au kesho, je huko burigi atarudi au atakaa huko huko hata miaka 3 mpaka iishe?
 
Mamlaka ya Uteuzi hakika haitendi haki kwani kwa jinsi Pasco, anavyoifagilia Serikali ya Magu, basi alipaswa apewe nafasi ya "Msemaji wa Serikali".....

Mkuu Mayala, punguza kujikomba na acha Kujinafikisha kwani JIWE, hana time na wewe....

Lakini pia kumbuka CHADEMA si viongozi bali ni Watanzania tulioichoka CCM na ndo maana Mtu kama Mdude Chadema, ni tishio kwa Mteuzi na CCM yote kwa ujumla !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom