Je, wajua kuwa idadi ya wapiga kura nchini inakaribiana sana na idadi ya watu wenye kutumia mtandao (internet)?

Je, wajua kuwa idadi ya wapiga kura nchini inakaribiana sana na idadi ya watu wenye kutumia mtandao (internet)?

Teh teh teh, chukua mkutano wowote aliofanya Magufuli sehemu yoyote, then, angalia aina ya watu wanaohudhuria halafu utapata majibu kama wanna access na mitandao au hawana.
Hizo polls zinazofanywa na watu obviously matokeo yake yatategemea muelekeo wake. Unajua Nini kitatokea kwenye Poll iliyoanzishwa na Fatuma Karume au Maria Sarungi kwa sababu 90% ya wafuasi wake ni wale wanaopendezwa na misimamo yake.
Matokeo yatakuwa hivo hivo kwenye page ya Gerson Msigwa, Antony Mavunde au Hamis Kigwangala.

So acheni kujipa matumaini bure, angalieni Population anayopata Magufuli tena barabarani na kwenye vimiji vidogo, angalia aina ya watu wanaokwenda kwenye mikutano ya Magufuli na wale wanaokwenda kwenye mikutano ya Loketo utaona tofauti.

Mmoja ana wapiga kura, mwingine ana wafuasi.
Unafurahisha..mwambie G.Msigwa au HK au H.Polepole aitishe POLLs kwenye account yake... Af utarudi kutupa majibu.
 
Kabisa mkuu! Sasa mtu unaanzisha polls kwenye group la Maria Sarungi unategemea upate matokeo gani?
Wakati huyo dada hatofautiani na Mange kwamba ukimchallange anakupiga ban?
umeambiwa uende kwenye post ya mwisho aliyoposti magu twita uone jinsi ambavyo hujui
 
Teh teh teh, chukua mkutano wowote aliofanya Magufuli sehemu yoyote, then, angalia aina ya watu wanaohudhuria halafu utapata majibu kama wanna access na mitandao au hawana.
Hizo polls zinazofanywa na watu obviously matokeo yake yatategemea muelekeo wake. Unajua Nini kitatokea kwenye Poll iliyoanzishwa na Fatuma Katume au Maria Sarungi kwa sababu 90% ya wafuasi wake ni wale wanaopendezwa na misimamo yake.
Matokeo yatakuwa hivo hivo kwenye page ya Gerson Msigwa, Antony Mavunde au Hamis Kigwangala.
So acheni kujipa matumaini bure, angalieni Population anayopata Magu tena barabarani na kwenye vimiji vidogo, angalia aina ya watu wanaokwenda kwenye mikutano ya Magu na wale wanaokwenda kwenye mikutano ya Loketo utaona tofauti.
Mmoja ana wapiga kura, mwingine ana wafuasi.

Binafsi watu wanaotabiri ushindi wa Tundu Lissu naona kama hamnazo hivi, Hivi Lowasa na Lissu nani anapata Mafuriko? Mashinery ya Lowasa ilikuwa na nguvu sana kuliko ya Lissu na kikubwa zaidi Lowasa alikuwa anavuka kwenye mistari ya vyama,makundi ya watu na itikadi mbalimbali, pia Mtizamo wa Watu wengi kwa Lowasa sio kama Lissu anavyoonekana wakala wa Kibeberu, Uwepo wa Barua na matamko mbalimbali toka nje ya nchi kwa maslahi ya Lissu unazidisha mashaka kwa watu wengi, Kimsingi wanajitekenya na kucheka wenyewe kama vile walivyokuwa wanafanya wakati wa kumshabikia Mende ihali wakijua hachaguliki!!

Majuzi nilikuwa naongea na jirani yangu na mkewe, jirani yangu ana msimamo mkali sana wa kichadema, anamchukia sana Magufuli pamoja na mafanikio aliyonayo kupitia kazi yake serikalini bado ni Hater sana. Wakati yeye hamtaki Magufuli lakini mkewe anamsapoti kiaina huku akiogopa kumuudhi Mume, na hawa ni wengi na ujisifia kuwa wao na familia zao watapigia CHADEMA.

Kura ni siri na huwezi hata siku moja ukajihakikishia kura YA MTU MWINGINE, Usiisemee, Jambo la mwisho, CCM ina wanachama wangapi? Hawa ndio mtaji wake kuna underground movement ya ushindi Wao wanahangaika na kelele za mitandaoni.
 
Soma kwa umakini nilichoandika

uzoefu unaonyesha watu hutumia laini tofauti kwa voice na si data.

Watumiaji ni loyal sana kwenye laini yao ya data unless mpaka mtandao husika upandishe gharama ziwe juu mno kulinganisha na wadau wengine.

Ila kwenye voice, watu hubadilibadili laini kulinfana na watu wanaowasiliana nao

Kwa hiyo hoja ya kuwa na laini nyingi, haina mashiko kwenye matumizi ya Internet, ila inaweza kuwa na mashiko kwenye voice.

Sababu nyingine kwa nini watu wanaotumia data wako loyal kwa laini moja kwenye ishu ya data ni kwa sababu wengi wamebind namba yao ya simu na social apps kama vile Whatsapp, authentication inafanyika kwa namba ya simu, wakitaka kuhamisha info zao za whatsapp kwenda laini nyingine lazima ziwe authenticated na laini yao ya zamani kwa kutumiwa sms kwenye namba hiyo. Kwa hiyo kimsingi watu wengi wana app moja ya Whatsapp kwenye simu iliyosajiliwa kwa laini moja na si app zaidi ya hiyo.

So kwenye voice, yes inamake sense kuwa na laini nyingi, ila kwenye data ambayo ndo msingi wa mada hii, watu wako loyal sana na laini moja!
 
Wewe kijana usituletee uongo hapa, hivi unadhani hii mitandao ya kijamii au hizi smart phone zinamilikiwa watanzania wengi? Kwa taarifa yako wanaotumia mitandao ya kijamii kati ya 30% na 35% ya wapiga kura. Kwa mfano huku mijini sio wote Wana hizo smart phone au laptop, kijijini ndio kabisaaa.
 
Gazeti la Nipashe tu ndio linafuatilia na kuandika kwa kina kampeni za Lissu..mengine yote wanaogopa..Dawa yao kutoyanunua
 
Wewe kijana usituletee uongo hapa, hivi unadhani hii mitandao ya kijamii au hizi smart phone zinamilikiwa watanzania wengi? Kwa taarifa yako wanaotumia mitandao ya kijamii kati ya 30% na 35% ya wapiga kura. Kwa mfano huku mijini sio wote Wana hizo smart phone au laptop, kijijini ndio kabisaaa.

Img-1600638456520.jpg
 
Tafadhali mie sikubaliani na hizo data, labda uniambie watumiaji wa simu na sio internet. Ni kweli watumiaji wa simu ni zaidi 23 milioni kwa sababu. Population ya Tanzania ni 60 Milioni kati ya hao 20 Milioni ni watoto kati ya mwezi mmoja na miaka 15 ambao ni wachache sana access internet. Kwenye 60 Milioni 60% - 70% wanaishi vijijini ambao wenye access ya mitandao hawazidi hata 40%. Kwa hiyo wewe mtu akiweka data zake basi unaamini 100%. Tafadhali la kuambiwa na wewe changanya na ubongo wako. Acha uvivu wa kutafakari mambo.
 
Hakuna mtanzania mwenye line moja ya simu. Wengine wana line mpaka 5 kila mtandao!! Hata maandamano ya Mange yalikuwa mtandaoni hivyo sioni cha ajabu. Bila kusahau wapiga kura za maruhani kwenye utabiri wenu feki!! Subirini mziki wa tarehe 28 Oct!! Msiseme mmeibiwa!! Endeleeni na kampeni zenu za mjini wakati wapigakura wapo vijijini!!

Nashauri mgombea mwenza wa Lissu apambane sio anabebwa kama demu!

Queen Esther
Kitu usichokijua ni kuwa nusu ya wananchi wa vijijini hawapigi kura wamechoka na hawana matumaini kuwa kura yao inaweza kuwasadia chochote ktk maisha yao.

Ila kwa wanaoishi mijini asilimia 80 hujitokeza kupiga kura hali inayopelekea uchaguzi ujao kuwa mgumu sana.

Zamani asilimia kubwa ya watu wa mijini walikuwa hawapigi kura ila leo ni kinyume na zamani asilimia kubwa ya wananchi wa vijijini walikuwa wanapiga sana kura lakini leo hii ni kinyume kabisa.
 
Tafadhali mie sikubaliani na hizo data, labda uniambie watumiaji wa simu na sio internet. Ni kweli watumiaji wa simu ni zaidi 23 milioni kwa sababu. Population ya Tanzania ni 60 Milioni kati ya hao 20 Milioni ni watoto kati ya mwezi mmoja na miaka 15 ambao ni wachache sana access internet. Kwenye 60 Milioni 60% - 70% wanaishi vijijini ambao wenye access ya mitandao hawazidi hata 40%. Kwa hiyo wewe mtu akiweka data zake basi unaamini 100%. Tafadhali la kuambiwa na wewe changanya na ubongo wako. Acha uvivu wa kutafakari mambo.

Sasa wewe unajitungia data zako kichwani unabishana na data za TCRA.

Hata hivyo vijiji unavyovisema, siyo kama vijiji vya zamani, siku hizi watu wanaingia kwenye mtandao kama kawa
 
Miaka yote huwa mnasema ccm inatumia mabavu kushinda uchaguzi kwamba kukiwa na tume huru basi ccm inatoka madarakani kwa maana watu hawaipendi na wameichoka ccm,na kila uchaguzi upinzani unashinda ila ni vigisu tu za ccm.
 
Watumishi wa serikali huko mikoani wanapigwa mkwara wahudhurie mikutano ya Magufuli.
Wakuu wa shule wanalazimishwa kufunga shule na kuwataka watoto wa shule wavae nguo za nyumbani na waende kwenye mikutano ya Magufuli
Mara watumishi wa serikali mara wanafunzi mara watu wanabebwa kwenye lori mara watu wanafuata wasanii wa muziki.
 
Kabisa mkuu! Sasa mtu unaanzisha polls kwenye group la Maria Sarungi unategemea upate matokeo gani?
Wakati huyo dada hatofautiani na Mange kwamba ukimchallange anakupiga ban?
Kumbe nae ana tabia hiyo ya kupiga watu ban?
 
Tena wanasombwa kutoka kila mahali kwa mabasi, watumishi wa umma wanalazimishwa kuhudhuria na tena wakishaingia kwenye hadhara ya mheshimiwa wanafungiwa kama mbuzi hawawezi kutoka tena kuendelea na shughuli zao, maana wakijaribu kutoka wanakutana na maaskari wanawazuia.

Halafu wananchi wanapewa chambo ya kwenda kuwaona wasanii wakubwa wakiperform.

Ukichunguza Interaction ya Magufuli na hadhira yake ni very poor, watu hawashangilii punchlines zake, yaani umma uko baridiiii, unachangamka tu ikiwekwa burudani ya msanii

Wakati kwenye mihadhara ya Lissu, watu wanakuja kwa utashi wao
Pili kuna atmosphere ya Umma kuinteract naye vyema na kuzifurahia points zake.
Hakuna wasanii wakubwa wa kuvuta hadhira.

It seems kuwa Licha ya kwenda kwenye mikutano ya Magufuli ambayo inaboa, miongoni mwa wananchi wengi tu waliolazimishwa au kupewa chambo ya kuhudhuria mikutano ya Magufuli, wengi watamkubali Lissu kwa kuwa anaongea masuala yao ya msingi.
Mkuu huu ndy ukweli wa mchana na usiku. Kukubalika na watu hii ndy definition halisi. Lissu mikutano yake inahamasa na furaha wakati kule nyuso za wananchi wengi zmejaa simanzi wakati mwingine hawa wananchi huenda wanaenda kushangaa...mtu aliewanyima furaha kwa mda wa miaka 5 je ni yule?
 
Hao milioni 23 wanaofatilia siasa hawazidi milioni tano wengine wako busy kwenye mambo yasiyohusiana na siasa kama umbeya, mpira, insta, WhatsApp na mengineyo hivyo takwimu za internet kwa Tanzania bado hazitoi picha halisi
 
Kwahiyo mkuu kwa akili yako ccm wenyewe hawana watu ambao hawaendi mikutano ila wataipigia kura?
Hawana watu wanaokoment mitandaoni ila watawapigia kura?


Katika watu wenye wapiga kura silent kilker ni ccm!

Yani ccm ina wapiga kura aina flani hivi ni wapole hawana mihemko huwezi kuwakuta popote wamebeba vibendera wanakimbizana na pikipiki njiani. Wakati nyie mnahangaika mikutanoni wao huwa wako tu nyumbani wanamsikiliza Dida au wanapika au wako shambani huko wanalima, au wako madukani humo wanajitafutia riziki.

Ni aina flani hivi ambao mjumbe wa ccm akiwapitia majumbani kuwambia jambo flani mfano kuandikisha wapiga kura wanaitikia kwa wingi tena huwa wa kwanza kufika vituoni.

Chadema na wapinzani wengine daima wapiga kura wao wapo jf, Twitter kuhanikiza kwa kelele ambapo mmoja utamkuta mtwara, mwingine arusha, nk.

Huwezi kuishinda ccm kwa kutegemea maoni ya watu wa mitandaoni.
Chadema inasifika sana kuwa na wanachama vijana, wenye exposure, elimu na wapenda mabadiliko na ukiona hali mtandaoni ina onesha uhalisia uliopo katika jamii...


Na hili kundi kuna wakati halihitaji sana kwenda kwenye mikutano ili kuaccess taarifa..tunasoma Ilani kwa mtandao...tunaangalia hotuba kwa mtandao...tunasoma na kupima sera za wagombea na tunafanya analysis ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi ambayo tunaamini ni sahihi ..

Lakini lipo group ambalo pia linafanya maamuzi kulingana na peer pressure hususani vijana chipukizi.....ambalo pia ni mtaji wa Chadema..

Wapo watu walioumizwa na serikali hii either direct au indirect....ambao pia wanadeviate katika group ulilosema hapo juu...

Elimu ya Uraia kwa sasa hata vijijini ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo baadhi ya watu walikuwa wanajua Nyerere bado yupo..


Last week nilikuwa kijiji fulani nikachokpoza mjadala fulani nilishangazwa sana na uelewa walio nao wale wananchi na mazingira wanayoishi havilingani...yaani ukimkuta mtu anatetea CCM au CDM anatetea kwa hoja....

Kingine hili ni kundi ambalo hatutegemei kuchagua mbunge ili atuletee maendeleo bali atunge na kutetea sheria zitakazowezesha maendeleo(enabling environment)...maendeleo binafsi tunapambana nayo sisi wenyewe japo tunaangushwa na sera mbovu zinazodidimisha ustawi wa waajiriwa na wafanyabiashara ...ndo maana tunapenda watu wenye midomo kama Zitto...Lissu n.k who can speak out kwa niaba yetu na sio mabubu kama Abood ambao uwepo wao hausaidii .

CCM mtaji wenu ni wazee na ndo hao ambao generation yao inaisha na pia mnawanyima Mafao....mnaharibu biashara zao za Korosho....nk
 
Mkuu huu ndy ukweli wa mchana na usiku. Kukubalika na watu hii ndy definition halisi. Lissu mikutano yake inahamasa na furaha wakati kule nyuso za wananchi wengi zmejaa simanzi wakati mwingine hawa wananchi huenda wanaenda kushangaa...mtu aliewanyima furaha kwa mda wa miaka 5 je ni yule??

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app

Lissu anatisha kama njaa
 
Back
Top Bottom